Tafuta

Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler ang'atuka kutoka madarakani. Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler ang'atuka kutoka madarakani. 

Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler Ang'atuka Madarakani Monrovia

Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler alizaliwa tarehe 4 Januari 1944 huko Harrisburg, Liberia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 22 Desemba 1974 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 30 Mei 2002 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Gbarnga nchini Liberia na kuwekwa wakfu 9 Novemba 2002. Ameng'atuka 7 Juni 2021

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameridhia ombi la kutaka kung’atuka kutoka madarakani lililowasilishwa na Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler wa Jimbo kuu la Monrovia, nchini Liberia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Lewis Jerome Zeigler alizaliwa tarehe 4 Januari 1944 huko Harrisburg, Liberia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 22 Desemba 1974 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre. Tarehe 30 Mei 2002 Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Gbarnga nchini Liberia na kuwekwa wakfu tarehe 9 Novemba 2002.

Tarehe 11 Julai 2009, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Askofu mwandamizi wa Jimbo kuu la Monrovia. Tarehe 12 Februari 2011 akasimikwa rasmi kuwa ni mchungaji mkuu wa Jimbo kuu la Monrovia nchini Liberia. Baada ya kuwahumidia watu wa Jimbo nchini Monrovia kama Padre kwa miaka 46 na kama Askofu kwa miaka 18, tarehe 7 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko akaridhia ombi lake la kutaka kung’atuka kutoka madarakani.

Monrovia

 

08 June 2021, 14:39