Amoris laetitia,ndoa ni sura ya upendo wa Mungu
Amoris laetitia (n. 120-164)
Kukua katika upendo wa wanandoa
Katika kifungu cha 120, kinaelezwa hivi: Wimbo wa Mtakatifu Paulo, ambao tumezungumzia, unaturuhusu kuendelea na upendo wa kindoa. Ni upendo unaounganisha wenzi wa ndoa, waliotakaswa, wenye utajiri na wenye nuru ya neema ya sakramenti ya ndoa. Ni “muungano unaofaa”, wa kiroho na wa kujitoa, ambao hata hivyo hukusanya ndani mwake ule upole wa urafiki na shauku ya kupendana kimapenzi, ingawa hiyo iwe na uwezo wa kuwapo hata wakati hisia na shauku zinapodhoofika. Papa Pio XI alifundisha kwamba, upendo kama huo upo katika majukumu yote ya maisha ya ndoa na unazingatiwa kama ukuu wote wa wakuu”. Kwa dhati upendo huu wenye nguvu, uliovuviwa na Roho Mtakatifu, ni kielelezo cha Agano lisiloweza kuharibika kati ya Kristo na ubinadamu, na kuishia kwa kujitoa hadi mwisho, msalabani: “Roho, ambayo Bwana uvuvia inatoa moyo mpya na hufanya mwanamume na mwanamke waweze kupendana kama vile Kristo alivyotupenda. Upendo wa wenzi unafikia utimilifu ambao umeamriwa mambo ya ndani, yaani upendo wa kindoa”.
Kwa maelezo zaidi ingia katika wavuti wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha: