Tafuta

Mazishi yaPadre Bernd Hagenkord SJ, aliyekuwa ni mkurugenzi wa matangazo ya idhaa ya kijerumani ya  Radio Vatican/Vatican News na mjembe wa CEM Monaco, 2.8.2021 Mazishi yaPadre Bernd Hagenkord SJ, aliyekuwa ni mkurugenzi wa matangazo ya idhaa ya kijerumani ya Radio Vatican/Vatican News na mjembe wa CEM Monaco, 2.8.2021 

Mazishi ya Pardre Bernd Hagenkord S.J huko Monaco ya Baviera

Leo asubuhi yamefanyika mazishi ya Padre Bernd Hagenkord S.J.,huko Monaco ya Baviera nchini Ujerumani ambapo kati ya washiriki waliotuwakilisha walikuwapo Gudrun Sailer na Christine Seuss,ambao wameweka shada la maua kutoka Jumuiya yetu ya kazi.Mungu ampumzishe kwa Amani.

Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 2 Agosti 2021 asubuhi yamefanyika mazishi ya Padre Bernd Hagenkord S.J., huko Monaco ya Baviera ambapo kati ya washiriki walikuwapo Gudrun Sailer na  Christine Seuss, kwa kuweka shada la maua kutoka kutoka Jumuiya  yetu ya kazi ya Radio Vatican. Kifo cha Padre Bernd kilitokea tarehe 26 Juali 2021. Ametuachia pengo kubwa ambalo siyo rahisi kusahulika.

Zifuatazo ni  picha kuonesha kilicho jiri asubuhi ya tarehe 2 Agosti 2021

Geneza la mwili wa Padre Bernd Hagenkord Sj
Geneza la mwili wa Padre Bernd Hagenkord Sj

Wakati geneza la mwili wake likiwa linashushwa kwenye kaburi katika bustani ya maziko..

Geneza la mwili wa Padre Bernd Hagenkord Sj likishushwa
Geneza la mwili wa Padre Bernd Hagenkord Sj likishushwa

JE ALIKUWA NI NANI PADRE BERND?

Kwa mtazamo wa kwanza alikuwa ni mrefu, sura nzuri, sauti nzito, mara nyingi katika mavazi yake rasmi na ungeweza kufikiria kuwani mgeni kaingia ofisini  au kwa wengine kuonekana kama mmoja wa waigizaji au maarufu, kwa wale ambao mara nyingi walikuwa wanazunguka kwenye korido za jumba la Pio huku wakisubiri kuingia kwenye studio katika mahojiano kabla ya kuzuia kutokana na  Covid. Hakuwa mwingine mgeni yeyote yule bali ni Padre Bernd Hagenkord,SJ mtumishi mdogo wa Radio ya Papa.

 Padre Bernd Hagenkord Sj
Padre Bernd Hagenkord Sj

Ugonjwa umemnyakua asubuhi ya tarehe 26 Julai 2021 akiwa na umri wa miaka 52 akiwa katikati ya mapenzi ya wengi ambao wamsindikiza kwa siki na dakika za mwisho wa maisha yake hasa familia ya kijesuit aliyojiunga nayo mnamo 1992 akiwa na umri wa miaka 24 na wenzake katika vyombo vya habari Vatican. Pamoja na harakati za matibabu hakuweza kupona muda mfupi baada ya kutoka Roma kurudi Ujerumani, mahali alipozaliwa mnamo tarehe 4 Oktoba 1968 huko Hamm, karibu na Dusseldorf.

Padre Bernd alifika Roma mnamo 2009 na alikuwa shabiki mkubwa wa uandishi wa habari, ambapo kwa haraka alichukua mwelekeo wa mipango ya vipindi vya lugha ya Kijerumani vya utangazaji wa Radio Vatican.  Akiwa kuhani tangu 2002, alikuwa amepewa daraja hilo huko Kolon, nyuma ya mabage yake namasomo ya kifalsafa, taalimungu, historia ya Kanisa na uandishi wa habari karibu na mji wa Hamburg, Munich na London. Hata hivyo Kolon ni jiji ambalo lilimuandaa kusoma Kiitaliano na kwa mafunzo katika Domradio kwa ajili ya shughuli ambayo shirika lilikuwa linamwandaa kumtuma kwenye shughuli za kipapa wakati wa kipindi cha Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI. Miaka kumi ya kazi imemfanya Padre Hagenkord athaminiwe na sio tu na wenzi wake katika kipaza sauti kwa wanaozungumza Kijerumani, ambao walimsifu si tu kwa utaalam wake lakini pia alikuwa na  sifa za kibinadamu na  mara nyingi ndiye alikuwa najitolea kufunika zamu zinazohitaji sana kwa ajili ya  wenzake, labda kwenye hafla kubwa na siku kuu  kwa mfano kwa wenye familia baba na mama waweze kuwa na wapendwa wao nyumbani.

 Padre Bernd Hagenkord Sj
Padre Bernd Hagenkord Sj

Padri Bernd polepole amechora nafasi za heshima kubwa katika ofisi nyingine za wahariri, ambazo katika Jumba la Pio, lenye kujaa lugha na tamaduni kadhaa zikishirikiana ikiwa inamaanisha juu ya ulimwengu  wote. Amewahi kuwa mratibu wa Wajesuit wanaofanya kazi katika Redio ya Vatican, iliyokabidhiwa kwa Shirika ya Yesu liloloanzishwa na Mtakatifu Ignatius wa Loyola hadi mageuzi ya vyombo vya habari Vatican kwa utashi wa Papa Francisko. Ameishi hadi mwisho wa maisha yake na busara, ambayo ni ya asili na iliyotafutwa, akiwa na akili yake ya kujitoa na kusimamia kile kilichompata. Vile vile kipande cha moyo wake ambacho amekiacha Roma, mpendwa na Warumi, inakumbukwa hata picha nzuri sana kwenye wasifu wake wa Instagram. Kwenye mlango wa ofisi yake, baada ya kufika Roma, alikuwa ametundika alama ya neno hili: Nafasi ya bure ya imani. Kwa sasa maandiko hayo hayapo tena na hayana maana kwa sababu urithi wake sasa umechapishwa ndani ya mioyo yetu na ya kila mmoja aliyeweza kukaa naye, kumsikiliza na kupata ushauri wake. Raha ya milele uumpe Ee Bwana Padre Bernd Hagenkord na mwanga wa milele umwangazie apumzike kwa amani, Amina.

31 July 2021, 15:01