Tafuta

Askofu Mkuu Henryk Hoser, Mstaafu wa  Praga (Poland) Askofu Mkuu Henryk Hoser, Mstaafu wa Praga (Poland) 

Askofu Mkuu Hoser,mjumbe wa kitume huko Medjugorje amefariki!

Baba Mtakatifu Francisko alikuwa amemtuma katika kituo kidogo cha Bosnia-Herzegovina kusindikiza jumuiy ya parokia na mahujaji bila kuingilia masuala ya matokeo ya Bikira Maria.Kwa mujibu wake Monsinyo Hosa alisema wengi wanakuja kukutana na Yesu kupitia Maria.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Askofu mkuu wa Kipoland Henryk Hoser, ambaye alikuwa ni mjumbe wa kitume wa parokia ya Medjugorje tangu 2018, ameaga dunia Ijumaa tarehe 13 Agosti 2021, katika Hospitali ya Wizara ya Mambo ya Ndani huko Warsaw, ambapo alikuwa na umri wa miaka 78. Hii imetangazwa na Baraza la Maaskofu wa Poland. Alikuwa ameambukizwa na Uviko-19 na alikuwa katika harakati za kupata nafuu, wakati alipopata tena maambukizi ambayo yaliendelea kuathiri utendaji wa viungo vingine, hadi alipolazwa hospitalini katika siku chache zilizopita. Mazishi yatafanyika Ijumaa tarehe 20 Agosti 2021  katika Kanisa Kuu la Warsaw-Praga.

Papa Francisko alikuwa amemkabidhi jukumu la kusindikiza kwa njia thabiti na endelevu ya  ya parokia ya mji huu mdogo huko Bosnia-Herzegovina na waamini wengi ambao huenda huko katika hija, ambao mahitaji yao yanahitaji umakini wa kipekee, kama maelezo ya barua ya Vatican. Ni ishara ya uangalifu wa Papa kwa mahujaji, kwani Msemaji wa Vyombo vya Wanahabari ya Vatican  alikuwa amesema wakati huo kuwa  "Askofu Mkuu Hoser alitumwa kwenda Medjugorje na jukumu madhubuti la kichungaji, bila kuingliia kwenye suala  la kutokea kwa Mara". Na kiongozi huyo alikuwa amethibtisha kwamba "Papa anatutuma pale, ambako watu wanaishi, ambapo waamin hukusanyika kutafuta nuru ya wokovu na katika mahujaji wa Medjugorje wanafika kutoka ulimwenguni kote kukutana na mtu,  kukutana na Mungu, kukutana Kristo, kukutana na mama yake".

Njia ya Maria alisema Hoser  ndiyo ya uhakika na salama zaidi kwa sababu inaongoza kwenda kwa Yesu na hapa waamini wana kitovu cha Misa Takatifu, kuabudu Sakramenti, na mlolongo mkubwa wa Sakramenti ya Kitubio. Ni ibada ya kweli,  kiini cha Kristo. Kwa mujibu wa mjumbe huyo rasimi wa kitume alikuwa amesema huko Medjugorje kuwa "hutupatia wakati, na nafasi ya neema ya kimungu kupitia maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Mungu na Mama wa Kanisa, anayeheshimiwa hapo kwa  jina la 'Malkia wa Amani'. Jina hili linajulikana kupitia Litania ya Loreto. Na ulimwengu unahitaji sana amani."

Askofu Mkuu Hoser alizaliwa huko Warsaw mnamo Novemba 27, 1942, alikuwa amesomea udaktari kabla ya kujiunga naShirika la  Kitume Katoliki (Pallottini) mnamo 1969. Alipewa daraja la Upadre  mnamo 1974 na kwenda  kama mmisionari nchini Rwanda, ambapo alikaa huko hadi 1995. Akiwa Kigali alianzisha Kituo cha Matibabu na Jamii, akikiongoza kwa miaka 17 na Kituo cha Mafunzo ya Familia. Kwa miaka kadhaa alikuwa katibu wa Tume ya Afya ya Baraza la Maaskofu, pia Tume ya Maaskofu ya Familia, rais wa Chama cha Vituo vya Matibabu vinavyohusika huko Kigali (BUFMAR), na aliyehusika na kituo cha ufuatiliaji wa magonjwa ya UKIMWI na mpango wa msaada wa kisaikolojia- matibabu na kijamii ya wagonjwa. Mnamo 1994 aliteuliwa kama mtaalam katika uwanja wa familia na maendeleo katika Sinodi Maalum ya Afrika. Pia mnamo 1994, kwa kukosekana kwa Balozi wa kitume nchini Rwanda, aliteuliwa kuwa mwakilisho wa kitume katika nchi hiyo, ofisi aliyoshikilia kwa zaidi ya miaka miwili.

Na katika mahojiano kadhaa anakumbukwa kujitoa kwa Kanisa Katoliki kwa ajili ya upatanisho na dhidi ya vurugu nchini: kwa namna ya pekee  alisisitiza kwamba katika mauaji yale  ya kimbari ambayo yalipoteza maaskofu wanne, mapadre 150, karibu robo ya mapadre wa mahali hapo, na watawa 140 walipoteza maisha yao, vile vile kama mamia ya maelfu ya waamini walei, wote Wahutu na Watutsi.

Utume wake Ulaya

Tangu mwaka 1996 hadi 2003 alikuwa mkuu wa kanda ya wapallottini na mshiriki wa Baraza la Wamisionari wa Baraza la Wakuu wa Mashirika huko Ufaransa. Mnamo 2004 alikuwa msimamizi wa Ofisi ya umisionari wa wapallottini, huko Brussels, Ubelgiji, na alihusika katika usimamizi wa kichungaji ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Mnamo 2005 Mtakatifu Yohane Paulo II alimteua kuwa katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu na rais wa shughuli za Kimisionari za kipapa na kuwa na hadhi ya askofu mkuu. Mnamo 2008, Papa Mstaafu Benedikto XVI, alimchagua kuwa Askofu Mkuu wa Majimbo ya Warsaw -Praga.

Ikumbukwe ilikuwa Februari 2017, Papa Francisko alipomtuma Medjugorje kama mjumbe maalum wa Vatican. Mnamo Desemba iliyofuata akawa askofu mstaafu wa Warsaw-Praga. Mnamo 31 Mei 2018, Papa alimteua kama mjumbe wa kitume na mhusika maalum kwa parokia ya Medjugorje, kwa kipindi kisichojulikana na ad nutum Sanctae Sedis. Askofu Mkuu Hoser ametoweka katika mwaka wa 40 tu baada yale yote yaliyotokwa huko Medjugorje, ambapo ni mnamo 24 Juni 1981 vijana kadhaa walisema kuwa  wamemwona Bikira Maria.

14 August 2021, 15:33