Tafuta

Papa Francisko amemteua  Askofu mkuu Andrzej Józwowicz kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Iran. Papa Francisko amemteua Askofu mkuu Andrzej Józwowicz kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Iran. 

Askofu mkuu Andrzej Józwowicz Balozi wa Vatican Nchini Iran

Askofu mkuu Andrzej Józwowicz alizaliwa kunako tarehe 14 Januari 1965 huko Boćki, Jimbo kuu la Warsaw nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 24 Mei 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Lowicz, nchini Poland. Papa Francisko mwaka 2017 akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda na Juni 28, 2021 Balozi nchini Iran.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Andrzej Józwowicz, kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Iran. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Andrzej Józwowicz alikuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Andrzej Józwowicz alizaliwa kunako tarehe 14 Januari 1965 huko Boćki, Jimbo kuu la Warsaw nchini Poland. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, kunako tarehe 24 Mei 1990 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre, Jimbo Katoliki Lowicz, nchini Poland. Alijiendeleza kwa masomo na hatimaye akapewa Shahada ya uzamivu katika Sheria za Kanisa.

Taarifa zinaonesha kwamba, alianza utume wa masuala ya kidiplomasia mjini Vatican tarehe 1 Julai 1997 na tangu wakati huo, akatekeleza dhamana na utume wake nchini Msumbiji, Thailand, Hungaria, Syria, Iran na Urussi. Baba Mtakatifu Francisko tarehe 18 Machi 2017 akatemteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Rwanda na kumpandisha hadhi kuwa Askofu mkuu. Akawekwa wakfu na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican tarehe 27 Mei 2017. Ilipogota tarehe 28 Juni 2021, Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Iran.

Uteuzi Irani
29 June 2021, 15:10