Tafuta

Mkutano Warsaw,Poland:'Utume wetu wa pamoja wa kulinda watoto wa Mungu' ndiyo kauli mbiu inayoongoza mkutano wa kimataifa kuanzia tarehe 19 hadi 22 Septemba 2021 Mkutano Warsaw,Poland:'Utume wetu wa pamoja wa kulinda watoto wa Mungu' ndiyo kauli mbiu inayoongoza mkutano wa kimataifa kuanzia tarehe 19 hadi 22 Septemba 2021 

Poland:Mkutano wa kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto Ulaya ya Kati na Mashariki

Kuanzia tarehe 19 hadi 22 Septemba huko Warsaw nchini Poland kutafanyika mkutano kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto katika Makanisa ya Ulaya ya kati.Kabla ya mkutano huo Profesa Hanna Suchocka,ambaye ni mjumbe tangu mwaka 2017 na wengine katika Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa watoto,alitoa maelezo kuhusu mkutano.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kuanzia tarehe 19 hadi 22 Septemba utafanyika mkutano wa kimataifai huko Warsaw, Poland ulioandaliwa na Tume ya kipapa ya Ulinzi wa Watoto kwa ajili ya ulinzi pamoja na  Baraza la Maaskofu Poland na wadau wanaojikita katika nyanya hiyo ya ulinzi wa watoto na vijana walioathirika. Washiriki ni kutoka Nchi 20 za Ulaya ya Kati na Mashariki.Utume wetu wa pamoja ni kulinda watoto wa Mungu” ndiyo kauli mbiu inayoongoza mkutano huo wa kimataifa, kwa lengo la kuruhusu kubadilishana uzoefu na kuanzisha matendo halisi ya pamoja, kwa namna ya kuweza kushirikiana kati ya Makanisa ya Ulaya ya Kati na Mashariki katika uwanja mpana wa kuzuia manyanyaso ya kijinsia kwa watoto. Mkutano huo utajikita si tu katika kutoa jibula pampja  la Kanisa katika mgogoro wa manyanyaso, lakini ni kwa namna ya kutathimini baadhi ya matatizo maalum katika muktadha huo hata matukio katika Kanisa na katika jamii, kwa mujibu wa Padre Adam Żak mratibu wa Ulinzi wa watoto na vijana wa Maaskofu wa Poland na wajumbe wa tume ya waandalizi.

Kwa mujibu wa Padre Żak amefafanua juu ya  matumaini ambayo mkutano wa kimataifa unaweza kubadilishana mazoezi mema na zaidi hata kushirikiana kati ya watu na Taasisi za Ulaya ya Kati na Masharikina hatimaya kujenga kwa pamoja kwa namna ya dhati ule  utamaduni wa ulinzi wa watu waathirika. Zaidi ya kusilikiza mada hizo washiriki watafanya kazi katika makundi ya lugha zao, huku wakishirikishana kama masuala ya ulinzi wa watoto kwa uwakilisho wa kila Nchi ambayo iweze kwa namna ya kuzuia na kusaidia waathirika. Washiriki pia watatathimini changamoto na kwamba waèpate fursa ya kushirikishana kwa Makanisa ambayo lazima yakabiliane na sehemu hii ya Ulaya. Kila siku kwa mujibu wa maelezo ya mratibu  kutakuwa na wakati wa sala ya pamoja, ikiwa ni pamoja na liturujia ya kitubio. Sehemu nyingine muhimu ya Mkutano huo itakuwa na ushuhuda wa watu mbali mbali kutoka katika Nchi ambao walipata manyanyaso  kutoka kwa wajumbe wa kanisa

Kwa mujibu wa Profesa Hanna Suchocka  kuhusu “Utume wetu wa pamoja”

Akihojiwa na vyombo vya habari Vatican hivi karibuni kuhusiana na mkutano huo, Profesa Hanna Suchocka ambaye ni profesa wa Sheria ya Katiba na mtaalam wa haki za binadamu katika Chuo Kikuu cha Poznan (Poland) alifafanua kwa kirefu. Alianza kuelezea asili ya tume ya ulinzi wa watoto na watu walio katika mazingira magumu. Tume ya Kipapa ya Kulinda Watoto ilianzishwa mnamo 2014 kama chombo cha ushauri katika utumishi wa Baba Mtakatifu. Jukumu la Tume hii ni kupendekeza mipango kwa Baba Mtakatifu inayolenga kukuza uwajibikaji hasa kwa Makanisa katika ulinzi wa watoto wote na watu wazima walio katika mazingira magumu (Ibara 1). Kuanzia mwanzo, wasiwasi mkubwa wa Tume umekuwa kutafuta njia bora ya kulinda watoto na kusaidia Papa na Kanisa ili kufikia lengo hili.

