Tafuta

Ni kukutana, mazungumzo, muungano wa upendo na maisha ya mwamini na Yesu Kristo, Njia, Ukweli na Uzima (taz. Yoh 14: 6). Ni kukutana, mazungumzo, muungano wa upendo na maisha ya mwamini na Yesu Kristo, Njia, Ukweli na Uzima (taz. Yoh 14: 6).  

Ecclesiam suam na Veritatis splendor,nyaraka mbili juu ya mazungumzo ya ukweli

Nyaraka zote mbili zenye tarehe moja 6 Agosti katika Siku Kuu ya Kung’ara kwa Bwana ni nyaraka mbili ya Mtakatifu Paulo VI(1964 na Yohane Paulo II(1993).Kwa umbali wa miaka 29 miongoni mwa masuala mengine zinakabiliana na tema ya uhusiano wa Kanisa na utumaduni wa kisasa.

Sergio Centofanti

Ecclesiam suam ulikuwa ni Waraka wa kwanza wa Mtakatifu Paulo VI uliochapishwa mnamo tarehe 6 Agosti 1964 ambao uliandikwa wakati wa Mtaguso wa Pili wa Vatican. Kwa maana hiyo Ecclesiam suam, waraka unaohusu njia zipi za Kanisa Katoliki linavyopaswa leo hii kutimiza utume wake ulikuwa ni mpango mzima wa Papa Montini ambaye alitamani Kanisa lililo wazi katika mazungumza na ulimwengu kuanzia na utambulisho wake kikristo. Ni Waraka wa mazungumzo yenye msingi wake juu ya ukweli.

Na wakati huo huo Waraka wa Veritatis splendor uliochapishwa tarehe 6 Agosti 1993 ulikuwa ni wa kumi wa Mtakatifu Yohane Paulo II na unakusudia kuthibitisha hoja thabiti za mafundisho Katoliki katika kipindi kinachozidi kuongezeka kwa ubadilishwaji katika nyanja ya maadili. Ni waraka juu ya ukweli ulio na msingi wake   juu ya mazungumzo yale ambayo kwamba yalikuwa kati ya Yesu na yule kijana tajiri. Maandishi yanaanza kutoka katika kifungu cha Injili ya Matayo 19:16-21. Nyaraka zote mbili katika fursa ya  Siku Kuu ya Kung’ara, ni katika kuonesha mwanga wa kweli kuwa ni Yesu, ukweli ambao unajikita katika mazungumzo kati ya Musa na Elia. Ni Yesu ambaye anatimiza Sheria na Manabii.

Paolo VI:dunia haiwezi kujiokoa kutoka nje

Papa Paulo VI anasisitiza udharura wa kupeleka Injili ulimwenguni. Hapa kuna mazungumzo: “Ulimwengu hauokolewi kutoka nje; inahitajika, kama Neno la Mungu aliyefanyika mtu, kujitambulisha, kwa kiwango fulani, katika aina ya maisha ya wale ambao mtu anataka kuwapelekea ujumbe wa Kristo, na hata kabla ya kuzungumza lazima"asikilize sauti, na zaidi moyo wa mwanadamu; kuilewa, na kadiri inavyowezekana kuiheshimu na inapostahili kwenda nayo. Lazima tuwe ndugu wa watu kwa kitendo ambacho tunataka kuwa wachungaji wao na baba na waalimu. Hali ya mazungumzo ni urafiki. Kwa hakika ni huduma (Es 90).

