Tafuta

Papa Francisko amemteua Askofu Frank Nubuasah, SVD, wa Jimbo Katoliki la Gaborone kuwa Askofu mkuu "Ad Personam" Papa Francisko amemteua Askofu Frank Nubuasah, SVD, wa Jimbo Katoliki la Gaborone kuwa Askofu mkuu "Ad Personam" 

Askofu Frank A. Nubuasah, Ateuliwa Askofu Mkuu "Ad Personam"

Askofu mkuu Franklyn (Frank) Atese Nubuasah, S.V.D, alizaliwa 1949 huko Likpe Abozome, nchini Ghana. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, tarehe 26 Julai 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 27 Juni 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Vikarieti ya Francistwon nchini Botswana na kuwekwa wakfu, 1998.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu Franklyn (Frank) Atese Nubuasah, S.V.D kuwa Askofu mkuu “Ad personam” wa Jimbo Katoliki la Gaborone nchini Botswana. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Franklyn (Frank) Atese Nubuasah, S.V.D, alizaliwa tarehe 7 Julai 1949 huko Likpe Abozome, nchini Ghana. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi na Kitawa, tarehe 26 Julai 1980 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 27 Juni 1998 akateuliwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Vikarieti ya Francistown nchini Botswana na kuwekwa wakfu tarehe 9 Novemba 1998.

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 9 Agosti 2017 akamteuwa kuwa ni Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Gaborone nchini Botswana. Tarehe 2 Oktoba 2017 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa Askofu wa Francistown. Tarehe 6 Juni 2019 akamwamishia Jimbo Katoliki la Gaborone na hatimaye kusimikwa rasmi tarehe 17 Agosti 2019. Baba Mtakatifu Francisko ilipogota tarehe 5 Julai 2021 akamteuwa kuwa ni Askofu mkuu “Ad personam”, yaani hiki ni cheo ambacho hakiamishiki kwa Askofu mwingine atakayekuja Jimboni Gaborone.

Askofu Ad Personam

 

06 July 2021, 08:10