Jukumu la Tume, hata hivyo, haijawahi kuchukua jukumu la visa vya unyanyasaji (jukumu, badala yake, mamlaka ya kimahakama. Hivi karibuni ilidhihirika kuwa katika hali nyingi tabia ya Kanisa inayolenga kujilinda ilijiingiza zaidi na zaidi katika hali ya hatari, kwa kusababisha uharibifu. Hasira kubwa ilikuwa imesababishwa na wale ambao, katika nafasi ya mamlaka, walitaka kulinda sifa za mtu binafsi na kujaribu kuzuia kashfa kwa kuficha wanyanyasaji, kuwahamisha na hivyo kusababisha unyanyasaji mpya wa watoto badala ya ulinzi wao.

Tume ilishiriki kanuni kuu msingi kama uaminifu, uwazi, uwajibikaji na uelewa. Mtu yeyote anayewajibika kwa wengine lazima awajibike, kwa njia ya uwazi, kwa njia ambayo wanatumia mamlaka yao; hakuna vigezo vya kujidhibiti nyuma ya milango iliyofungwa inaruhusiwa, pamoja na usimamizi wa nyanja za kitaalam za uchungaji, ualimu, ushauri na majukumu ya ushiriki wa jumuiya. Katika kipindi cha kwanza, Tume ya Kipapa ilizindua shughuli na mipango mbali mbali ambayo iligusia shida za jumla kama usiri wa Kipapa na jukumu la kuripoti. Wakati huo huo, mipango mingine ilizinduliwa katika kiwango cha sehemu mahalia. Lengo ni katika maeneo ambayo tayari kulikuwa na mazungumzo mengi juu ya dhuluma, na manyanyasi kama vile nchini Chile.

Tume inahusika katika kuandaa mipangao na makongamano, kama  vile Mkutano wa Amerika Kusini wa Ulinzi wa Watoto mnamo 2017, ulioandaliwa kwa pamoja na Tume ya Kipapa na Jimbo kuu la Bogotà na ushiriki wa CLAR (Shirikisho la Mashirika ya kitawa ya  Amerika Kusini), Celam (Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini), shule za Katoliki, mashirika ya serikali, NGO za kimataifa na za mahalia, vyombo vya habari vya kimataifa na Makanisa ya madhehebu mengine ya Kikristo; au kama burudani ya hali ya ulinzi katika elimu na mafunzo katika shule za Kikatoliki, na miapnago ya majaribio iliyozinduliwa Afrika Kusini, Colombia, India, Ufilipino na Tonga.

Kati ya washiriki 80 waliojiorodhesha kuna wajumbe wa Tume ya Kipapa, ya maaskofu, ya Mashirika makuu ya kidini ya wanawake na wanaume na kama ilivyo pia  walei walio hai  ambao wako mstari wa mbele katika uwanja wa ulinzi wa watoto katika nchi hizo. Hawa wanawakilisha Kanisa Katoliki la Roma na Kigiriki la kiroma nchini Poland, Slovakia, Jamhuri ya Czech, Ukraine, Romania, Kroatia, Belarusi, Hungari, Slovenia, Lithuania, Latvia, Estonia, Urusi, Serbia, Montenegro, Kosovo, Makedonia Kaskazini, Moldova, Albania, Bulgaria, Ujerumani (na Renovabis). Watu walioteuliwa na baraza la Maaskofu watashiriki kutoka kila nchi, pamoja na waratibu au wajumbe wa Mkutano na wawakilishi wa makutano ya kidini. Barua binafsi au Motu proprio ya Baba Mtakatifu Francisko “Vos estis lux mundi” ya 2019, ambayo inaweka utaratibu ambao unatilia shaka mamlaka za kanisa, ndiyo hati ambayo Mkutano huu unategemea kuongozwa nayo.

