Tafuta

2021.10.25 Njia  za Moyo 2021.10.25 Njia za Moyo 

Afya ya moyo imefika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro!

Sio kwa mara ya kwanza kuona mfuko wa Kitume wa Kipapa unaonesha umakini juu ya afya ya watu maskini na watu wadhaifu wa kiuchumi na kijamii:Inakumbukwa hatua ya chanjo za kwanza dhidi ya UVIKO-19 kwa watu maskini na walio wadhaifu wa kijamii na sasa afya ya moyo ambacho ni kiungo muhimu katika maisha ya binadamu.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Njia za moyo:afya ya moyo imefika katika uwanja wa Mtakatifu Petro ili kuweza kupeleka chanjo ya kuzuia UVIKO kwa watu wadhaifu lakini pia haya upimaji wa moyo. Sio kwa mara ya kwanza hata hivyo kwamba Mfuko wa Sadaka ya kitume ya Papa inaweka umakini wa afya katika kuzuia magonjwa kwa watu maskini na wale ambao ni wadhaifu kiuchumi na kijamii. Kwanza ni chanjo dhidi ya UVIKO -19  na sasa wanajikita katika afya ya moyo kama kiungo muhimu cha maisha.

Tarehe 25 Oktoba 2021 mara baada ya mafanikio makubwa ya siku tatu katika Uwanja wa Risorgimento, Roma, ‘Hospitali katika Kambi’ imehamishiwa kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa kuwa na hatua maalum inayowezekana, shukrani kwa ushirikiano na Sadaka ya Kitume, Ofisi ya Makao Makuu Vatican ambayo inajikita katika kutoa msaada wa upendo kwa ajili ya maskini kwa niaba ya Baba Mtakatifu. Papa Francisko yuko, makini sana kuhusiana na mahitaji ya maskini zaidi hasa yanayohusiana na masuala ya kiafaya. Ni mipango mingi sana ambayo imeanzishwa kwa utashi wa Papa Francisko kwa mfano ya chanjo ya mshikamano, upimaji wa damu bure, upimaji wa mwili kwa ujumla kwa wale wote ambao hawawezi kufikia matibabu.

KLINIKI YA HUDUMA YA VIPIMO VYA MOYO KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO
KLINIKI YA HUDUMA YA VIPIMO VYA MOYO KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO

Ka njia hiyo katika uwanja wa Mtakatifu Petro kuna Cliniki inayotemba ambayo inafanya vipimi vya bure kwa ajili ya moyo na kupata ushauri wa madaktari humo humo bure kwa watu wote wenye kuhitiaji msaada huo hasa walio wadhaifu.  Kila mwaka nchini Italia karibia vifo 250,000 vinatokana na magaonjwa ya moyo na walio wengi ni magonjwa ya mishipa. Mnamo 2020 kutokana na dhaurur ya janga, idadi ya vifo kwa sababu ya kiharusi iliongezeka mara tatu kulingana na mwaka 2019(katika dada za kijamii za Italia kuhusiana na moyo), na mtu mmoja mwenye ugonja wa moyo kati ya wawili amejiwakilisha kupimwa kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka kwa Profesa Giuseppe Speziale, mratibu wa magonjwa ya moyo ya ‘GVM Care & Research’.

Kwa mujibu daktari huyo ameongeza kusema kwamba “GVM Care &amp Research”, ilianzishwa kutokana na ugonjwa wa mou ona katika kipindi hiki cha janga limeongeza zaidi kuweka umakini hasa katika mchakato wa kuzuia , kwa sababu ya kujechelewesha kwa janga limeongeza fasu nyingi za matatizo kwa watu wenye matatizo ya moyo au wale aliokuwa wako katika kusubiri. Kwa sasa wanajaribu kurudisha hali hii kwenye ukawaia wake lakini ni muhimu hata kuzungumzia kuzuia, kuwatia moyo katika kuzuia, na kufanya hata kwa kupitia njia hizi ambazo kwa kukatisha Italia inaguza mikoa mingi ambayo wamo na si tu bali kuweka umuhimu zaidi wa kuthibiti kawaida kwa afya ya moyo. Naye Kardinali Krajeewski, Mwenyekiti wa Sadaka ya Kitume ya Papa amewapelekea kikundi hiki cha madakatati Rosa ya ambayo ni zawadi ya Papa  kama ishara ya shukrani.

26 October 2021, 16:02