Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu  Adolfo Tito Camacho Yllana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Cyprus na Mwakilishi wa Kitume Yerusalemu na Palestina. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Cyprus na Mwakilishi wa Kitume Yerusalemu na Palestina. 

Askofu mkuu Adolfo Tito: Balozi wa Vatican Israeli na Cyprus!

Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana ameteuliwa na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Cyprus. Atakuwa pia Mwakilishi wa Kitume mjini Yerusalemu na Palestina. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Australia. Alizaliwa Mwaka 1948. Daraja Takatifu ya Upadre 1972 na Uaskofu, 2002!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteuwa Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Cyprus. Atakuwa pia Mwakilishi wa Kitume mjini Yerusalemu na Palestina. Kabla ya uteuzi huu, Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana alikuwa ni Balozi wa Vatican nchini Australia. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana alizaliwa tarehe 6 Februari 1948 huko mjini Naga, Jimbo la Caceres nchini Ufilippin. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 19 Machi 1972 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre.

Baadaye aliendelea na masomo ya juu na kujipatia Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran kilichoko mjini Roma na hatimaye akajiunga na Chuo cha Diplomasia ya Kanisa mjini Roma. Tangu wakati huo, ametumwa kutekeleza shughuli mbalimbali za kidiplomasia nchini Ghana, Sri Lanka, Uturuki, Lebanon, Hungaria na Taiwan. Tarehe 13 Desemba 2001, Mtakatifu Yohane Paulo II akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea na kumpandisha hadhi kuwa ni Askofu mkuu. Tarehe 6 Januari,2002 Sherehe ya Tokeo la Bwana, Mtakatifu Yohane Paulo II, akamwekwa wakfu kuwa Askofu mkuu, katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Tarehe 5 Februari 2002 akaongezewa tena Kituo cha kazi kwa kuteuliwa kuwa ni Balozi wa Vatican kwenye Visiwa vya Solomon. Tarehe 31 Machi 2006, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Pakistan. Tarehe 20 Novemba 2010, tena Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini DRC. Na tangu tarehe 17 Februari 2015, Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa kuwa ni Balozi wa Vatican nchini Australia. Na ilipogota tarehe 3 Mei 2021 Baba Mtakatifu Francisko akamteuwa Askofu mkuu Adolfo Tito Camacho Yllana kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Israeli na Cyprus. Atakuwa pia mwakilishi wa kitume mjini Yerusalemu na Palestina.

Uteuzi Vatican

 

 

03 June 2021, 15:42