Tafuta

2021.09.11 Papa akiwa katika Kanisa Kuu la Bikira Maria mkuu katika sala kwenye Picha ya Salus Populi Romani tarehe 10-9-2021 jioni. 2021.09.11 Papa akiwa katika Kanisa Kuu la Bikira Maria mkuu katika sala kwenye Picha ya Salus Populi Romani tarehe 10-9-2021 jioni. 

Ziara ya kitume ya Papa Francisko:akabidhi Hungaria na Slovakia kwa Maria

Papa Francisko alikwenda Ijumaa jioni 10 Septemba katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Mkuu kama sehemu yake ya kawaida ya kukaibidhi ziara yake ya kitume katika moyo wa Ulaya kuanzia tarehe 12 hadi 15 Septemba.Akiwa katika Kikanisa kinachohifadhi Picha ya Maria aliweka maua na baadaye kukaa na kusali sala.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika kikanisa pembeni mwa Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria Mkuu kinachohifadhi Picha ya Bikira Maria (Salus Popouli Roman) na Mtoto mikononi mwake, wokovu wa watu wa Roma ambaye Papa Francisko amekuwa akimkabidhi kila wakati shida na hasa kabla ya ziara zake. Papa Francisko alikwenda  Ijumaa jioni ya saa moja, tarehe 10 Septemba 2021  akaweka shada la maua kwenye altare na baadaye kusali.

Papa akiwa anasali katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu
Papa akiwa anasali katika Kanisa Kuu la Maria Mkuu

Ni mama Maria ambaye atakongoza ziara yake ya kitume ya 34 katika moyo wa Ulaya kati ya nchi ya Hungeria na Slovakia na ikiwa kwa hakika ziara ya kiroho ambayo inaanzia na kuabudu Ekaristi huko Budapest na kuhitimisha kwa sala ya Bikira Maria wa Mateso Saba nchini Slovakia.

Kwa hakika Papa Francisko atawasili huko Budapest Jumapili asubuhi tarehe 12 Septemba kwa ajili ya  sherehe ya kufunga Kongamano la Ekaristi la Kimataifa na baadaye atahamia nchini Slovakia katika mji mkuu wa Bratislava, na tena miji mingine ya Prešov, Košice na mwishowe Šaštin ambapo ataadhimisha Misa ya kuhitimisha katika madhabahu  ya kitaifa ya Bikira Maria iliyotolewa sasa ni  miaka 250 iliyopita na ambayo kiutamaduni wa watu inaitwa Mama Yetu wa Mateso saba. Kuanzia hapo tarehe 15 Septemba 2021 atarudi Roma mapema , kwa mujibu wa taarifa za msemaji wa vyombo vya habari Vatican alifahamisha kuwa sala hiyo ilikuwa ni katika maandalizi ya hija yake ya kitume kama ilivyo kawaida yake kabla ya kwenda na baada ya kurudi.

11 September 2021, 12:08