Tafuta

Imechapishwa leo hii Dikrii kuhusu kanuni zinazotakiwa za Motu Proprio "Magnum principium"  kuhusu tafsiri ya vitabu vya kiliturujia vya Ibada ya Kirumi. Maaskofu ni wawajibikaji ili vitabu hivyo vitafisiriwe kwa lugha mahalia. Imechapishwa leo hii Dikrii kuhusu kanuni zinazotakiwa za Motu Proprio "Magnum principium" kuhusu tafsiri ya vitabu vya kiliturujia vya Ibada ya Kirumi. Maaskofu ni wawajibikaji ili vitabu hivyo vitafisiriwe kwa lugha mahalia. 

Dikri Magnum principium:Maaskofu ni wahusika wa tafsiri za vitabu vya kiliturujia

Mwenyekiti wa Baraza la kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti za Kanisa amefafanua juu ya Dikri ya Motu Proprio“Magnum principium”ambayo Papa Francisko amerekebisha mamlaka ya Baraza la Vatican na Mabaraza ya Maaskofu kuhusu tafsiri za vitabu vya kiliturujia vya Ibada ya Kirumi katika lugha mbalimbali.Jukumu la maaskofu ni kutafisri vitabu vya kiliturujia kutoka kilatino kuwa katika lugha mahalia.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Ibadan na nidhamu ya Sakramenti za Kanisa, akiwa katika studio za Vatican News, amefafanua juu ya Dikri au Hati ya Motu Proprio iliyotolewa leo  tarehe 21 Oktoba 2021, iitwayo ‘Magnum principium” yaani 'Msingu mkuu,' ambayo Papa Francisko amerekebisha mamlaka ya Baraza la Vatican na Mabaraza ya Maaskofu kuhusu tafsiri za vitabu vya kiliturujia vya Ibada ya Kirumi katika lugha mbalimbali. Haya ni mageuzi yanayotaka kuonesha dhima ya Mabaraza ya Maaskofu katika kazi kubwa kwa ajili ya mazungumzo na Kiti cha Kitume, ya kukamilisha kazi ngumu ya kutafsiri matini za kiliturujia za lugha ya Kilatino kuwa katika lugha ya Ibada ya Kirumi.

Askofu Mkuu Arthur Roche, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti  za Kanisa amethibitisha, kuhusu utekelezaji wa kanuni hiyo ya Motu proprio Magnum principium ya tarehe 3 Septemba 2017 ambayo Papa Francisko aliibadilisha Kanuni ya Sheria ya 838  ya Kanoni inayohusiana na tafsiri za vitabu vya kiliturujia katika lugha mahalia. Dikri au Hati iliyochapishwa  tarehe 22 Oktoba 2021 katika ukumbusho kiliturujia wa Mtakatifu Yohane Paulo II, inatafsiri na kuweka bayana taratibu za utekelezaji wa mabadiliko haya yanayohusu uwezo wa maaskofu na wa Jimbo ma na Baraza la Kipapa Vatican kufanya hivyo kwa ajili ya watu wa Mungu.

Hati hiyo (Dikri) yenye kichwa 'Postquam Summus Pontifex',  inakumbusha kwamba, kwa kuwa “jukumu kubwa katika jambo hili ni la Maaskofu, Baraza la Maaskofu lazima lilichukue wajibu moja kwa moja, likitumia ushirikiano unaohitajika wa watu wanaofaa, wakiwemo wataalam waliofunzwa katika tafsiri ya lugha ya Kilatino  ya kiliturujia. Kusudi lake ni kuhakikisha kwamba katika lugha fulani usemi sahihi na fungamani wa imani ya Kanisa Katoliki, inayopitishwa kulingana na mafundisho yake na msamiati unaofaa vinaeleweka kwa wote. Utambuzi na uthibitisho huo ni juu Baraza la Kipapa la Ibada na Nidhamu ya Sakramenti. Utambuzi huo unajumuisha marekebisho ya yale yaliyoidhinishwa na Baraza la Maaskofu na uhalali wa mchakato unaofuatwa kwa kuzingatia sababu zinazoamriwa na utamaduni, mapokeo ya nchi na mahitaji ya kichungaji. Uthibitisho huo ni katika uthibitisho uliotolewa na Makao ya Kitume kwa tafsiri ya maandiko ya Kibiblia na kiliturujia, baada ya kuhakikisha uhalali wa mchakato wa kukubaliwa na mabaraza ya maaskofu.

Katika barua ya Oktoba 2017 juu ya tafsiri sahihi ya Motu Proprio, Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amebainisha kuwa sheria mpya ya sasa inawapa Mabaraza ya Maaskofu kile kitivo cha kuhukumu uzuri na uthabiti wa tafsiri kutoka Kilatino, lakini pia ikiwa katika mazungumzo na Makao Makuu. Aidha alikuwa meeleza kwamba utambuzi huo unaonesha  uthibitisho tu na ulinzi wa utiifu wa sheria na muungano wa Kanisa ambao tangu wakati huo haupaswi kusababisha roho ya 'kulazimishwa kwenye Mabaraza ya Maaskofu ya tafsiri iliyotolewa na Baraza la Kipapa kwani hiyo ingedhoofisha haki ya maaskofu. Kwa upande mwingine alisema uthibitisho kwa hiyo haupendekezi tena uchunguzi wa kinaga ubaga wa neno kwa neno, isipokuwa katika kesi za wazi ambazo zinaweza kuwasilishwa kutoka kwa  maaskofu katika tafakari yao zaidi. Kwa njia hiyo kazi iliyopewa mabaraza ya maaskofu inawakilisha wajibu mkubwa kwa sababu, kutokana na tafsiri hizo, Neno lililofunuliwa linaweza kutangazwa na sala ya Kanisa inaweza kuoneshwa katika lugha inayoeleweka kwa watu wa Mungu.

Mkuu wa Baraza hilo akielezea miaka minne tangu kuchapishwa kwa motu proprio amesema uzoefu wake katika miaka ya hivi karibuni kama Katibu wa Askofu Mkuu na, kwa miezi ya hivi karibuni kama Mwenyekiti ni mzuri na unatajirisha. Katika kazi yao ya kila siku wanaona umoja wa Kanisa na, wakati huo huo, upekee wa kila Kanisa mahali , Maaskofu, kama wasimamizi, wahamasishaji na wasimamizi wa maisha ya kiliturujia katika Makanisa yao husika,wana usikivu mkubwa, unaotokana na malezi ya kitaalimungu na kiutamaduni, ambayo yanawawezesha kutafsiri matini za Ufunuo na Liturujia katika lugha inayoitikia tabia ya Watu wa Mungu waliokabidhiwa, ili kuwa, kadiri ya matakwa ya Baba Mtakatifu, chombo katika ibada ya Kanisa zima. Kwa hayo yote yanaweza kufupishwa kwamba kiini cha mabadiliko haya ni shauku ya kuwaleta Watu wa Mungu karibu na Liturujia na Liturujia kwa Watu wa Mungu!

MAELEZO YA MAGNUM PRINCIPIUM
22 October 2021, 17:39