Tafuta

2021.07.27 Chama cha Wanawake katoliki nchi Cameroon 2021.07.27 Chama cha Wanawake katoliki nchi Cameroon  

Mons.Balvo,Osce:Kusiwe na ukosefu wa usawa kati ya wanawake na mme katika ajira

Katika mkutano uliohitimishwa wa Jukwa la 29 lauchumi na mazingira wa OSCE kuhusu usalama ulimwenguni,msimamo na maendeleo endelevu,na maendelo ya uchumi kwa wanawake,mwakilishi wa Vatican ameomba wanawake wawe na usawa kiuchumi unaotambuliwa kwa wanaume na anawakumbasha Waraka Wote ni ndugu wa Papa Francisko.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Bado kuna mengi ya kufanya ili kuhakikisha kuwa hakuna mifumo miwili ya usalama wa jamii ambayo inasababisha tofauti kati ya wanaume na wanawake katika suala la malipo, bima na usalama wa kijamii. Hayo ndiyo aliyosema katika hotuba yake aliyoitoa alhamisi tarehe 9 Septemba 2021  huko Praga, katika Jamuhuri ya Czech kwenye  ufunguzi wa  Mkutano wa 29 wa Uchumi na Mazingira wa OSCE (Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya) na Monsinyo Carlo Balvo, Balozi wa kitume katika Jamhuri ya Czech na Mwakilisho wa Vatican.

Katika mkutano huo, ambao ulimalizika Ijumaa 10 Septemba 2021 kwa kuongozwa na kaulimbiu: “Kuhamasisha usalama wa ulimwengu, utulivu na maendeleo endelevu katika eneo la Osce kupitia ukombozi wa wanawake kiuchumii”, Monsinyo Balvo amekiri kwamba mengi yamefanywa kuhusiana na usawa kazini na Nchi zinazoshiriki na kukumbuka kuwa miaka 10 iliyopita, katika mkutano wa 18 wa Baraza la Mawaziri la OSCE uliofanyika Vilnius, ilitambuliwa kwamba ushiriki wa wanawake katika nyanja ya uchumi unachangia pakubwa kufufua uchumi, ukuaji endelevu na kuunda jamii zenye mshikamano na kwa maana hiyo ni muhimu kwa usalama na utulivu wa kanda ya Osce.

Lakini Balozi huyo wa kitume akaini kuwa, licha ya maendeleo muhimu yaliofikiwa, kama vile Papa Francisko anavyoandika katika Waraka wake Fratelli Tutti yaani Wote ni ndugu, shirika jumuiya ya Umoja wa mataifa  ulimwenguni kote bado halijadhihirisha wazi kwamba wanawake wana hadhi sawa na haki sawa kama wanaume na kwamba maneno yanathibitisha mambo fulani, lakini maamuzi na ukweli hupiga kelele ujumbe mwingine na, kama vile isemavyo Wosiwa wa Evangelii Gaudium , kwamba  “mara mbili maskini ni wale wanawake ambao wanakabiliwa na hali za kutengwa, dhuluma na unyanyasaji, kama kawaida wanajikuta wana nafasi ndogo ya kutetea haki zao”.

Balozi wa kitume Balvo aidha mesema kwamba Baba Mtakatifu Francisko yuko wazi vile vile wakati anazungumzia suala la mishahara na kukumbuka kile ambacho Papa alisema wakati wa katekesi yaketarehe 29 April 2015, akialika watu kuunga mkono kwa dhati haki ya malipo sawa kwa kazi sawa, na  kuonesha kwamba wanawake na wanaume wana haki sawa na kwamba ukosefu wa usawa katika hali ya kiuchumi 'ni kashfa ya wazi. Kama ilivyobainika mara kadhaa wakati wa mzunguko ya Jukwaa la Uchumi na Mazingira, ni jambo lisilopingika kwamba wanawake wameathiriwa sana na matokeo ya janga la Covid-19. Mchango wao mkubwa kama wafanykazi wa afya na uwepo wao katika sekta mbali mbali za kazi isiyo rasmi, na pia jukumu lao muhimu katika kutoa huduma ya watoto, vimewaleta kuwa mstari wa mbele katika mgogoro huo kwa kuwabebesha mzigo mzito hasa. Kwa mujibu wa Balozi wa kitume Balvo haya ni mambo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika mpango wowote kamili wa kupona kutokana na  Covid-19. Hatimaye kiongozi huyo wa kitume aliwashukuru waandaaji wa mkutano wa kufunga Mkutano wa 29 wa Uchumi na Mazingira, akihakikisha nia inayoendelea na kujitoa kwa Vatican kwa usalama wa ulimwengu.

11 September 2021, 12:38