Tafuta

Papa Francisko wakati wa Misa ya liturujia ya kibizantino  Prešov nchini Slovakia amesema msalaba"Hauna faida yoyote ikiwa hatukubali msalaba jinsi ulivyo wa ukweli". Papa Francisko wakati wa Misa ya liturujia ya kibizantino Prešov nchini Slovakia amesema msalaba"Hauna faida yoyote ikiwa hatukubali msalaba jinsi ulivyo wa ukweli".  Tahariri

Msalaba,kutoka ishara ya utambulisho hadi chanzo cha maisha mapya

Katika mahubiri ya liturujia ya Siku iliyoadhimishwa huko Prešov kwa ibada ya Kibizantini,Papa Francisko ameomba waamini ili wasitumie kamwe msalaba kwa manufaa binafsi.Ushuhuda ambao upo katika moyo wa msalaba na sio tu shingoni mwake,hauoni mtu yeyote kama adui,bali kila mtu ni kama kaka na dada ambao Yesu alitoa uhai wake.

ANDREA TORNIELLI

Msalaba ni nini? Kitu cha kujitolea, ishara ya utambulisho kiutamaduni inayotakiwa kutumiwa, bendera ya kuinuliwa? Katika siku ambayo Kanisa linasheherekea Siku Kuu ya Kutukuka kwa Msalaba, Papa Francisko akiwa Prešov nchini Slovakia  amewaomba Wakristo kwamba kamwe wasiupunguzie msalaba katika katika mambo haya yote na hata iwe kwa ishara ya kisiasa au ishara muhimu ya kidini na kijamii. Utumiaji uliopo kila wakati, ni rahisi kwa njia fulani kuufunua wazi kwa sababu ni dhahiri. Ni vigumu zaidi kukubali changamoto kwa kila mmoja wetu iliyo katika maneno ya Papa. "Kwa sababu sisi pia tuna hatari ya kutokubali mantiki ya msalaba, bila kukubali kwamba “Mungu anatuokoa kwa kuruhusu uovu wa ulimwengu umgeukie hata yeye".

Tunakubali kwa maneno tu, Mungu dhaifu na aliyesulubiwa ambaye hujinyenyekeza na kujiangamiza kwa kujitoa sadaka, lakini kichini chini tunaota yule mungu wa ushindi na Ukristo wa washindi”, wenye kuwa na wasiwasi juu ya kuhesabu jukwaa la ulimwengu, wasiwasi juu ya umuhimu wa jamii yake, juu ya utambuzi, wa heshima na utukufu ambao ulimwengu unatoa. “Ni jaribio kubwa”, amesema Papa Francisko na ni kwa sababu kufanya hivyo Ukristo unakuwa wa kidunia na tasa".

Jinsi gani, basi ya kuutazama msalaba kulingana na mantiki ya Mungu? Papa anakumbusha kwamba baadhi ya watakatifu wengine wameufananisha na kitabu ambacho ili kijulikane, lazima kifunguliwe na kusomwa. Haitoshi kutoa mtazamo wa macho yako  juu yake tu wakati unakinunua na baadaye kukiweka kwenye maonesho ya nyumba zetu. "Msalaba katika viwanja vyetu na makanisa havihesabiwi, misalaba tunayovaa shingoni au kuibeba mifukoni mwetu haihesabiwi. Walakini pia haina maana ikiwa hatuelekezi mtazamo wetu juu ya Msalaba, ikiwa haturuhusu kusukumwa nao kwa kutazama vidonda vyake vilivyo wazi kwa ajili ya wokovu wetu. Hakuna faida yoyote ikiwa hatukubali msalaba jinsi ulivyo wa ukweli".

“Ushuhuda ambao upo katika moyo wa msalaba na sio tu shingoni mwake, Papa Francisko amesema, hauoni mtu yeyote kama adui, bali kila mtu ni kama kaka na dada ambao Yesu alitoa uhai wake kwa ajili yao. Shuhuda wa msalaba hakumbuki makosa ya zamani na halalamikii juu ya sasa. Shuhuda wa msalaba hatumii njia za udanganyifu na nguvu za ulimwengu: hataki kulazimisha yeye mwenyewe na walio wake, japokuwa hutoa maisha yake kwa ajili ya wengine. Hatafuti faida zake mwenyewe na baadaye kujionesha kama anayejitoa”.

Mnamo tarehe 22 Machi 1988, wakati mjadala mmoja juu ya uwepo wa msalaba katika mashule, mwandishi Natalia Ginzburg aliandika nakala muhimu katika gazeti la kila siku la “unita”, yaani  Umoja: “Msalaba hauleti ubaguzi wowote. Huko kimya... Msalaba ni ishara ya maumivu ya mwanadamu. Taji la miiba na misumari, huashiria mateso yake. Msalaba ambao tunadhani uko juu ya mlima ni ishara ya upweke katika kifo. Sijui ishara nyinginezo ambazo hutoa maana zaidi ya hatima yetu ya kibinadamu. Msalaba ni sehemu ya historia ya ulimwengu”. Ni mtazamo wenye uwezo wa kufahamu ni kitu gani kilicho muhimu.

14 September 2021, 14:31