Tafuta

2021.09.09 Kardinali Stefan Wyszyński akiwa na picha ya Mama wa Czestochowa. 2021.09.09 Kardinali Stefan Wyszyński akiwa na picha ya Mama wa Czestochowa. 

Kard.Semeraro:Wenyeheri wapya waliunganisha imani moja katika Injili

Imani kama zawadi iliyopokelewa na maisha ya mtu kama zawadi inayotolewa ndivyo vilikuwa sifa moja ya Kardinali Stefan Wyszyński na Mama Elisabetta Róza Czacka kwa mujibu wa Kardinali Marcello Semeraro,Rais wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu wakati wa kutangaza wenyeheri,Septemba 12 huko Warsaw Poland katika Kanisa la Mungu Mpaji.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican.

Wote wawili walikuwa nguzo na wote na walikuwa wa kipoland, walikuwa wamepokea kutoka kwa Bwana, kupitia familia, Kanisa na taifa hili, wema mzuri wa imani na uchangamfu wa mila ya zamani ya upendo kwa Mungu. Baraka mbili mpya pia mfano wa kawaida wa maisha yote, kuanzia  na uhakika wa kuishi wa ubora wa Mungu anayeweza kurudisha utu wa mwanadamu. Pia kuna ushuhuda wa ajabu, kama huo: wa maisha ya uaminifu kwa ajili ya Injili kwa gharama yoyote. Hii ni moja wapo ya urithi mkuu ambao Kardinali Stefan Wyszyński na Mama Elisabetta Róza Czacka walikuwa nayo sawa, iliyosemwa wakati wa mahubiri na Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Tatakatifu, Kardinali Marcello Semeraro.

Kardinali Wyszynski na Karol Wojtyla
Kardinali Wyszynski na Karol Wojtyla

Katika maadhimisho ya misa takatifu katika Kanisa la Mungu mpaji huko Warsaw nchini Poland, Dominika tarehe 12 Septemba 2021, Kardinali Semeraro amekumbusha mkutano wa kihistoria ambao ulifanyika kati ya hao wawili huko Laski mnamo 1926, ambapo kuhani kijana wa wakati huo Wyszyński alikuwa mchungaji wa taasisi ya vipofu, sekta ambayo Mama huyo, alikuwa kipofu piakijikita nayo. Kuhani kijana alijengwa na imani na uthabiti wa yule mwanamke ambaye, akiongozwa na upendo wa kimungu, alikuwa amejitoa kabisa kwa Mungu na jirani. Kutokana na kukutana huko ushirikiano wa thamani ulizaliwa, kwa malengo, lakini awali ya yote ushirikiano wa imani na upendo kwa Mungu na kwa mtu maskini na asiye na ulinzi. Tofauti pekee kati yao ilikuwa ni utambulisho wa mtu maskini na asiye na kinga ambaye walielekeza kujitoa kwao, hasa  wale walioumizwa katika uhuru wao na kuzuiwa katika imani zao kwa Kardinali Wyszyński ambaye alikuwa mtarajiwa kwa siku za usoni; Na kwa mama Czacka walikuwa ni kwa watu wasioona kimwili na kiroho na wale ambao walikuwa pembezoni mwa jamii. 

Wito na agano kwa Kardinali Wyszyński ilikuwa ni kupenda kwa maana hiyo, Kardinali Semerato amezungumzia juu ya tukio muhimu ambalo lilitolea huko Laski, nje kidogo ya mji wa Warsaw, karibu miaka ishirini baadaye, wakati wa ghasia katika mji mkuu manamo 1944,ambazo ni mojawapo za kurasa za kutisha za Vita vya II vya Kidunia  na ambayo alikuwa kama mhusika mkuu Wyszyński. Kuhani huyo aliokota kipande cha karatasi kutoka ardhini ambacho kilikwepa moto uliokuwa ukiwaka katika jiji hilo, ambalo lilikuwa limeandikwa  neno moja “utapenda”. Alivutiwa na kile kilichokuwa kimetokea, alichukua kibarua hiyo kwenda kwenye Kanisa hilo akiwaonesha watawa na akasema: 'Huu ndio wito mtakatifu zaidi kwetu na kwa ulimwengu wote ambao mpiganaji Warsaw anatuachia. Kwa wito na  agano: utapenda Kwa kitenzi hiki rahisi lakini cha msingi, baadaye mwenyeheria alijua jinsi ya kufananisha maisha yake yote,  ya kutoa huduma yake kama mchungaji na askofu huko Lublin kwanza,baadaye  huko Gniezno na Warsaw, akikabiliwa na shida zote ambazo taifa lake lilipaswa kuteseka.

Mama Elizabeth, alikuwa kipofu kati ya vipofu: Kwa maana hiyo tunaweza kufupisha mfano wa kibinadamu wa mtawa huyu, ambao juu ya yote anasisitiza imani isiyotikisika kwa Mungu na katika Utoaji wake, amesema Kardinali. Kwa kuhisi ndani yake tangu utoto wake  wito wa kimungu ambao alikuwa tayari ameujibu moyoni mwake, akiwa na umri wa miaka 22 alipofuka na ilikuwa tukio hili ambalo lilimwoneesha njia sahihi: kuwatunza vipofu ambao wakati huo hawakupokea vya kutosha elimu nchini Poland. Kardinalli amesisitiza hasa  imani isiyanguka ya Mungu na juu ya utuoaji wake.  Kwa maana hiyo alianisha Jumuiya kwa ajili ya kutunza wasioona na Shirila la Wafransiakani wa Mabitni wa Msalaba, na akabadilisha alfabeti ya Braille kwa lugha ya Kipoland na akakamilisha njia fupi za maandishi.  Mfano wake unatuambia kwamba hakuna vizuizi kwa wale ambao wanataka kumpenda Mungu na kama Mungu.

Madre Elizabeta Czacka
Madre Elizabeta Czacka

Kuishi kama Watakatifu kunawezekana: Katika kuhitimisha  mahubiri yake, KardinaliSemeraro ameomba kwa  maombezi ya wenye heri wapya  ili kuwa na shauku ya kuishi kama watakatifu na waweze kuwashwa ndani  mwetu akinukuu maneno ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye alitukumbusha katika katekesi ya  tarehe  7 Aprili 2021 juu ya nini maana ya watakatifu kwamba ni"mashahuda ambao tunawaabudu na ambao kwa njia elfu tofauti wanatuelekeza kwa Yesu Kristo, Bwana wa pekee na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu.

12 September 2021, 16:59