Tafuta

2021.09.21 Picha ya pamoja katika Mkutano huko Warsaw nchini Poland kuhusu ulinzi wa watoto 2021.09.21 Picha ya pamoja katika Mkutano huko Warsaw nchini Poland kuhusu ulinzi wa watoto  

Poland:jitihada ya Kanisa la Kipoland kuwa na dhamiri ya ulinzi wa watoto

Mgogoro uliosababishwa na unyanyasaji wa kijinsia wa watoto umekuta Kanisa la Kipoland na jamii kutokuwa tayari.Mifumo hasi ilishinda katika athari za kwanza.Katika miaka ya hivi karibuni,Kanisa la Kipoland limeweza kuunda mfumo jumuishi wa ulinzi wa watoto na misaada kwa waathiriwa, shukrani kwa maswali ya waandishi wa habari na msukumo ulio wazi wa Vatican.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Nchini Poland, Kanisa liliingia karne ya 21 na hisia ya mafanikio yaliyopatikana na majivuno. Hisia hii ilikuwa na nia zake katika historia ya mbali na ya hivi karibuni ya Poland. Hadi 1918, kwa miaka 123 ambayo serikali ya Kipoland, iliyogawanywa kati ya mamlaka za jirani, ilifutwa, Kanisa Katoliki lilikuwa limeunda kwa Wasiwani ngome ya uhuru na ilikuwa imechangia uhai wa lugha na tamaduni ya taifa, vile vile kuhusu matumaini ya uhuru. Katika kipindi cha Vita vya Pili vya Kidunia hakukuwa na ukosefu wa mitazamo ya kishujaa ya mapadri wengi wakatoliki na walei wakatoliki. Baada ya 1945, wakati Poland ilijikuta katika eneo la ushawishi la Umoja wa Kisovieti, Kanisa lilikuwa karibu na watu, likijaribu kuhifadhi uhuru na kurudisha utu na haki za mwanadamu. Katika muktadha huu Karol Wojtyła yaani Mtakatifu John Paulo II alikulia katika mazingiara haya. Hija za Papa za kwenda Poland zilichangia sana kuamka pole kwa pole, zikichochea ukuaji wa hali ya umoja wa kitaifa na kuimarisha jukumu la Kanisa katika maisha ya kijamii ya Kipoland. Huko Ulaya, ambapo kwa miongo mingi, Poland ilibaki kuwa nchi ambayo waliobatizwa walikuwa zaidi ya 90% ya idadi ya watu, karibu nusu yao walifanya mazoezi mara kwa mara, na seminari zilijazwa na waseminari kuekea ukuhani. Mamlaka ya maadili ya mapadre hayakuwa na ubishi katika jamii ya Wapoland.

Hisia hii halali ya mafanikio na majivuno imefanya iwe ngumu kufikia ukweli wa unyanyasaji wa watoto uliofanywa na wajumbe wa Kanisa. Kiukweli, ilikuwa ngumu kukubali, kujua kwamba katika Kanisa lile lile, uhalifu mbaya kama huo dhidi ya watoto pia ulifanyika. Kwa hivyo, habari ya kwanza kwenye vyombo vya habari  juu ya unyanyasaji wa kijinsia wa watoto na kutoka kwa washiriki wa  Kansa ilichochea athari ya kiasili ya kujitetea kati ya makuhani na watu wa walei huko Poland. Walichukuliwa kama shambulio na uadui na vyombo vya habari na usemi mwingine wa mapambano dhidi ya Kanisa, inayojulikana tangu siku za ukomunisti.

Pigo kubwa kwa maoni ya umma lilikuwa historia, zilizofunuliwa na vyombo vya habari, za mapadre wawili wa Kipoland ambao walifanya kazi katika Jamhuri ya Dominika: Balozi wa kitume na mmisionari, aliyeshtakiwa kwa kuwanyanyasa watoto kijinsia (2013). Filamu za ndugu wa Sekielski zilizochapishwa kwenye YouTube zilikuwa tetemeko la ardhi la kweli: “Lakini usimwambie mtu yeyote” (2019) na “Kucheza kujificha na kutafuta"(2020). Leo hii lazima tugundue kwa uaminifu kwamba sauti ya waandishi wa habari ilikuwa jambo la msingi ambalo lilihamasisha Kanisa huko Poland kushughulikia uovu wa unyanyasaji wa kijinsia.

Hakuna sababu muhimu ambazo zimeathiri mabadiliko katika njia ya Kanisa kwa janga la unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto, haya  yalikuwa maamuzi ya Vatican na mabadiliko yanayofanyika katika Kanisa. Mifano miwili inaonesha hii. Ya kwanza ni historia ya uandishi wa hati inayofafanua sheria za kesi za jimbo huko Poland katika kesi za mashtaka dhidi ya mapadre wa unyanyasaji wa kijinsia. Toleo la kwanza la waraka huo liliidhinishwa na Maaskofu wa Kipoland mapema mnamo 2009, lakini sheria hizo zilikuwa za siri kwa asili, hazikuwekwa wazi kwa umma. Kwa kujibu tu pendekezo la Baraza la Kipapa la  Mafundisho Tanzu ya Kanisa  2011, Baraza la Maaskofu wa Kipoland  ulipitishwa mnamo Oktoba 2014 na kuchapisha nyaraka mbili ambazo bado zinafuata mwelekeo wa utendaji wa Kanisa nchini Poland.

Mfano mwingine unahusu wawakilishi  kwa ajili ya ulinzi wa watoto na vijana, ambao wana jukumu la kupokea malalamiko. Ingawa wajumbe walioteuliwa na maaskofu na wakuu wa mashirika tayari kuelekea mwisho wa 2014, katika miaka iliyofuata maelezo ya mawasiliano yalikuwa bado hayajachapishwa kwenye wavuti rasmi za majimbo mengi na maagizo mbali mbali ya mashirika ya kitawa. Uchapishaji wa takwimu hizi ukawa kiwango cha jumla tu mnamo 2019, wakati ilipochapishwa Barua binafsi ya Papa Francisko ya motto proprio “Vos Estis Lux Mundi” na kuanza kutumika.

22 September 2021, 18:19