Tafuta

Vatican News
2019.11.21 Guarasci waandishi wakisubiri tukio 2019.11.21 Guarasci waandishi wakisubiri tukio 

Vatican:Urbańczyk:uhuru wa vyombo vya habari ni msingi wa kuhamasisha demokrasia na haki

Jumuiya za kidini zimealikwa kujieleza maono yao na kuchangia katika mijadala ya kijamii juu ya masuala ya sasa,kwa namna ya kuhakaikisha kwa kiasi kikubwa utajiri katika kutoa matarajio mbadala ya kimaadili.Amesema hayo Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Baraza la OSCE.Ni katika kikao kuhusu uhuru wa vyombo vya habari.Habari na vyombo vya habari ni zana kwa kupitisha habari ya uwazi na halisi

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 13 Mei  2021, Monsinyo Janusz Urbańczyk, Mwakilishi wa Kudumu kwa wa Vatican katika Ofisi ya Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE), lenye makao yake Vienna Uswiss, akizungumza katika kikacho cha 1313 cha Baraza la Kudumu la shirika lenyewe, kuhusu uhuru wa vyombo vya habari amesema “Habari na vyombo vya habari ni zana muhimu kwa upitishaji wa habari ya uwazi na halisi na kwa maana hiyo  uhuru wao ni sehemu muhimu ya kuhamasisha maadili ya kidemokrasia na jamii za haki zaidi. Kuanzia ukweli halisi, ambao kwa hakika unaleta wasiwasi wa matukio ambayo yanaathiri vibaya uhuru wa waandishi wa habari na kazi yao muhimu katika eneo lote la OSCE, ndilo mwakilishi wa Vatican amekumbusha kuhusu haki ya watu ya kutafuta, kupokea na kusambaza habari na maoni, hata linapokuja suala la masuala ya kidini na maadili.

Kwa bahati mbaya ameongeza kuseama “Leo hii suala hili si rahisi, zaidi imerekodiwa kesi zenye kutia wasiwasi mahali ambapo wakristo, wayahudi, waislamu na wajumbe wa madhehebu mengine wanashukiwa wako hatarini na kuogopeshwa kujieleza adharani mawazo yao, yenye msingi wa imani yao. Na hii inawazuia kuwa sehemu ya jamii”. Sio hivyo tu: kiongozi huyo amesisitiza kwamba “uvumilivu huu unapitia mashtaka ya kufanya matamshi ya chuki, ambayo ni sawa na kulinganisha imani ya kidini na chuki na hivyo kuonesha dini kama shida”. Kinyume chake, amesisitiza kwamba vyombo vya habari vinapaswa kutoa maoni ya kwa mapana pamoja na mtazamo wa dini tofauti, ili kuhimiza, kubadilishana kwa mawazo na maoni ndani ya jamii.

Katika mtazamo huo Mwakilishi wa Kudumu, amelishauri OSCE kujitahidi kuzingatia maslahi ya jumuiya ya kidini ili kushiriki mazungumzo ya umma hata kwa njia ya vyombo vya habari, kwa kuwatia moyo, katika hujumuishwaji wa mijadala ya kunzisha sheria. Na wakati huo huo, Jumuiya za kidini zimealikwa na mwakilishi huyo kujieleza maono yao na kuchangia katika mijadala ya kijamii juu ya masuala ya sasa, kwa namana ya kuhakaikisha kwa kiasi kikubwa utajiri katika kutoa matarajio mbadala ya kimaadili.

Wito mkuu Mwakilishi, wa Vatican kwa  wahusika wote ni Uhuru wa kujeieleza, kama kila ya haki ya binadamu, inayo sindikizwa na uwajibikaji ambao haiwezi kweli kudharauliwa hasa mbele ya watoto, ambao daima lazima walindwe. Maadili ya mawasiliano kwa hakika yanakuwa kiini cha mtu na jumuiya ya binadamu, hasa maendelei yao fungamani. Kutokana na hilo, Mwakilishi wa kudumu, ametoa wito pia wa kuwa makini sana katika mitandao ya kijamii na Internet, kwa namna ya kuzuia na kufanya mang’amuzi na uwajibikaji wa kudanganywa kwa habari, kuenezwa kwa habari mbaya na kuenea kwa habari bandia “fake news”. Hatimaye mwakilishi wa kudumu amesisitiza umuhimu wa kuhamasisha fursa za kwa wanawake ambao wanafanya kazi katika sekta ya mawasiliano, pamoja na  kulinda haki ya kila mwandishi hasa  ikwa ni suala la kike, dhidi ya kila aina ya vurugu na kuhamasisha amani na usalama kwa ujumla wake kwa wote.

15 May 2021, 13:59