Mazungumzo yanaundwa na upole, sio ya kukarisika wala ya kukera

Mazungumzo hayapunguzi ukweli, lakini yameundwa na “haki, heshima, huruma, wema kwa upande wa wale walioanzisha; hayajumuishi kulaaniwa kwa haki, kukera na tabia mbaya (Es 81). Tabia nyingine ya mazungumzo ni upole kwani “Mazungumzo hayajivuni, sio ya kukasirika, na hayachukizi. Mamlaka yake ni ya ndani kwa ajili ya ukweli unaofunua, kwa upendo ambao unaeneza kwa mfano anaopendekeza; sio amri, sio kulazimisha. Ni ya amani; yanaepuka njia za vurugu; yana uvumilivu; yana ukarimu. Uaminifu, kwa wema wa neno la mtu mwenyewe, na kwa mtazamo wa mshiriki anayemkaribisha: yanahamasisha ujasiri na urafiki; yanaingiliana na roho katika kushikamana kwa wema, ambao haujumuishi malengo yoyote ya ubinafsi (Es 83). Katika mazungumzo, yaliyofanywa kwa njia hiyo, umoja wa ukweli na upendo, wa akili na upendo unafanikiwa (Es 85).

Mazungumzo kama zoezi la uvumilivu na utafiti wa kina

Katika mazungumzo anaandika Papa  Paulo VI kuwa tunagundua jinsi njia ambazo zinaongoza kwenye nuru ya imani ni tofauti, na jinsi inavyowezekana kuungana ili kufikia mwisho huo. Hata zikitofautiana, zinaweza kuwa za ziada, zikisukuma hoja zetu kutoka katika njia za pamoja na kuimarisha utafiti wake na kufanya upya maoni yake. Haja ya zoezi hili la mawazo na uvumilivu litatufanya kugundua mambo ya ukweli hata kwa maoni ya wengine, itatulazimu kuelezea mafundisho yetu kwa uaminifu mkubwa na itatupa sifa kwa juhudi ya kuifunua katika pingamizi la wengine, polepole na  wengine. Yatatufanya tuwe na hekima, na kutufanya kuwa walimu ”(Es 86).

Hakuna mtu mgeni katika moyo wa Kanisa

Papa Montini anaiita mazungumzo ya wokovu. Hayo yanatii mahitaji ya majaribio, huchagua njia za kupendeza, hayafungamani na upendeleo wa bure, hayarekebishiki kwa misemo isiyo na mwenendo, wakati zinapopoteza sifa ya kuongea na kuhamasisha watu ”(Es 88). Ni mazungumzo ambayo Kanisa linataka kusuka na kila mtu: “Hakuna mtu mgeni wa moyo wake. Hakuna mtu asiyejali huduma yake. Hakuna mtu ambaye ni adui yake ambaye yeye mwenyewe hataki kuwa mmoja”(ES 98).

Yohane Paulo II: upendo zaidi ya tafsiri ya kisheria

Mazungumzo ya kiinjili yamejaa utukufu wote katika Waraka wa Veritatis splendor wa Papa Yohane Paulo II. Kijana tajiri alimwuuliza Yesu swali hili: “Bwana, nifanye nini kizuri ili nipate  uzima wa milele? (Mt 19:16). Hili sio swali la “mtego, kama lile lililoulizwa na  Mafarisayo, lakini ni swali la utimilifu na maana ya maisha” (Vs 7). Mtu huyo anaheshimu sheria, lakini alikwenda akiwa na huzuni baada ya kukutana na Kristo, “sheria hai” ambayo inaonesha njia ya kweli ya upendo, zaidi ya “tafsiri ya sheria ya amri” (Vs 16). Kijana huyo anamtafuta Yesu na anazungumza naye, lakini kile kinachoombwa kwake kinaonekana ni kikubwa sana yaani ukamilifu katika kupenda. “Hakuna juhudi za kibinadamu, hata utunzaji wa amri, unaweza kutimiza “Sheria”, anaelezea Papa Wojtyla, kwa sababu utimilifu wake “unaweza kutokana na zawadi ya Mungu (Vs 11). Walakini, anabainisha kuwa “mtu anaweza 'kubaki' katika mapenzi tu kwa sharti la kutii amri” (Vs 24).

