Tafuta

Vatican News
Msalaba wa Siku ya vijana Msalaba wa Siku ya vijana 

Siku ya vijana kijimbo:hija na udugu kibinadamu

Baraza la Kipapa kwa ajili ya walei familia na maisha wamewakilisha tarehe 18 Mei 2021 Hati ya maelekezo ya kichungaji kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya vijana ulimwenguni katika Makanisa mahalia ambayo itaadhimishwa kijimbo katika siku kuu ya Kristo mfalme.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Maelekezo ambayo yanawakilisha sababu za mawazo na uwezekano wa matendo ya dhati ili Siku ya vijana kijimbi/ paroka viweze kuwa fursa ya kuonekana nguvu ya wema, ukarimu, kiu ya thamani za dhati, na mawazo makuu ambayo kila kiajana anapeleka ndani mwake. Ndiyo lengo la Maelekezo ya kicungaji kwa ajili ya maadhmish ya siku ya Vijana katika makanisa maalumu na ambapo Hati ya baraza la Kipapa kwa ajili ya walei familia na maisha wamewakilisha tarehe 18 mei 2021 kwa waandishi wa habari wa vatican.

Mwaliko kwa majimbo yote ni ule wa kuadhimisha siku ya vijana ulimwenguni kujimbo katika siku kukuu ya Kristo Mfalme. Kwa hakika ni shauku ya Baba Mtakatifu ambaye siku hiyo Kanisa la ulimwengu linaweka vijana katikati kwa ajili ya umakini wa kichugaji, kusali kwa ajili yao, kutimiza ishara ambazo zinawafanya vijana wawe mstari wa mbele na kuhamasisha kampeni za mawasiliano. Kama inavyojulikana kwa hakika wakati wa maadhimisho ya kimataifa ya tukio, kwa kawaida wanazingatia miaka mitatu katika nchi ambayo inakuwa imechaguliwa na ambapo kuna hata ushiriki wa Papa, wakati maadhimisho ya kawaida ya siku ya vijana kijimbo inafanyika kila mwaka katika makanisa mahalia, na ambapo wao hufanya maandalizi kwa kujitegemea katika tukio hilo.

Hili ni tukio kubwa na lenye maana na thamani kiroho, si  kwa vijana tu ambao wanaishi katika mwelekeo na sababu hizo,   lakini pia hata jumuiya nzima ya makanisa mahalia, kama inavyoeleza hati hiy ambayo inawelekeza mabaraza yamaaskofu, Sinodo za makanisa ya kipatriaki, na maaskofu wakuu, majimbo yote na matriaki yote. Vyama vya kichungaji ambavyo vinakusudia kutia moyo makanisa mahalia kutamanisha daima maadhimisho ya siku ya vijana kijimbo na kuendelea na safari katika fursa ya kupanaga na kutumiza kwa ubinfua wa kuanzisha mkakati mmoja ambao Kanisa linafikia utume waka na vijana kwa kutoa kiapimbele cha kichungaji jinsi ya kuwekeza wakati, nguvu na rasilimali.

Hati hiyo baadaye inaonesha ishara msingi za siku ya vijana (WYD) ili hafla hiyo iweze kuwa siku kuu  ya imani, uzoefu wa Kanisa na wakati huo huo ya kimisionari, fursa ya utambuzi wa mang’amuzi na wito wa utakatifu. Kwa kuongezea, Siku ya Vijana lazima iwe uzoefu wa hija na udugu wa ulimwengu. Hakika, sherehe ya siku ya vijana (WYD) inawapa vijana uzoefu wa kusisimua, wa kufurahisha wa imani na ushirikiano, na nafasi ya kuona uzuri wa uso wa Bwana. Miongozo inaangazia, na kusisitiza kwamba ni muhimu sherehe hiyo iwe tukio ambalo watu wanaweza kupata ushirikiano wa kikanisa na kukua katika ufahamu wa kuwa sehemu muhimu ya Kanisa. Yote hayo kwa ikizingatia kwamba mtindo wa kwanza ya kuwashirikisha vijana lazima we wa kusikiliza

Kwa mujibu wa maandishi yanatbibitisha kuwa , Majimbo yote na   mapartiaki  katika siku ya vijana  (WYD) inaweza kuwa fursa nzuri ya kuoneesha utajiri wa Kanisa mahalia, na kuzuia vijana ambao mara nyingi hawapo na wala  hawana bidii kuingia katika miundo ya kichungaji iliyojumuishwa tayari ili wasijisikie kutengwa. Kila mtu lazima ahisi kualikuwa kuwa wageni maalum; kila mtu lazima ahisi anatarajiwa na kupendwa sana, katika upekee wake usioweza kurudiwa na utajiri wa kibinadamu na kiroho. Tukio hilo la kijimbo  kwa maana hiyo  linaweza kuwa fursa nzuri ya kuchochea na kuwakaribisha vijana wale wote ambao labda wanatafuta nafasi yao Kanisani na ambao bado hawajapata . Hati hiyo inahitimisha kwa kuoneesha kwamba bila shaka sikukuu ya kijimbo ya siku ya vijana ni hatua muhimu katika maisha ya kila Kanisa, wakati mzuri wa kukutana na vizazi vya vijana, chombo cha uinjilishaji wa ulimwengu wa vijana na wa mazungumzo nao.

18 May 2021, 15:27