Tafuta

Papa Francisko amemteua Padre Peter Nworie Chukwu kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Abakaliki nchini Nigeria. Papa Francisko amemteua Padre Peter Nworie Chukwu kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Abakaliki nchini Nigeria. 

Askofu Peter Nworie Chukwu Jimbo Katoliki la Abakaliki, Nigeria

Askofu mteule Peter Nworie Chukwu alizaliwa mwaka 1965, Jimboni Abakaliki. Tarehe 13 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo kama Padre, ameweza kuwatumikia watu wa Mungu Jimboni Abakaliki kama: Paroko-usu, Gambera Msaidizi wa Seminari St. Augustine na hatimaye kati ya Mwaka 1996 hadi mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya St. Paul.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi lililowasilisha kwake na Askofu Michael Nnachi Okoro wa Jimbo Katoliki la Abakaliki, lililoko nchini Nigeria la kutaka kung’atuka kutoka madarakani.  Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa sana Padre Peter Nworie Chukwu, ambaye hadi kuteuliwa kwake, alikuwa ni Paroko wa Parokia ya St. Patrick iliyoko Nduruku-Amagu na pia alikuwa anafundisha Chuo Kikuu cha Ebonyi, huko Abakaliki, Nigeria na Padre wa maisha ya kiroho kwa wanovisi wa Shirika la Yesu Kristo Mchungaji mwema. Itakumbukwa kwamba, Askofu mteule Peter Nworie Chukwu alizaliwa tarehe 5 Novemba 1965, Jimboni Abakaliki.

Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 13 Julai 1993 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tangu wakati huo kama Padre, ameweza kuwatumikia watu wa Mungu Jimboni Abakaliki kama: Paroko-usu, Gambera Msaidizi wa Seminari St. Augustine na hatimaye kati ya Mwaka 1996 hadi mwaka 2000 aliteuliwa kuwa Paroko wa Parokia ya St. Paul huko Uburu. Kati ya mwaka 2002 hadi mwaka 2007 alitumwa nchini Marekani kujiendeleza zaidi kwenye Chuo Kikuu cha “Franciscan University of Steubenville huko Ohio (2000-2001) na baadaye Marquette University, kilichoko Milwaukee kati ya mwaka 2001-2007 na hatimaye kutunukiwa Shahada ya Uzamivu katika Falsafa.

Uteuzi Nigeria
06 July 2021, 15:41