Tafuta

Vatican News
2021.04.27 Mahakama ya Vatican 2021.04.27 Mahakama ya Vatican  

Uteuzi wa Rais wa Mahakama ya Rufaa ya Serikali ya Jiji la Vatican

Monsinyo Alejandro Arellano Cedillo ndiye Rais wa Mahakama ya Rufaa ya Serikali ya Jiji la Vatican.Alipata daja la ukuhani 1987 na mwanashirika la Wakuhani wafanyakazi wa Ufalme wa Kristo na ambaye Papa alikuwa amemteua Machi iliyopita kuwa Dekano wa Mahakama ya Rota Romana.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Papa Francisko, Jumamosi tarehe 8 Mei 2021 amemteua Rais wa Mahakama ya Rufaa ya Serikali ya Jiji la Vatican Monsinyo Alejandro Arellano Cedillo, Dekano wa Mahakama ya Kitume ya Kanisa Katoliki, ijulikanayo kwa jina la Rota Romana. Monsinyo Alejandro Arellano Cedillo alizaliwa manamo tarehe 8 Juni 1962 huko Olías del Rey (Uhispania). Alipewa daraja la ukuhani tarehe 25 Oktoba 1987 huko Toledo katika Shirika la Makuhani wa Wafanyakazi wa Ufalme wa Kristo na akafuatia  masomo na kupata shahada na Udaktari wa Sheria, katika Chuo Kikuu cha Gregoriana Roma.

Alikuwa msaidizi wa makamu wa mahakama katika Jimbo kuu la Madrid na hakimu katika Mahakama ya Rota ya Ubalozi wa Kitume nchini Uhispania. Yeye ni profesa wa Sheria ya Canoni na Sheria. Tangu 2007 amekuwa mkaguzi mkuu wa Mahakama ya Kitume ya Kanisa Katoliki au Rota Romana.

Vile vile ni mjumbe wa Tume Maalum ya sababu za kubatirisha ndoa iliyoridhiwa na isiyokamilika na pia kuhusu masuala ya kuondolewa majukumu ya ushemasi na ule wa ukleri. Mnamo tarehe 30 Machi Papa alikuwa amemteua kuwa dekano wa Mahakama ya Kitume ya Kanisa Katoliki, au kwa jina Rota Romana.

08 May 2021, 13:52