Hakuna dhambi ya mwanadamu inayofuta huruma ya Mungu

Katika suala hili, Papa Paulo II, alikabiliwa na shinikizo la ubadilishaji imani, na hivyo anasisitizia hitaji la kutetea ukweli wa Kikristo katika nyanja ya maadili na anazungumza juu ya “kanuni adili za ulimwengu na zisizobadilika, ambazo wakati mwingine zinahitaji juhudi kubwa na kujitoa sadaka. Katika muktadha huo zinafunguliwa nafasi mbili: ile ya matumaini, kwa msaada wa neema ya kimungu, na ile ya huruma ya Mungu mbele ya udhaifu wa kibinadamu. Yesu “alikuja sio kulaani lakini kusamehe, kutumia huruma” na “hakuna dhambi ya kibinadamu inayoweza kufuta huruma ya Mungu,  kuzuia nguvu zake zote za ushindi, ikiwa tu tutaiomba” (Vs 118). Maadili ya Kikristo anathibitisha yanajumuisha, kwa urahisi wa uinjilishaji, katika kumfuata Yesu Kristo, kwa kujiachia kwake, kwa kujiruhusu kubadilishwa na neema yake na kufanywa upya na huruma  yake” (Vs 119).

Akili ya imani inakua

Kuna kanuni zisizobadilika, lakini ukweli ni wa nguvu. Kama Katekisimu ya Kanisa Katoliki (108) inavyosema, imani ya Kikristo sio “dini ya Kitabu” lakini lakini ni dini ya “Neno” la Mungu: la Neno ambalo sio “neno lililoandikwa na bubu, lakini ni Neno lililomwilishwa na linaishi”. Kwa kuwa ni Neno hai, linaendelea kuzungumza nasi. Kwa hivyo, Yohane Paulo II anakumbusha kwamba kinachopaswa kutetewa ni Utamaduni hai ule ambao unatoka kwa Mitume na “unaendelea katika Kanisa chini ya msaada wa Roho Mtakatifu”: na kwa shukrani kwa hatua ya Roho , na linaendeleza “Tafsiri halisi ya sheria ya Bwana"” iliyokabidhiwa kwa “Majisteriamu hai ya Kanisa”. “Roho yule yule, ambaye ni asili ya kufunuliwa kwa amri na mafundisho ya Yesu, anahakikisha kuwa lazima kuhifadhiwa kitakatifu, kufunuliwa wazi na kutumiwa kwa usahihi katika nyakati na hali zinazobadilika. Utekelezaji huu wa amri ni ishara na tunda la kupenya zaidi kwa Ufunuo na ufahamu katika mwanga wa imani ya hali mpya za kihistoria na kiutamaduni (Vs 27). Kwa dhati akili ya imani hukua katika kipindi.

Imani ni mazungumzo na muungano wa upendo na Yesu

Mazungumzo kati ya Yesu na yule kijana tajiri yanatukumbusha kwamba ni Kristo tu, ukweli aliyefanyika mwili, ndiye chanzo cha furaha ya kweli, “jibu pekee linalokidhi kabisa hamu ya moyo wa mwanadamu” (MST 7). Yohane  Paulo II anaalika Kanisa kuonesha, kwanza kabisa, uzuri wa imani, “uzuri wa kuvutia wa ule ukweli ambao ni Yesu Kristo mwenyewe” (MST 83). “Ni muhimu kupona na kupendekeza tena sura ya kweli ya imani ya Kikristo - anathibitisha - ambayo sio tu seti ya mapendekezo ya kukubalika na kuridhiwa na akili. Badala yake, ni ujuzi ulioishi wa Kristo, kumbukumbu hai ya amri zake, ukweli wa kuishi. Kwa kuongezea, neno halikubaliki kweli isipokuwa linapita katika vitendo, ikiwa sio wakati linatumika. Imani ni uamuzi ambao unashirikisha maisha yote. Ni kukutana, mazungumzo, muungano wa upendo na maisha ya mwamini na Yesu Kristo, Njia, Ukweli na Uzima (taz. Yoh 14: 6). Inajumuisha tendo la kumwamini na kujiachia kwa Kristo, na kutuwezesha kuishi kama alivyoishi (rej. Gal 2:20), ambayo ni, katika kumpenda Mungu na ndugu zetu”(Vs 88).

ECCLESIAM SUA NA VERITATIS SPLENDOR
06 August 2021, 16:38