Tafuta

2021.09.07 Kardinali  Krajewski atembelea vijana kutoka Afghanistan huko Torbellamonaca, Roma. 2021.09.07 Kardinali  Krajewski atembelea vijana kutoka Afghanistan huko Torbellamonaca, Roma. 

Kard. Krajewski kati ya watoto wa Afghanstan Roma wanapata vipimo na kwenda shule

Kardinali Krajewski Msimamizi wa Sadaka ya Kitume kwa kusindikizwana na mmoja wa madakatari anayehudumia katika ofisi ya sadaka ya kipapa wamekwenda mchana katika mtaa moja Roma ya Tor Bella Monaca kwa ajili ya kufanya vipimo kwa watoto wa Afghanistan waliofika Italia wiki mbili zilizopita

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Walikuwa katika kujipati vipocho pocho vya mchana vijana 14 wa Afghanistan, 11 wa kike na 3 wavulana waliofika mjini Roma wiki mbili zilizopita. Walikuwa pamoja na kikundi cha watu wa kujitolea wa Tor Bella Monaca alipofika kwa ghafla mchana Msimamizi wa sadaka ya kitume ya Papa, Kardinali Konrad Krajewski,  akisindikizwa na Dk. Massimo Ralli na Dk. Leonardo Russo, waliojiwakilisha katika makao yao mapya, ambayo ni nyumba ya watawa wa kimisionari wa Upendo.

Shughuli ya kuchukua vipimo ilikuwa ni kufanya kila mtu, pamoja na watawa, pamoja na matokeo ya uchunguzi muhimu ili kuruhusu kikundi hiki kuhitimisha karantini na kuanza shughuli za shule na maisha yao nchini Italia. Walipofika Roma, walikuwa wamesindikizwa kutoka Afghanistan na Masista wanne wa Mama Teresa ambao waliwasaidia huko Kabul. Wote wenye umri kati ya miaka 6 na 22, waliachwa na familia zao kwa sababu walikuwa walemavu.

Mchana tofauti na mwingine

Walisubiri zamu yao huku wakivutiwa na maabara ndogo, iliyowekwa kwa dakika chache, nyuma ya kikanisa ambacho watawa kawaida hukusanyika kwa ajili ya  sala zao. Mchana  huo ulikuwa tofauti kwao pamoja na malaika wao walezi ambao hawawapotezi kamwe kwa mtazamo. Vipimo na msaada wa matibabu muhimu utafuatwa na taratibu za kutoa hati, hata kama, walivyo kwa Masista wa Mama Teresa, ambao wamekuwa wakihudumu katika moja ya vitongoji vigumu zaidi vya Roma tangu tarehe 6, Januari 1990, wamekwisha zoaea hata ukiritimba huo na kwa maanda hiyo kwao  ni mdogo. Ustawi na utulivu wa watoto unakuja kwanza kabla ya yote  na umakini wa moja kwa moja wa Baba Mtakatifu Francisko uliowafariji. Katika siku zijazo, kiukweli, mahitaji msingi pia yatawasilishwa ili kusaidia zaidi utume huo.

Ice crean elfu kumi na tano gerezani

Ziara ya Kardinali Krajewski kama hiyo  ni moja  ya hivi karibuni katika safu ya shughuli ziliozo hamasishwa katika miezi ya majira ya joto. Unaitwa  “Mkono wa upendo  wa Papa" ambao umefanya ishara ndogo za kiinjili kwa kusaidia na kuwapa matumaini maelfu ya watu katika magereza ya mji mkuu! Katika siku za hivi karibuni, Ice cream 15,000 zilitolewa kwa wafungwa wa magereza ya Regina Coeli na Rebibbia, Roma.  Na zaidi kama ilivyo kwa kila mwaka vikundi vidogo vidogo vya watu wasio na makazi maalum na wakaazi wa mabweni walisindikizwa hata baharini kuogela  au ziwa la Castel Gandolfo, kwa kupitisha mchana wa kupumzika na chakula cha jioni kwenye maeneo ya kuuza pizza.

Upendo wa Papa hata katika sehemu nyingine ulimwenguni

Hata Maskini katika sehemu nyingine za ulimwengu pia wameweza kufaidika na misaada kutoka Vatican. Misaada hiyo na kama vile  dawa, mashine za kupumulia mapafu na vifaa vingine vya matibabu. Katika mwezi wa Agosti pekee, tomografi ilinunuliwa kwa ajili ya Madagascar, yenye thamani ya dola 600,000, na maandalizi ya kliniki za matibabu, zilizosafishwa au kujengwa kutoka mwanzoni, kwa karibu gharama zilikamilishwa  euro 2,000,000, katika nchi maskini kabisa za Kiafrika.

08 September 2021, 09:52