Tafuta

Balozi Adikwu Oga Paul wa Nigeria, tarehe 21 Juni 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko Balozi Adikwu Oga Paul wa Nigeria, tarehe 21 Juni 2021 amewasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francisko 

Balozi Paul Oga Adikwu wa Nigeria Awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi Paul Oga Adikwu alizaliwa tarehe 19 Februari 1958. Ana shahada ya uzamili kutoka Seminari kuu ya St. Augustine iliyoko Job, Nigeria. Baadaye alijiendeleza katika elimu na kujipatia Shahada ya uzamili katika elimu. Kati ya mwaka 1985-1995 alikuwa ni mwalimu. Sekretarieti kuu ya Vatican inamtakia heri, baraka na ufanisi katika majukumu yake kwa ajili ya ustawi wa watu wa Mungu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumatatu tarehe 21 Juni 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Paul Oga Adikwu, Balozi mpya wa Nigeria mjini Vatican. Balozi Paul Oga Adikwu alizaliwa tarehe 19 Februari 1958. Ana shahada ya uzamili kutoka Seminari kuu ya St. Augustine iliyoko Job, Nigeria. Baadaye alijiendeleza katika elimu na kujipatia Shahada ya uzamili katika elimu. Kati ya mwaka 1985 hadi mwaka 1995 alikuwa ni mwalimu.

Kati ya mwaka 2006 hadi mwaka 2010 aliteuliwa kuwa Makamu mkuu wa Shule ya Sekondari ya Aune iliyoko huko Otukpo, Benue State, Nigeria. Kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2013 alikuwa mwalimu wa Shule ya Sekondari Otukpo na hatimaye, kati ya mwaka 2013 hadi mwaka 2018 akateuliwa kuwa ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Otukpo.

Nigeria

 

22 June 2021, 15:03