Tafuta

2021.05.18 Chakula kwa ajili ya Maisha.Jukumu la wanawake katika kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu 2021.05.18 Chakula kwa ajili ya Maisha.Jukumu la wanawake katika kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu  

Wanawake ni wakala wa mabadiliko katika usalama wa chakula

Umeanza mkutano wa kwanza katika mfulilizo wa mikutano 3 kwa njia ya mtandao inayoangaziwa na Laudato si’ katika Wiki iliyoanza tangu tarehe 16 Mei.B.Martinelli amesema uhusiano wa wanawake ni kitovu cha ujumuishwaji na utamaduni wa utunzaji.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Mchana tarehe 17 Mei 2021 umefanyika mkutano wa kwanza kati ya mitatu iliyozinduliwa katika na Katibu wa Vatican, Utume wa Kudumu wa Vatican katika Makao ya mashirika ya Kimataifa FAO, IFAD na  PAM, Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamu na Tume ya Vatican kwa ajili ya COVID-19 pamoja na washirika ambao wanafanya kazi katika uwanja huo wa usalama wa vyakula.  Mkutano huo ni katika fursa ya mwanga wa maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mifumo ya Vyakula 2021. Sauti ya wanawake katika mazungumzo kutoka sehemu mbalimbali za dunia wametajirisha mkutano juu ya jukumu la wanawake katika kuhamasisha maendeleo fungamani kwa namna ya pekee umakini wa jinsi ya kusaidia uongozi wao ili kuimarisha mifumo ya vyakula ulimwengu mzima. Waliokaribisha jukwaa hili ni Roma kwa kupewa jina la “Chakula kwa ajili ya maisha: Jukumu la wanawake katika kuhamasisha maendeleo fungamani ya binadamu.

Katika mfulilizo wa mikutano hiyo ambao umeanza katika Wiki ya Laudato si, kuanzia tarehe 16-24 Mei, kwa hakika unaongozwa na Waraka wa Papa Francisko. Mikutano hii inataka kuonesha jinsi ambavyo Ekolojia Fungamani, inafanana na kile ambacho kinafikiriwa kuunganisha kwa pamoja kati ya mambo mengi ya watu, kati ya mifumo ya kijamii na kiuchumi kijamii  na inaweza kweli kuungizwa na kuzaliwa mifumo mipya ya vyakula katika wakati ujao baada ya COVID.  Mikutano inataka kubainisha jinsi ambavyo Kanisa na washirika wengine wanaweza kweli kuchangia katika mabadiliko ya mifumo ya chakula kuelekea utunzaji bora wa nyumba yetu ya pamoja na kuondoa kabisa njaa, kulinda na hadhi ya kibinadamu na huduma ya wema wa pamoja kwa namna ya kwamba hakuna yoyote anabaki nyuma

Aliyeudhuria mchana kutano huo tarehe 17  Mei kwa njia ya mtandao pia ni Chiara Martinelli, mratibu msaidizi wa Kikundi kazi cha Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19: na ambaye amethibitisha kwamba Vatican na wakala wengine wa Kanisa wanataka kutoa mchango wao katika mchakato wa kuelekea Mkutano Mkuu huo wa Umoja wa Mataifa (UN) na kwamba ulio na maono ya ekolojia fungamani ambayo Papa Francisko alituwakilishia kwenye Watraka wake wa Laudato si. Vile vile Bi Martinelli amesema wamefanya uzoefu kama Tume ya Vatican kwa ajili ya Covid-19 wakati wa mwaka huu wa mwisho na kwamba ni ufunguo wa kukabiliana na changamoto za ulimwengu kwa namna ya mifumo na siyo kisekta. Haitakiwi kutazama ukosefu wa haki ya vyakula tu kama matatizo ya ukosefu wa chakula ambao kwa hakika lazima kukabiliana nalo lakini jinsi gani tatizo hili linatokana ukosefu wa usawa

Ni lazima kukabiliana na ukosefu wa usawa kwa njia ya hatua za mifumo ya vyakula. Kwa maana hiyo ni kuanzia na uzalishaji hadi kufikia ulaji, kuanzia ugawaji hadi kufikia uendeshaji wa wanaobaguliwa. Ni maono ya nyuzi 360 ambao amesema unawasaidia kutoa mchango kwa mambo yale ambayo ni muhimu ili kuweza  kuwa na mfumo wa vyakula kutoka shambani hadi kufikia kwenye sahani na kwamba uwe na umakini wa kujibu ukosefu wa chakula kwa baadhi ya sehemu za waathirika wa sayari  hii , lakini pia hata mifumo ya vyakula iliyopo, yenye uwezo wa kuzoea mabadiliko ya tabianchi, ambayo yanazui na kuleta athari za kupasha joto ulimwengu na kuhakikisha ufikiaji wa vyakula kwa wote.

18 May 2021, 16:03