Tafuta

Balozi Bernhard Erhard Kotsch tarehe 2 Septemba 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. Balozi Bernhard Erhard Kotsch tarehe 2 Septemba 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Francisko mjini Vatican. 

Balozi Bernhard Erhard Kotsch Awasilisha Hati za Utambulisho!

Balozi Bernhard Erhard Kotsch, alizaliwa tarehe 25 Agosti 1969 huko Regensburg, nchini Ujeruman. Baada ya masomo ya Sayansi ya Hesabu, Siasa na Historia kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 1999 alijiendeleza na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Siasa. Kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2002 alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. –Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Alhamisi, tarehe 2 Septemba 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Bwana Bernhard Erhard Kotsch, Balozi mpya wa Ujerumani mjini Vatican. Itakumbukwa kwamba, Balozi Bernhard Erhard Kotsch, alizaliwa tarehe 25 Agosti 1969 huko Regensburg, nchini Ujeruman. Baada ya masomo ya Sayansi ya Hesabu, Siasa na Historia kati ya mwaka 1995 hadi mwaka 1999 alijiendeleza na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamivu katika Sayansi ya Siasa. Kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2002 alifanya kazi katika Wizara ya Mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa Kimataifa nchini Ujerumani.

Katika maisha na utume wake, amewahi kufanya kazi katika ofisi ya uhusiano wa kimataifa, DCU kati ya mwaka 1997-2000. Balozi wa Ujerumani nchini Macedonia kunako mwaka 2000. Mkurugenzi wa uhusiano wa Kimataifa wa CDU kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2005. Kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2007 alifanya kazi kwenye Ofisi ya Chancela mjini Berlin. Kati ya mwaka 2007 hadi mwaka 2009 aliteuliwa kuwa Balozi wa Ujerumani nchini Senegal. Kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2018 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Chancela wa Ujerumani na kati ya Mwaka 2018 hadi mwaka 2021 aliteuliwa kuwa Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Chancella wa Ujerumani.

Balozi
02 September 2021, 15:00