Tafuta

Bikita Maria Mpalizwa mbinguni mwili na roho. Bikita Maria Mpalizwa mbinguni mwili na roho. 

Tumezaliwa na hatutakufa kamwe,kifo ni mwelekeo wa mbingu!

Ifuatayo ni tafakari ya Padre Luigi Maria Epicoco,Msimamizi wa Kikanisa cha Makao ya Radio Vaticankuhusu Siku Kuu ya Kupalizwa Bikira Maria Mbinguni mwili na roho.“Tumezaliwa na hatutakufa kamwe kwa sababu kifo ni mwelekeo wa mbingu”.

Katika fursa ya Siku kuu ya Kupalizwa Bikira Mbinguni, Mama Maria tarehe 15 Agosti, Padre Luigi Maria Epicoco ametoa tafakari yake kupitia gazeti la Osservatore Romano akifafanua maana ya siku hii. Padre anaadikia kuwa “Kuna mwanga zaidi kuhusiana na sikukuu ya Kupalizwa kwa Maria mbinguni. Ni vigumu kubaki na mtazamo wazi. Ni kazi ngumu ambayo inahisiwa mbele ya Fumbo ambalo hatuwezi kufanikiwa kikamilifu katika kanuni sahihi, katika taalimungu yenye uwezo zaidi. Kwa kadri tunavyojaribu kutoa sauti na mwili kwa mafundisho ya Kikristo (miongoni mwake pia yale yanayomtaja hasa Maria), kitu cha pekee kilichobaki ni kuona kitu ambacho ni Fumbo hilo katika nuru kubwa. Hii ndiyo sababu tunaweza kusema kwamba sikukuu ya Kupalizwa Maria mbinguni ni moja ya siku kuu ambazo zinainjilisha mtazamo.

Hiki ni kuelekeza cha hali ya juu ambapo lazima tuangalie. “Tulizaliwa na hatutakufa tena”, aliandika mwanamke maarufu anayeitwa Chiara Corbella ambaye alituachia ushuhuda mzuri wa kimama, mke, mama na rafiki. Kwa sababu kifo ni mwelekeo tu wa mbingu ambao tunachukuliaa na kushangazwa na kidogo kuwa na hofu. Maria anayepalizwa mbinguni anatukumbusha kuwa huo ndio mwisho wetu, ambao ndio mahali tunaptarajia yaani hatima yetu. Na hii ndiyo sababu Maria kwa kila mmoja wetu ni ishara ya uhakika wa matumaini, kwa sababu ya kumtazama tunaelewa kidogo kile tutakachofanya hata sisi.

Liturujia inayosindikiza sikukuu ya leo inatufanya tusome kifungu cha Mwinjili Luka ambamo anasimuliza juu ya mkutano kati ya Maria na binamu wake Elizabeth (Lk 1, 39-56). Ni mkutano ambao matokeo yake kwa upande mwingine unaitwa furaha kwana: “Tazama, mara tu salamu yako iliponifikia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe tumboni mwangu”, anasema Elizabeth, na Maria anajibu: “Nafsi yangu yamtukuza Bwana”. Hii ni sifa ambayo inaonesha kuwa tumeumbwa kwa ajili ya mbinguni, ina inaweza kuonekana katika furaha tunayohisi na tunayoitoa. Mkristo ama anatoa furaha au yeye sio Mkristo. Lakini sio furaha ya kutabasamu tu, bali ni furaha ya kujua kwamba kwa hakika anapendwa.

Hata hivyo hii ni furaha ya wale wanaoweza kuona kwamba Mungu huwaangusha wenye nguvu kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuwakweza wanyenyekevu. Inatoa maarifa kwa wanyenyekevu na inachanganya mawazo ya wenye kiburi. Hutoa kwa wale wanaojitambua kuwa maskini na huwaacha wale wanaodhani wanajitosheleza na kuwaacha vinywa vitupu. Sikukuu ya leo, kwa maana hiyo, kama Pasaka ya pili ya Maria, inaangaza nuru ya matumaini juu ya hatima yetu. Nuru hii, hata hivyo, sio taa tu ambayo inazungumza nasi mambo y baadaye, lakini pia ni nuru ambayo inazungumza nasi mambo ya hapa na sasa! Kiukweli, ni pale hasa kwa kufikiria Maria kwamba maisha yetu yote sasa yanageuka kwa upya kuwa ya kina. Ndiyo maana Dante ana haki ya kusema juu ya Mariamu: “Wewe ni chemchemi hai ya tumaini”.

Jambo la mwisho linahusu “kashfa ya mwili”. Maadamu tunafikiria imani na maisha ya kiroho kama kitu kinachogusa roho zetu tu, kanuni zetu za kiroho, ya ndani, hatutapotoka sana kutoka katika uzoefu mwingine wa kidini. Lakini imani ya Kikristo ni imani katika “mwili wa Mfufuka”, ni imani katika ufufuo wa mwili. Ukweli kwamba Mariu yuko mbinguni, sio tu na roho yake bali na mwili wake, unatutafakarisha kwa kina juu ya imani yetu katika ufufuo. Ukristo unategemea au unaanguka hasa juu ya hili: juu ya kashfa ya mwili wetu ambao sio, kama Plato alivyosema, “kaburi la roho”, badala yake ni “hekalu la Roho Mtakatifu” (1 Wakor 6:13), pia, kwa maana tukiwa tunangojea ukombozi. Tunaweza kwa maana hiyo kuongeza leo kuwa hii ni sikukuu ya upatanisho na miili yetu.

14 August 2021, 16:08