Tafuta

Kard.Parolin:Papa anaomba ushuhuda wa Kanisa kuupeleka ulimwenguni

Budapest na Slovakia wanasubiri Papa Francisko.Huko Šaštin atawakabidhi watu wote wenye kujikuta katika halli ya udhifu kwa Mama Maria,kwa mujibu wa Kardinali Parolin Katibu wa Vatican akihojiana na na mwandishi wa Vatican News.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa anajiandaa kuanza ziara yake ya kitume ya 34. Atafunga Kongamano la Ekaristi huko Budapest nchini Hungaria na kutembelea nchini Slovakia. Kuna matarajio makubwa na shauku ya kufika kwa mfuasi wa Petro. Kwa mujibu wa Kardinali Pietro Parolin Katibu wa Vatican katika mahojiano kufafanua ziara hii amesema kuna ziara mbili za kitume ambazo Papa mwenyewe alizitangaza wakati anarudi kutoka Iraq na ambazo zinatokana na shauku na kwa njia ya tafakari ya sala. Katika madhabahu ya kitaifa ya Mama maria huko Šaštin, kwa mujibu wa Katibu wa Vatican, itauiwa hija inayofanyika mara baada ya operesheni ya utumbo , na kwa namna nyingine ni katika kumshukuru Mama Maria kwa kufanikisha operesheni hiyo. Papa mwenyewe wakati wa mahojiano akirudi kutoka Iraq alikuwa ametangaza shauku yake na nia ambayo kama ilivyo mara nyingi katika safari hizi, ilizaliwa kutokana tafakari na sala. Shauku na nia ya kwenda kuadhimisha misa ya hitimisho la Kongamamo la Ekaristi kimataifa huko Budapest na ambalo lilikuwa limekwisha ahirishwa kwa sababu ya UVIKO- 19 na kutokana na ukaribu wa nchi mbili badi ukatoa hata nafasi ya kutembela Slovaki.

Kardinali Parolin akijibu swali kuhusu maneno ua Kardinali Erdo kwa ajili ya  nchi ya hungeria ambayo inahitaji mwanga wa imani na kuhisi udugu na watu wote, amesema,Kongamano zote za kiekaristi kwa kawaidia ni fursa ya kadhimisha, kutafakari, mafunzo na kujikita kwa kina katika fumbo la Ekaristi na kwa maana hiyo hata Kongamano la kimataifa huko Budapest ndiyo lengo lake. Kiukweli, katika siku hizi zote, za kusherehekea na za mafunzo zaidi, na za kujikita kwa kina zaidi. Kongamanano la Ekaristi lazima lipelekee baadaye katika maisha ambayo ni ya kiekaristi. Katika kutafakari  siku hizi, Kardinali Parolin arudia kusoma mahubri ya Papa Francisko aliyotoa huko Molfetta mnamo 2018 katika fursa ya miaka 25 tangu kifo cha don Tonino Bello. Kati ya mengine Kardinali ameongeza kusema kuwa Papa alisema kwamba “ kila parokia , kila Kanisa linapaswa liandike neno hili: baada ya misa si kuishi binafsi, bali kuishi kwa ajili ya wengine”, na kwa maana hiyo Kardinali Parolini anaamini kuwa ndiyo maana aliyokuwa anaamania Kardinali Erdo ambaye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu katoliki la Budapest….kwamba Ekaristi hutuzamisha katika upendo wa Kristo, katika maisha ya Kristo ambayo ni upendo wa vipimo vya ulimwengu wote, na kwa hivyo lazima ituwezeshe kumwona kila mtu, kwa kila mtu kuwa ni ndugu ambaye tunabeba mizigo yake.

Nchini Slovakia wanaompokea Papa ni watu ambao wako na kumbu kumbu za watakatifu Cirilly na Metodius: kwa namna hiyo ziara inaonesha  uwepo wa daraja la kiroho  la mazungumzo kati ya nchi za Mashariki na magharibi. Kardinali Parolin akifafanua  anakubalina na hilo kwa sabababu,amesema  Watakatifu  Sirilly na Matodius ni sura ambazo zina tabia yote ya historia ya kislovakia. Katika utangulizi wa katiba yao kama hakosei, inawazungumzia kuwa ni  Mababa wa Kiroho na utamadunia wa Taifa. Na Mtakatifu Yohane Paulo  II, katika Waraka wa  Slavorum Apostoli (2 Juni 1985) unaohusu kazi ya uinjilishi wa Mtakatifu Cirilly na Metodius anazungumza juu yao kama daraja kati ya Mashariki na Magharibi. “Tunachoweza kufahamu Watakatifu hawa  na  ujumbe wao ni wa sasa, wa kudumu, pamoja na mambo mengine, pia ni Walezi wa Ulaya, waliopendwa na Mtakatifu Ypohane Paulo  II. Kwa maana nyingine Walijua jinsi ya kuongea na watu wa wakati wao, walijua jinsi ya kutangaza Injili katika vikundi ambavyo wangeweza kukutana nao, na huu ni mwaliko wa kufanya kile ambacho Baba Mtakatifu Francisko ananomba kwa kila wakati anapozungumza juu ya Kanisa ambalo linapaswa kutoka nje,  Kanisa ambalo linapaswa kushughulikia kwa hakia na uinjilishaji wa ulimwengu: kulenga uinjilishaji wa ulimwengu kunamaanisha kupata lugha inayofaa ili ulimwengu uweze kupokea tangazo la Injili. Kwa hivyo, kwa upande mmoja utamaduni huu, harakati hii ya wamisionari, na kwa upande mwingine pia ukweli wa kujua jinsi ya kuingiza utofauti huu wa kiroho, wa aina za kiroho, na utamaduni wa lugha pia katika umoja wa Katoliki ambao unakuwa umoja lakini usio kama sare.

