Tafuta

Papa Francisko katika picha ya pamoja wakati wa kukutana na maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya China wakati wa hija yao ya kitume mnamo 2018 Papa Francisko katika picha ya pamoja wakati wa kukutana na maaskofu wa Baraza la Maaskofu wa Kanda ya China wakati wa hija yao ya kitume mnamo 2018  

Kard.Parolin:fahari ya ushuhuda wa imani ya Wakatoliki wa China

Katika mahojiano na jarida la kila siku katika mtandao wa Trentino,mahali ambapo yuko kwenye likizo,Katibu mkuu wa Vatican anazungumzia juu ya masuala kadhaa ya mada za sasa:kutoka uhusiano na China hadi kuanza kwa huduma yake Papa tena mara baada ya operesheni,vile vile kwa heshima ambayo inahusiana na Rais Mattarella,ambaye amefikia mwisho wa uongozi wake kama rais wa Italia.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika kipindi cha mwezi Agosti, ajenda za viongozi zilizo nyingi zimefungwa au zinasasishwa taratibu, japokuwa hawendi likizo. Hayo yanaweza kuonekana haa kwa umabli mahali pa maeneno ya kawaida ya nafasi zao kuwato hata kwa mbali katika makao na katika maeneo ya kawaidia ya nafasi zao walipo: ya kwanza ni mhudumu wa Papa ambaye yupo na amejikuta anasasisha masuala mbali mbali ya kimataifa. Imetokea kwa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, aliyehojiwa na Gazeti la Kila siku liitwalo 'La Voce del Nordest' yaani sauti ya kila siku Kaskazini Mashariki, mahojiano yaliyowekwa kwenye mtandao wa Trentino, mahali ambapo Katibu wa Vatican anapumzika.

China, mazungumzo ya mapinduzi

Kati ya mada zilizoguswa na Kardinali Parolin ni kuhusu uhusiano na China. Kardinli amesema daima wapo katika hatua ya mazungumzo kwa kukumbusha Mkataba wa Beinjing  uliotiwa saini mnamo 2018 na kupyaishwa  kwa miaka miwili tena mnamo 2020. Kwa mujibu wa Kardinali amethibitisha kuwa janga la Uviko-19  limegusa hata mantiki hiyo na kufanya ngumu wa kukabiliana moja kwa moja lakini ni matumaini yake kuweza kuanza kwa upya mikutano na kuweza kujihusisha na masuala mengine yaliyo kwenye jamvi na ambayo yanahusu Kanisa Katoliki nchini China. Kwa upande wa Wakatoliki wa Nchi hiyo kubwa ya bara la Asia, Katibu wa Vatican ameonesha ukaribu wa sala,  lakini zaidi hata mshangao kwani amesema: “ tuna fahari ya ushuhuda wa imani wanayotoa. Ni matumani kuwa wanaiweza kuwa wazalendo wema na wakatoliki wema daima ambao wanajua kufafanua hukuu huo  wa aina mbili hata katika maisha yao ya dhati ya kawaida.

Ujumbe wa Papa unafungua peo za ulimwengu

Katika ujumbe uliofuata baada ya makubaliano ya muda na  China kuna sentensi ya Kardinali Parolin aliyokuwa ametamka katika mahojiano, hasa ilipotokea manung’uniko ya  kichini chini kuhusu Papa kutokana na kufanya ufunguzi na Mashariki, ambapo Kardinali alikuwa amesema kuwa “nchi za Magaharibi lazima ziombe msamaha Papa”. Akiombwa arudi katika mtazamo wa sentensi hiyo, Kardinali Parolin  amebainisha kwamba "tangazo la Kiinjili ambalo  linasikika katika maeneno yake Papa Francisko , labda mara nyingi halikubaliki na hata kwa mapendekezo yake,na  ujumbe wake". Pamoja na hayo Papa yupo anaelekeza njia, na hasa kwa sasa amefanya hivyo na ndugu wote mara baada ya janga la uviko , ambalo linaweza kutusaidia kutoka katika ukavu ndani ya jamii zetu na kuelekeza kujenga ulimwengu mpya, ulimwengu ulio bora", amsisitiza Kardinali Parolin.

Afya ya Papa, na sifa kwa Rais Mattarella

Kuhusiana na swali linalohusu afya ya Papa Francisko baada ya kufanyiwa opereshini katika hospitali ya Gemelli, Roma mnamo tarehe 4 Julai 2021 iliyopita, Kardinali amethibitisha kuwa "anaendelea taratibu kurudisha afya yake, japokuwa inahitaji muda hata yeye, lakini anaonekana kuendelea vizuri. Hii inaoneshwa, na ahadi zilizoanza tena, kwa mfano katekesi  lakini pia safari iliyopangwa mnamo Septemba na vituo vyake atakavyosimama huko  Hungary na Slovakia". Kardinali Parolin pia alikuwa na maneno ya  kutoa shukrani na mapendo kwa Rais wa Italia, Bwana Sergio Mattarella, ambaye amefikia wakati wake wa kung'atuka madarakani  kwa kipindi chake cha miaka saba. Amefafanua kwamba amekuwa na furaha kwake kukutana naye, hasa kwa sababu ya hali yake ya juu ya maadili ya kirohona  ambayo anaelezea na kwa utume aliotimiza katika miaka ya hivi karibuni  hasa kipindi cha mwisho, klicho kigumu zaidi na ambacho amejua kweli kuonesha ubora wa Italia na kutoa dalili za kutosha sana za utatuzi wa  matatizo. .Ujumbe wa mwisho ulihusu ratiba zake  zinazokuja za Kardinali Parolin, pamoja na safari ya karibu kwenda Lithuania kwa kumweka wakfu balozi mpya  wa kitume nchini  Ukraine.

12 August 2021, 19:19