Tafuta

Shambulizi la kigaidi 11 Septemba 2001,New York Marekani. Shambulizi la kigaidi 11 Septemba 2001,New York Marekani.  

Kard.Parolin,Septemba 11 ni hofu na kiwewe,elimu inahitajika

Katibu wa Vatican,akiwa katika kutia saini ya Maktaba ya Leoniana Roma kwa hati ya makubaliano kuhusu njia za mitaa jijini Roma katika matazamio ya jubilei 2025,amejibu maswali ya waandishi pembeni mwa tukio.Alikumbuka shambulio jijini New York 2001.Chanjo na suluhisho la janga.Kuchanja ni kitendo cha uwajibikaji kwa mtu binafsi na kwa wengine.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kardinali, Pietro Parolin, katibu wa Vatican amebainisha juu ya jinsi ambavyo  ulimwengu ulivyojaa vitisho na viwewe, kwa kuzua hofu  ambayo ilifanyika miaka ishirini iliyopita huko New York kwa  shambulio la kigaidi la majengo marefu mawili  ‘Twins tower’. Ilikuwa ni siku ambayo ilia mwaka tarehe 11 Septemba hufanyika kumbu kumbu hili tang mwaka 2001, katika tukio ambamo kwa hakika lilibadilisha maisha ya watu ulimwenguni. Katika Siku ya kumbukumbu ya tukio hilo la kushangaza, Kardinali  pembeni mwa  tukio òa kutiwa saini kwa Hati ya Makubaliano ya Njia ya  Roma (Francigena, Romea Germanica na Romaa Strata), kwenye Maktaba ya Leoniana huko Roma, alishirikisha habari binafsi ya kumbukumbu hii na Waandishi kwamba:“Nilikuwa nimerudi tu kutoka Marekani ambapo nilikuwa nimeshiriki katika mpango uliotolewa na Marekani kwa wanadiplomasi ulimwenguni kote. Habari zilizonifikia zilinigonga sana. Basi na kile kilichosababisha ulimwenguni kote kilikuwa cha kutisha na kiwewe… ”. Kardinali aliongeza “Nakumbuka kwamba moja ya tafakari ambayo ilifanywa wakati huo ilikuwa kuwa ugaidi huwezi kupambana nao tu kwa kuzingatia usalama, badala yake ni kwa kujaribu kubadilisha utamaduni kupitia elimu na mafunzo”. Kulingana na Katibu wa vatican, hali “hiyo bado ni ufunguo katika ulimwengu ambao bado unapata ugaidi leo. Ni kitu kidogo sana kimebadilika miaka mingi baadaye na ulimwengu unaendelea kujaa shida”.

Njia pekee ya kutoka katika janga ni chanjo

Akizungumzia juu ya Janga la sasa, Kardinali amesema kati ya shida hizi ni pamoja na janga la Uviko-19 ambalo linaendelea kusababisha vifo na maambukizi. Katika muktadha huu, Kardinali Parolin anakumbuka miito mingi ya Baba Mtakatifu Francisko kuhusu chanjo, hasa ule ya mwisho: ‘Chanjo ni tendo la upendo’. “Tafakari yetu kama Kanisa lazima iwe kwamba  tunakumbuka mwelekeo wa maadili ya chanjo. Ni kitendo cha uwajibikaji: lazima tuwajibike sisi binafsi na wengine. Tuna jukumu la kuhifadhi afya zetu na zaidi ya yote sio kuwadhuru wengine”. Kwa maana hii, Kardinali amesema, maandamano ya hivi karibuni ya kile kinachoitwa ‘No-Vax’ yanatia wasiwasi, hasa habari za hivi karibuni za vitendo vya vurugu zilizopangwa kupitia mitandao ya kijamii na kuzuiliwa na polisi: “Sielewi ni kwanini lazima tujilazimishe na vurugu mbele ya mambo haya ”, alisema Kardinali Parolin. “Tatizo leo hii ni kuweza kuzungumza na kusadikika, kwa sababu mara nyingi kila mmoja wetu hujisikiliza yeye mwenyewe au wale wanaofikiria na kuzungumza kama yeye. Hakuna juhudi za kuingilia  maoni ya wengine”. Badala yake, kulingana na Kardinali, “njia pekee ya kutoka katika hali hii ni kuambiana, jipe ​​moyo kwa sababu inafaa kupata chanjo kama suluhisho dhidi ya janga hili. Kiukweli, yeye anakubali  kwamba  “ni njia ndefu ambayo inahitaji uvumilivu, hasa wakati wa mapambano ambayo sielewi ”.

Mkutano wa Askofu Mkuu Gallagher na Seneta Salvini

Alipoulizwa na waandishi wa habari, katibu wa Vatican pia alijibu swali juu ya mkutano kati ya kiongozi wa  Chama cha Ligi, Italia Bwana Matteo Salvini, na katibu wa Uhusiano na Ushirikiano na Nchi Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, kama sehemu ya mikutano ambayo askofu mkuu mara kwa mara anafanya  na wabunge kutoka ulimwenguni kote. Kardinali amesema: “Sikuwepo kwenye mkutano huo, kwa hivyo siwezi kutoa maoni mengi, lakini Kardinali Parolin alisisitiza, kuwa alimsikia Askofu Mkuu Gallagher ambaye alimwambia kuwa yeye pia alikuwa na furaha na kwamba inawezekana, kwa njia ya utulivu, kupata vidokezo ya makubaliano hata kwenye masuala ya moto zaidi”. Miongoni mwa hayo, pia yalikuwa ni kuhusu hali ngumu nchini Afghanistan, na ambayo ilikuwa ni  sababu kuu ya mkutano.

Barabara za Roma kwa ajili ya hija kwa matazamio ya Jubilei 2025

Kardinali Parolin baadaye alitoa maoni yake juu ya itifaki iliyosainiwa asubuhi hiyo ambayo inajumuisha takriban Nchi kumi na tano na inakusudia kukuza ushirikiano katika kuhudumia mahujaji kutoka Ulaya yote ambao watasafiri kuja Roma kwa mwaka wa Jubilei 2025. “Hatutaki kuiteka nyara njia kwa mtazamo wa imani, kuna hali halisi  ya kiutamaduni ya wanadamu na kadhalika. Walakini, ningependa kusisitiza nafasi kubwa ya utaftaji wa imani ambayo mpango huu unawakilisha. Leo tuna shida ya kupata mitindo mipya za kutangaza Injili na hii ni moja wapo ya njia ambazo zinafunguliwa ili watu waweze kurudi kwao na kupata mambo ya ndani, na baadaye kuwa wazi katika pendekezo la Kikristo ambalo linapatikana kwa ukimya wa moyo na sio kwa kelele za nje”.

13 September 2021, 14:48