Tafuta

2021.08.10 profesa Jennifer Anne Doudna 2021.08.10 profesa Jennifer Anne Doudna 

Mwanasayansi mwingine wa Nobel ya elimu ni Jennifer Anne Doudna

Kwa mara nyingine ni mwanamke mwingine mwanasayansi na profesa wa Kemia,ambaye amepewa utambuzi wa heshima na anaingia kuwa sehemu mjume wa Taasisi ya Vatican ya Sayansi iliyoanzishwa mnamo 1603.Amechaguliwa na Papa leo hii tarehe 11 Agosti 2021.

Kwa mara nyingine tena mwanamke, mwanasanyansi na Profesa wa Kemia anaingia kuwa sehemu ya wajumbe wa Baraza la Kipapa la Elimu ya Sayansi. Uteuzi mpya huu kwa ngazi ya juu kati ya washiriki wa kawaida wa Chuo cha Kisayansi cha Kipapa, taasisi ambayo iko Vatican inakubali uwanja wa sayansi safi, ikihimiza utafiti na maendeleo. Papa amemchagua Profesa Jennifer Anne Doudna, Profesa wa Chuo Kikuu cha California, Berkeley, Marekani.

Alizaliwa mnamo 1964 huko Washington. Profesa Doudna alimaliza masomo yake ya  Kemia katika Chuo cha Pomona huko Claremont, akibobea katika mafunzo ya Biokemia katika Shule ya Matibabu ya Harvard huko Cambridge; aliendelea na masomo yake katika Chuo Kikuu cha Colorado huko Boulder. Hivi sasa ni profesa wa Kemia ya Molekuli katika Chuo Kikuu cha California huko Berkeley Marekani.

Nobel shirikishi

Utambulisho wa kifahari wa Tuzo ya Nobel katika Kemia aliipokea mwaka jana 2020, kwa ajili ya maendeleo ya njia ya uhariri wa genome ya CRISPR-Cas9, ambayo ni hatua muhimu kati ya muhimu zaidi kwenye uwanja wa uhandisi wa maumbile unaoweza kuonesha kwa usahihi katika Utaratibu wa Vinasaba (DNA) vya wanyama, mimea na vijidudu na kusaidia kufungua njia mpya za matibabu ya magonjwa mengi.

Hata hivyo Profesa Doudna alishiriki Tuzo ya Nobel na mwenzake na mwanasayansi Mfaransa aliyebobea katika Biolojia, Microbiolojia , Biokemia na Jenetiki, Profesa Emmanuelle M. Charpentier, ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanachama wa Chuo hicho cha Kipapa na Papa Francisko. Kwa maana hiyo ni ushirikiano mpya na ushirikiano wa kisayansi pia Vatican, katika makao ambayo leo hii yanakaribisha wanasayansi na wasomi mashuhuri kutoka nchi 36 ulimwenguni.

Kutokana na uteuzi huu wanakuwa watu watatu kwa siku chache ambao wamechaguliwa na  Papa Francisko kama vile mwingine wa Tuzo za Nobel kwa Chuo cha Kipapa tangia tarehe 2 Agosti ni mwanasayansi wa Canada, Donna Theo Strickland, (62), profesa wa Fizikia ya macho katika Idara ya Fizikia na Unajimu wa Chuo Kikuu cha Waterloo. Mnamo 1985 alipewa heshima ya kifahari kwa kuwa alivumbua, pamoja na Profesa Mourou, mkusanyiko wa mapigo ya kinya kwa lasers.

11 August 2021, 16:42