Tafuta

Sinodi ya Maaskofu Sinodi ya Maaskofu  

Vatican:Hati ya maandalizi ya mchakato wa Sinodi ijayo ya 2023!

Sekretarieti ya Sinodi imechapisha Hati ya maandalizi na mhutasari wa kufanyia kazi katika hatua ya safari ya maadhimisho ya Sinodi ya XVI ya Maaskofu itakayo adhimishwa tarehe 9-10 Oktoba jijini Roma na tarehe 17 Oktoba katika Makanisa Mahalia wakati huo huomchakato huo utahitimishwa jijini Vatican mnamo 2023.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Kusikiliza bila kuhukumu. Kuwa na ujasiri na kutoa neno. Kusikiliza na Kanisa, jamii na madhehebu mengine ya kikristo. Katibu Mkuu wa Sinodi amechapisha Hati ya maandalizi na ndondoo za waswali kwa ajili ya wakurugenzi kuhusu maelekezo ya mchakato wa safari ya Sinodi inayoongozwa na kauli mbiu: “Kwa ajili ya Kanisa la Kisinodi: Umoja, Ushiriki na Utume”, itakayofanyika tarehe 9 hadi 10 Oktoba jijini Roma na tarehe 17 katika Makanisa Mahalia na ambayo itihitimisha na maaskofu jijiji Vatican mnamo 2023. Hati hizi mbili zinataka kwa hakika kuwa chombo madhubuti hasa cha kusaidia kuhamasisha awamu ya kwanza ya kusikiliza na kushauriana na Watu wa Mungu katika Makanisa Mahalia na Taasisi zote za Kanisa ambayo itafanyika kuanzia mwezi Oktoba 2021 hadi Aprili 2022. Wakati 'Vademecum' ambayo ni mhutasari wa dondoo za maswali ambayo yanachukuliwa kama mwongozo unaotoa msaada wa vitendo kwa wawakilishi wa majimbo ili kuandaa watu wa Mungu. Mwongo huo una maombi hata kupitia mtandaoni, mambo mihimu ya mifano ya Sinodi za hivi karibuni zilizofanyika, na orodha ya maneno ya mchakato wa sinodi. Kwa maana hiyo sio kitabu cha sheria, lakini ni mwongozo wa kuunga mkono juhudi za kila Kanisa Mahalia katika mchakato wa safari hii ya kisinodi.

Katika misingi miwili ya uchapishwaji wa hati hizo kuna swali la kina ambalo linauliza: “Je ni jinsi gani ya kuweza kutimiza katika ngazi (ile ya mahalia na ile ya Kiulimwengu) mchakato ule wa safari ya pamoja ambayo inaruhusu Kanisa kutangaza Injili, kulingana na utume ambao ndiyo uliokabidhiwa; na ni hatua gani ya roho ambayo inatualika kutumiza kwa ajili ya kukua kama Kanisa la kisinodi? Ili kujibu swali hilo, Katibu wa Sinodi amesisitizia ulazima wa kuishi katika mchakato wa kikanisa wa ushiriki na ujumuishwaji ambao unatoa fursa kwa kila mmoja kwa namna ya pekee anayeishi pembeni, ile fursa ya kujieleza na kusikilizwa; baadaye kujitambua na kuthamini ukweli wa karama mbali mbazi na kutathmini jinsi ambavyo katika Kanisa kuna kuishi uwajibikaji na madaraka.

Jumuiya ya Kikristo inaombwa idhibitishwe kama somo la kuaminika na mshiriki wa kuaminika.  Vile vile inahusu kuzaliwa kwa upya mahusiano, na wawakilishi wa madhehbu mwengine, mashirika ya kijamii, asasi za kiraia na vyama vya watu. Hatua za dhati, hata hivyo ni ambazo zinajikita ndani ya picha ya kihistoria ambayo imegubikwa na janga la UVIKO na katika muktadha ambao Kanisa linakabiliana ndani mwake na ukosefu wa imani, ufisadi, na manyanyaso. Ni kwa sababu ya vivuli hivyo ambavyo vimevumbuliwa mateso, lakini pamoja na hayo yote kuna kuchanua michakato mipya ya kuweza kusimamisha msingi wa safari ya maisha ya kikristo na Kikanisa.

Katika hati hiyo ndefu vile vile imepewa nafasi kubwa ya walei. Hati hiyo inabainisisha kuwa wabatizwa wote ni wawakilishi hai wa uinjilishaji na kwamba ni msingi kuwa wachungaji wasiwe na wasiwasi wa kujikita katika kusikiliza zizi lao. Katika Kanisa la Kisinodi, kwa hakika kila mmoja analo la kujifunza kutoka kwa mwingine. Hati hiyo ya maandalizi baadaye inapendekeza maswali ili kuongoza mashauriano ya Watu wa Mungu, kuanzia na swali: Je ni jinsi gani ya kutembea kwa pamoja leo hii katika Kanisa lako mahalia? Kwa maana hiyo wanashauri kujifunza kutoka katika uzoefu wa kila jimbo juu ya mtazamo huo kwa kuzingatia mahusiano ya ndani ya majimbo na kati ya waamini, makleri, maparokia, lakini hata kati ya maaskofu na mitindo mbali mbali ya maisha ya kidini na watawa, vyama, harakati za kijamii na taasisi kama shule, hospitali, vyuo vikuu na mashirika ya upendo. Lazima kuzingatia pia mahusiano na shughuli za pamoja na dini nyingine na ulimwengu wa kisiasa, utamaduni, fedha, ajira, vyama vya wafanyakazi na watu walio wachache.

Hatimaye Hati hiyo inonesha mantiki kumi inayohusu hali ya kuishi kisinodi kwa kujikita kwa undani zaidi ili kutajirisha mashauriano. Mingoni mwake ni kutafakari juu ya yule anayeshiriki na ambaye anafafanulia katika Kanisa letu; kusikiliza vijana, wanawake watawa, waliobaguliwa, waliopweke: kufikiria ikiwa katika Kanisa kuna uhamasishaji wa mtindo wa kuwasiliana kwa dhati, bila kuwa ndumila kuwili; kutathamashi maombi na liturujia zinazoelekeza safari ya upamoja. Kutafakari jinsi gani jumuiya inasaidia wajumbe wanaojikita katika utoaji wa huduma; kufikiria tena maeneo na mitindo ya mazungumzo katika majimbo, na majimbo yaliyo karibu, na jumui za za kitawa na vyama vya kitume taasisi mbambali mbali na wale wasio amini.

Bado kuna hata suala la kuhoji jinsi gani mamlaka inavyotumiwa katika Kanisa Mahalia, na jinsi gani maamuzi yanafanywa; ni zana gani zinazohamasishwa kwa uwazi na uwajibikaji, je ni jinsi gani kwa wale walio katika nafasi za uwajibikaji wanavyofundishwa. Matunda ya tafakari hizi za kuhamasisha majadiliano katika ngazi ya Mabara kwa mujibu wa Katibu wa Sinodi ni kwamba tayaweza kukusanywa kwa pamoja katika makumi ya kurasa katika majarida, lakini si kwa kutaka kuzalisha Hati badala yake ni kutaka kufanya ichanue ile ndoto ya kinabii na matumaini.

MIONGOZO YA MCHAKATO WA KISINODI
07 September 2021, 12:24