Tafuta

Waamini nchini China wakiwa katika sala Waamini nchini China wakiwa katika sala 

Askofu mpya amewekwa wakfu nchini China

Ni Padre wa Kifransiskani,Cui Qingqi ambaye ni Askofu wa sita aliyechaguliwa na Papa Francisko kwa utaratibu wa mkataba wa makubaliano ya muda ya 2018 kati ya Vatican na China.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Vyombo vya habari Vatican Dk, Matteo Bruni, akijibu waandishi wa habari kuhusiana na kuwekwa wakfu kwa askofu mpya wa Hankou/Wuhan, nchini China amesema:  “Ninaweza kuthibitisha kuwa leo hii Jumatano tarehe 8 Septemba 2021, huko Wuhan, jimbo la Hubei nchini China kumeadhimisha misa ya kuwekwa wakfu, kwa Mhesh. Padre mfanciskani Cui Qingqi, O.F.M., aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa Askofu wa Hankou/Wuhan, mnamo tarehe 23 Juni 2021. Huyo ni Askofu wa sita wa china kuchaguliwa na kuwekwa wakfu katika muktadha wa Mkataba wa makubaliano ya muda juu ya kutangazwa kwa maaskofu nchini China”.

Mkataba wa makubaliano ya muda uliotiwa saini huko jijini Beijing mnamo tarehe 22 Septemba 2018 na wawakilishi wa Vatican pamoja na wa Jamhuri ya watu wa China, ni kwa matarajio ya kushirikishana ili kusaidia mchakato wa mazungumzo ya kitaasisi na kutoa mchango chanya wa maisha ya Kanisa katoliki nchini China kwa ajili ya wema wa watu wa China na kwa amani ulimwenguni.

Mkataba huo umeweza hata hivyo kupyaishwa kwa miaka miwili tena mnamo 2020 na ambao hautazami moja kwa moja masuala ya mahusiano ya kidiplomsia katika ya Vatican na China, na  wala sheria za Kanisa Katoliki nchini China au mahusiano kati Makleri na Mamlaka ya Nchi , badala yake unahusu mchakato wa kuteuliwa kwa maaskofu kwa lengo la kichungaji hasa hasa katika kuruhusu waamini katoliki wawe na maaskofu ambao wana muungano kamili na Mfuasi wa Mtakatifu Petro na wakati huo huo weweze kutambuliwa na mamlaka ya Jamhuri ya Watu wa China.

08 September 2021, 16:12