Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Juni 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Eric Chesnel wa Gabon. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 12 Juni 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Eric Chesnel wa Gabon. 

Balozi Eric Chesnel Toka Gabon Awasilisha Hati za Utambulisho

Balozi Eric Chesnel alizaliwa kunako mwaka 1952. Ni mtaalam wa masuala ya fedha, uchumi sanjari na uendeshaji wa makampuni. Katika maisha na utume wake, amefanya kazi zaidi katika sekta ya mawasiliano ya jamii, masuala ya kijamii, sheria, uchumi na fedha pamoja na mahusiano ya kimataifa. Balozi Eric Chesnel katika masuala ya kisiasa amewahi kuwa ni mshauri maalum wa Rais.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko, Jumamosi tarehe 12 Juni 2021 amepokea hati za utambulisho kutoka kwa Mheshimiwa Bwana Eric Chesnel, Balozi mpya wa Gabon mjini Vatican. Balozi Eric Chesnel alizaliwa kunako mwaka 1952. Ni mtaalam wa masuala ya fedha, uchumi sanjari na uendeshaji wa makampuni. Katika maisha na utume wake, amefanya kazi zaidi katika sekta ya mawasiliano ya jamii, masuala ya kijamii, sheria, uchumi na fedha pamoja na mahusiano ya kimataifa.

Balozi Eric Chesnel katika masuala ya kisiasa amewahi kuwa ni mshauri maalum wa Rais kunako mwaka 2014. Amewahi kuwa Katibu mkuu mwambata wa Rais kati ya mwaka 2011 hadi mwaka 2014. Amewahi pia kuteuliwa kuwa ni Mshauri binafsi wa Rais Omar Bongo Ondimba wa Gabon. Aliwahi pia kuwa ni mshauri wa Rais kwenye Ubalozi wa Gabon nchini Ufaransa.

Balozi Gabon
12 June 2021, 14:20