Tafuta

pope-francis-in-panama-for-world-youth-day--w-1548443330635.jpg

Kongamano la Maria kimataifa kuanzia 8-11 Septemba 2021

Kwa mara ya kwanza litafanyika Kongamano la Maria Kimataifa kunzia tarehe 8 hadi 11 Septemba 2021 kwa njia ya mtandao iliyoandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Maria Kimataifa (Pami).Kongamano hilo litawaona washiriki zaidi ya mia tatu kutoka sehemu mbali mbali za mabara matano.Na itakuwa na makundi saba ya lugha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa kwa mara ya kwanza litafanyika kwa njia ya Mtandao Kongamano kimataifa la  Maria lililoandaliwa na Taasisi ya Kipapa ya Elimu ya Mariana Kimataifa (Pami). Tukio hili limefikia sasa toleo lake la 25, likiongzwa na mada: “Maria kati ya taalimungu na tamaduni za leo. Mifano, mawasiliano, matarajio”. Kazi hiyo itaongozwa na Kardinali Gianfranco Ravasi, Rais wa Baraza la Kipapa la Utamaduni. Karibu ni washiriki 300 wanaotarajiwa, ambao wanawakilisha Jumuiya za Maria wa nchi tofauti ulimwenguni, pamoja na wasomi waliojiandikisha kutoka mabara matano ambao watajadili katika vikao mbali mbali vya mkutano na katika vikundi 7 vya lugha.

Kwa mujibu wa Padri Stefano Cecchin, Rais wa  Taasisi ya Elimu Kimataifa ya Maria (Pami), ameeleza kuwa ni fursa muhimu ya kutafakari juu ya njia ya taalimungu  ya Maria pia kwa kuzingatia mazungumzo ambayo yanatupatia changamoto kati ya imani na tamaduni. Lengo kuu la kazi hiyo, amesema litakuwa ni kutafuta jibu la swali: "Kwa nini Mari wa Nazareti, mama wa Yesu ambaye amekuwa dhana ya anthropolojia ya mama bora, 'ishara yenye nguvu na maarufu ya utamaduni wa miaka elfu mbili iliyopita; mwanamke mwenye nguvu zaidi ulimwenguni,' (National Geographic 2015), ambaye anaashiria 'maisha ya watu wengi na ambaye ni msingi wa fikira za Kikristo' (Mtakatifu Yohane  Paulo II), leo hii anapendekezwa kama ishara ya Nyumba ya pamoja na mfano wa anthropolojia mpya ya kinidhamu?

Kwa ufafanuzi huo mpango wa kazi ni pamoja na kutafakari juu ya sura ya Maria katika utamaduni wa Kifaransa, Kiingereza, Kijerumani, Kihispania, Kireno, tamaduni za Kislaviki na Asia; pia uchambuzi uliowekwa kwa ajili ya Elimu ya Maria kati ya taalimungu na tamaduni na kwa ajili ya kutathmini miaka 25 tangu kuanza kongamano la Kimataifa la Maria. Hata hivyo amesema kuwa wakati wa ufunguzi wa Kongamno hilo wanatarajia kupata ujumbe wa Papa Francisko.

07 September 2021, 16:17