Ziara ya Papa Francisko inatazamia kukutana na jumuiya ya Warom, yaani watu wasio kuwa na makazi maalum, ikiwa ni ishara ya umakini wa Papa mbele ya hali halisi hii.  Kardinali amekumbusha juu ya mwendelezo wa mkutano huo kama ule ambao Papa alikwa nao huko nchini Romani miaka miwili iliyopita, na jumuiya ya Warom, na ambapo alielezea ukina wake wa moyo juu ya maumivu yote ya mateso ambayo jumuiya hii imekuwa nayo, na  kwamba jumuiya hii ililazimika kuvumilia kwa muda. Kwa njia hiyo ushiriki huu mzito wa Papa hasa katika maumivu ya watu pia na ombi la msamaha kwa jukumu kubwa ambalo tunaweza kuwa nalo, la Kanisa au watu wa Kanisa wanaweza kuwa  katika hali hii. “Na wakati huo huo pia inakuwa, kwa upande mmoja, umakini kwa idadi hii, kwa hivyo heshima, lakini pia shukrani kwa maadili ambayo wanaelezea na ni mengi: kutoka katika thamani ya familia hadi thamani ya mshikamano, ukarimu, utunzaji wa wazee na kadhalika, na kwa upande mwingine, kwa juhudi inayofanywa kuwaingiza na kuwaunganisha kikamilifu katika jamii”, Kardinali Parolin amesisitiza.

Papa Francisko wakati wa kuadhimisha misa katika Madhabahu ya Satin katika siku kuu ya Maria wa Mateso saba na msimamizi wa Slovakia, Kardinali amesema hii kwa hakika ndiyo imewezesha kuresha safari hii, ili kushiriki siku kuu ya watu wenyenye ibada kubwa kwa Msimamizi wa nchi ya Slovakia. Kardinali Parolin anaamini kwamba kwa upande mmoja hii ni ishara ya kuzingatia sana kwamba Papa amekuwa akitoa heshima kubwa, uaminifu kwa watu wengi lakini zaidi ya yote kujitoa kwa Mama yetu, ambaye alimjua na kukutana naye moja kwa moja huko Amerika Kusini, nchini Argentina, kidogo kwa kila mtu … nchi za bara hilo, lakini ambayo pia ina mizizi sana Ulaya. Madhabau ya Šaštin ni mfano wa jinsi kujitoa kwa Mama yetu; ni muhimu kwa maisha ya imani ya watu, ya jumuiya. Na wakati huo huo pia ni kusisitiza ukweli kwamba hii ni hija ambayo inafanyika baada ya upasuaji ambao Papa alioupata  kwa maana fulani pia kumshukuru Mama yetu, kwa hakika, kwa kufanikiwa kwa uingiliaji huu lakini pia kukabidhi  wale wote ambao hujikuta katika hali za udhaifu, mateso, hata kimwili, kama alivyopitia katika kipindi hiki, hasa kwa kuzingatia hali hiyo, hali ya janga ambalo kwa bahati mbaya, bado inaendelea kusababisha maumivu katika nchi nyingi .

Hatimaye Kardinali ameelezea juu ya Roho ya Papa ambayo anakwenda nayo kwenye ziara na kwamba aliitamka yeye mwenyewe, mara baada ya sala ya malaika wa Bwana  Dominika tarehe 5 Septemba 2021: “Ninayo shuku  kubwa kwa dhati ya kukutana na waamini hawa, kukutana na Makanisa haya”, pia kwa kuzingatia kwamba safari zake za kitume zimepungua kwa sababu ya Covid, Papa anahisi hitaji, hasa, kwa nguvu kuanza tena aina hii ya utumiaji wa huduma yake ya kipapa na uwezekano huu wa kuwasiliana na watu ambao huonesha mtindo wake na njia yake ya kuwa jinsi alivyo.

11 September 2021, 11:23