Mazingira yamebadilika tangu kuanzishwa kwa Tume hii. Awamu mbili zinaweza kutofautishwa katika Makanisa mengi ya mahali hapo: ya kwanza, ambayo yanaona mwamko unaokua wa ukweli kwamba baadhi ya mapadri wamewanyanyasa watoto; pili, inapobainika kuwa uongozi wa Kanisa umeshindwa kujibu malalamiko yaliyopokelewa. Mfuatano wa karibu wa tukio ya mwaka 2018, na tuhuma zinazohusisha viongozi mashuhuri Kanisani, kama vile Kardinali Theodore McCarrick na uzembe wa viongozi wa kanisa katika kushughulikia malalamiko hayo yalikuwa na athari kubwa kwa maoni ya umma juu ya uaminifu na uaminifu katika uongozi wa Kanisa. Tafsiri ya sheria, kuhusu jukumu kuu kuhusu hatua ya mtu aliye na mamlaka, imebadilika: hii inamaanisha kuwa leo hiiinawezekana kushikilia taasisi ya kisheria ya kanisa inayohusika na uharibifu unaosababishwa na unyanyasaji wa kijinsia na kuhani, hata ikiwa hii haijatokea katika muktadha wa utimilifu unaowezekana wa ofisi ya kisheria na kuhani, kama vile mafundisho ya dini au usimamizi wa sakramenti. Katika muktadha wa mamlaka ya kanisa, Papa Francisko ameamua kwamba ikiwa maaskofu watashindwa katika jukumu lao, lazima wawajibishwe. Mgogoro huu unahitaji tafakari ya kitaalimungu na kikanuni juu ya jukumu la askofu wa jimbo kuhusu dhamana ya kuzuia, kuingilia kati, haki na malipizi.

Profesa Hanna Suchocka alieleza kuwa katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki, mwamko wa kijamii na kitaasisi wa shida zinazotokana na unyanyasaji wa kijinsia wa watoto unakua. Kanisa (mahalia) pia linatambua shida hii. Bado kuna mawazo mazito ya usiri na kutokuaminiana, urithi wa zamani wa kikomunisti. Ni muhimu sana kwamba kipengele hiki kizingatiwe katika Mkutano. Kwa maana hiyo mkutano huu uajishughulisha na masuala haya yafuatayo: Kuhamasisha mamlaka katika Kanisa kuchukua majukumu kwa sababu ya kushughulikia vibaya unyanyasaji wa watoto na jibu la kutosha kwa uhalifu unaofanywa na waumini wa dini na makosa makubwa ya mamlaka ya kanisa, pamoja na kujitolea kwa nguvu kuzuia; Kukuza katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki ufahamu mzuri wa msimamo wa Vatican kuhusu unyanyasaji wa kijinsia wa watoto uliofanywa na washiriki wa makasisi; Kukuza uelewa mzuri katika taasisi na Vatican  juu ya hitaji la Makanisa ya Ulaya ya Kati na Mashariki kwa msaada maalum katika kushughulikia hali ya unyanyasaji wa kijinsia na mapadre.

Kutengeneza jukwaa la kushirikiana mara kwa mara na kubadilishana kati ya nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki; Kuhamasisha mawasiliano kati ya viongozi wa kanisa na waamini na asasi za kiraia katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki; Uundaji wa kikundi kinachofanya kazi ambacho kinawakilisha jukwaa la ubadilishaji wa kawaida na wa kushirikiana katika ujenzi wa mazingira salama kwa watoto. Ikumbukwe Profesa Hanna Suchocka ni profesa wa Sheria ya Katiba na mtaalam wa haki za binadamu katika Chuo Kikuu cha Poznan (Poland). Alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Poland kutoka 1992 hadi 1993 na balozi wa nchi hiyo kwa Vatican kutoka 2001 hadi 2013. Mnamo 2018 alithibitishwa tena na Baba Mtakatifu Francisko kama mshiriki wa Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto.

16 September 2021, 14:27