Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu George Desmond Tambala O.C.D kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi. Papa Francisko amemteua Askofu George Desmond Tambala O.C.D kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi. 

Askofu Mkuu George Desmond Tambala, O.C.D, Jimbo Kuu la Lilongwe

Askofu George Desmond Tambala, O.C.D ameteuliwa na Papa Francisko kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe nchini Malawi. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule Tambala alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Zomba. Aliwahi kuwa ni mshauri wa Shirika la Wakarmeli, Makao makuu, mjini Roma. Askofu mkuu mteule alizaliwa kunako tarehe 11 Novemba 1968, Jimboni Zomba.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu George Desmond Tambala, O.C.D kuwa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Lilongwe nchini Malawi. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu mteule alikuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Zomba, Malawi. Aliwahi kuwa ni mshauri wa Shirika la Wakarmeli, Makao makuu, mjini Roma. Askofu mkuu mteule alizaliwa kunako tarehe 11 Novemba 1968, Jimboni Zomba. Baada ya masomo na majiundo ya kipadre na kitawa huko Enugu, Nigeria na Tangaza, Nairobi, akaweka nadhiri zake za daima tarehe 15 Agosti 1995 na kupadrishwa tarehe 13 Aprili 1996. Tangu wakati huo ametekeleza dhamana mbali mbali katika maisha na utume wa Kanisa kama Paroko msaidizi, Parokia ya Kapiri Jimbo kuu la Lilongwe, Malawi kati ya mwaka 1996 hadi mwaka 1998. Mwaka 1998 hadi mwaka 2000 alikuwa masomoni Hispania.

Baadaye akateuliwa kuwa ni mlezi wa Watakaji Kanda ya Wakarmeli, nchini Malawi utume alioutekeleza kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2002. Kunako mwaka 2002 hadi mwaka 2008 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika na Mwakilishi wa Shirika Kanda ya Malawi na Mkurugenzi msaidizi wa Kituo cha Tasaufi cha Mtakatifu Yohane wa Msalaba, Nyungwe-Blantyre, Malawi. Kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2015 akachaguliwa kuwa mshauri wa Shirika la Wakarmelitani, kwa ajili ya Afrika na Madagascar. Mwaka 2015 amekuwa ni mshauri mkuu wa Navarra, Malawi na Rais wa Shirikisho la Wakuu wa Mashirika ya Kitawa na Kazi za Kitume nchini Malawi.

Jimbo kuu Lilongwe

 

15 October 2021, 14:53