Tafuta

Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Donimique Tinoudji kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Pala. Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Donimique Tinoudji kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Pala. 

Askofu Dominique Tinoudji Jimbo Katoliki la Pala, Nchini Chad

Askofu mteule Dominique Tinoudji alizaliwa tarehe 8 Agosti 1973 Jimboni Moundou. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 8 Januari 2005 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Moundou. Katika maisha na utume wake kama Padre, amewahi kuwa Paroko-usu. Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2011 alikuwa ni mlezi katika Seminari ya Bakara.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Dominique Tinoudji, wa Jimbo Katoliki la Moundou kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Pala, nchini Chad. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mteule Dominique Tinoudji alikuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya Taalimungu ya “Saint Luc” iliyoko Bakara, Jimbo kuu la N’Djaména. Askofu mteule Dominique Tinoudji alizaliwa tarehe 8 Agosti 1973 Jimboni Moundou. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 8 Januari 2005 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Moundou.

Katika maisha na utume wake kama Padre, amewahi kuwa Paroko-usu. Kati ya mwaka 2008 hadi mwaka 2011 alikuwa ni mlezi katika Seminari ya Bakara. Akajiendeleza kwa masomo ya Sayansi ya Biblia kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2015 na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu katika Taalimungu ya Kibiblia. Kati ya Mwaka 2015 hadi mwaka 2016 alikuwa ni mlezi na jaalimu wa Seminari kuu ya Falsafa ya Sarh. Na tangu mwaka 2016 hadi kuteuliwa kwake amekuwa ni Gambera wa Seminari kuu ya “Saint Luc” huko Bakara, Jimbo kuu la N’Djaména nchini Chad.

Uteuzi Chad
03 July 2021, 14:29