Tafuta

2021.09.20:Mkutano wa Kimataifa huko Warsaw,Poland,siku ya pili: hotuba ya Profesa Myriam Wijlens. 2021.09.20:Mkutano wa Kimataifa huko Warsaw,Poland,siku ya pili: hotuba ya Profesa Myriam Wijlens. 

Prof.Myriam Wijlens:Ukuaji wa dhamiri kuwa nyanyaso zipo

Kuna ongezekaji la dhamiri kutokana na kwamba baadhi ya makleri walinyanyasa watoto.Watoto na vijana wanabaki hawana hadhi na ufungamanishwaji wao na mara nyingi maisha yao yote yana majeraha ya kina katika imani ya kikristo.Haya yamesemwa na Prof Wijlem Mjumbe wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa watoto katika mkutano wa kimataifa huko Warsaw,Poland.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Kikao cha mkutano uliofunguliwa tarehe 19 Septemba 2021, kuhusu ulinzi wa watoto, na ambacho kinaongozwa na mada: “Utume wetu wa kulinda watoto wa Mungu” kwa ajili ya Nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki, Profesa Dk Myriam Wijlens, wa Sheria ya Kanoni huko Erfurt na mjumbe wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto,  (PCTM) Jumatatu tarehe 20 Septemba 2021 amesema kuwa, mgogoro uliotokana na kutangazwa kwa kesi za manyanyaso ya kijinsia kwa watoto kwa upande wa Makleri, unajikita katika sehemu kubwa ya Makanisa mahalia ulimwengu wote kwa hatua mbili: kwanza, inatazama ukuaji wa dhamiri kutokana na kwamba baadhi ya makleri, walinyanyasa watoto. Watoto na vijana wanabaki hawana si tu kutokuwa na hadhi na ufungamanishwaji wao, lakini pia  mara nyingi maisha yao yote yana majeraha ya kina katika imani ya kikristo

Matokeo yake yanakuwa wazi kwamba viongozi wa Kanisa walioshindwa kwa kiasi kikubwa kutangaza katika nuru haya yaliyojitokeza. Walizingatia sifa ya Kanisa badala ya ulinzi wa watoto. Uaminifu uliowekwa ndani yao na jumuiya ya waamini na jamii ni hatari sana na husababisha ukosefu wa mamlaka ya maadili. Papa Francisko ameamua kwamba ikiwa maaskofu watashindwa katika jukumu lao, lazima wawajibike kwa hilo. Mgogoro huo unahitaji tafakari ya kitaalimungu na ya sheria ya kikanoni juu ya jukumu la askofu wa jimbo kuhusu dhamana ya kuzuia, kuingilia kati, haki na uponyaji. Kwa mujibu wa Neville Owen hakimu mkuu mstaafu katika Mahakama kuu ya Australia Magharibi na Rais Mstaafu wa “The Truth, Justice and Healing Council”  Baraza la Ukweli, hakia na upeneshaji la Baraza la Maaskofu nchini Australia na Mjumbe wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa watoto, katika maoni yake amesema kuwa, si Baba Mtakatifu lakini hata jamii ya raia na Serikali, wanatambua ulizni wa watoto na  kuingilia kati ikiwa Kanisa linashindwa kulinda kwa kiasi cha kutosha waathiriwa zaidi na ikiwa manyanyaso yanafunikwa.

Haya yote amebainisha kwamba yametokea katika sehemu mbalimbali, ikiwemo hata nchini Australia. Jibu la Kanisa Katoliki, katika suala hili kuhusu  Serikali inatoa fursa ya tafakari kwa mabaraza mengine ya kiaskofu. Kwa miaka mitano tangu (2013 hadi 2017), athari mbaya ya unyanyasaji wa kijinsia wa watoto kwa upande wa makleri na wengine ndani ya Kanisa Katoliki nchini Australia imekuwa mada ya uchunguzi mkali ambao umechukua mtindo wa Tume ya Kifalme, aina ya uchunguzi wenye nguvu zaidi uliotabiriwa katika mfumo wa sheria wa Australia. Uchunguzi ulifunua kiwango cha matukio ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto katika taasisi za Kanisa. Lakini, angalau hata umuhimu sawa, ulioneshwa wazi kutofaulu kwa janga la uongozi wa Kanisa kushughulikia mikasa hii vya kutosha, au hata kutoshughulikia kabisa. Kukosekana kwa uwajibikaji na kujali kulidhihirika kwa upande wa wote. Waathiriwa na waamini waliomba kuingilia kati na mamlaka ya raia na serikali walijibu wito huo.

Akiendendelea na ufafanuzi huo Neville Owen hakimu mkuu mstaafu katika Mahakama kuu ya Australia Magharibi amesema kuwa hata hivyo mchango utawakilishwa na kuonesha mitindo ambayo serikali ya Australia imeonesha kwa niaba ya kuleta mabadiliko na kutekeleza kanuni ya uwajibikaji na ambayo kimsingi imebadilisha njia ambayo Kanisa linashirikiana na mamlaka ya Serikali. Hakuna Kanisa mahalia, mahali popote ambapo hakina matokeo haya mabaya ya janga la manyanyaso kwa watoto wadogo. Ni lazima kwa maana hiyo uwajibikaji, kujali na uwazi wa kutenda na wanasheria wengine miongono mwake Australia ambao wawe ndiyo mafunzo kwa wote.

20 September 2021, 15:44