Tafuta

2021.01.09 Papa mbele ya picha ya  Pauline Jaricot 2021.01.09 Papa mbele ya picha ya Pauline Jaricot 

PMS yazindua maadhimisho ya miaka 200

Shirika la Kipapa la matendo ya Kimisionari (PMS) limeanza maandalizi ya maadhimisho ya miaka 200 tangu kuanzishwa kwake yatakayofikia kilele chake mnamo tarehe 3 May 2022.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Tarehe 3 Mei 2022 itakuwa ni siku muhimu katika historia ya Shirika la Kipapa la matendo ya Kimisionari (PMS) kwa maana mwaka kesho inatimiza miaka 200  tangu kuanzishwa kwake  rasmi kwanza kama Chama cha kukuza Imani ” na miaka 100 tangu Kuchapishwa kwa Motu Proprio ya Romanorum Pontificum ambayo Papa Pio XI alikuwa anathibitisha chama hiki kama Shirika la Kipapa la matendo ya Kimisionari (PMS) kwa ajili ya kukuza imani. Kuanzia Jumatatu tarehe 3 Mei, Shirika la Kipapa la Maedno ya Kimisionari (PMS)limeanza maandalizi ya sherehe hizo za 2022, kwa kutazama kwa kina vyanzo vya karama ya mwanzilishi wake ambaye ni mlei, Pauline Jaricot.

Pauline alizaliwa huko Lione nchini Ufaransa, tarehe 22 Julai 1799, baada ya kupitia wakati mgumu wa ujana wake kwa sababu ya kuanguka na kumsababisha madhara makubwa ya kimwili, mwanamke huyo alihisi ndani mwake wito wa kimisionari. Tarehe 3 Mei 1822 pamoja na kikundi cha wanawake, walinzisha chama cha kukuza imani, na ambacho baadaye kikaridhiwa na Papa Pio VII mnamo 1823. Pauline alijikita kwa dhati kuhudumia maskini na wagonjwa, akiwatembelea kila siku katika Hospitali na watu wenye magonjwa yasiyo tibika.

Msaada kwa walio na mahitjii ulikuwa umesindikizwa kwa maisha ya sala ya kina. Kila siku alipokea Ekaristi, alikuwa akiwaombea uongofu wa wadhambi na uinjilishaji ulimwenguni. Mauti yalimjia akiwa maskini huko Lione mnamo tarehe 9 Januari 1862. Mnamo tarehe 25 Februari 1963 alitangazwa kuwa Mtumishi wa Mungu na Mtakatifu Yohane XXIII. Tarehe 26 Mei 2020 Papa Francisco alilirhdia mchakato wa kutangazwa Mwenyeheri, kufuatia na muujiza kwa njia ya maombezi yake.

Shirika la Kipapa la matendo ya Kimisionari PMS lipo katika nchi 130 Ulimwengu ambalo linahesabu wamisionari 354,000, makatekista milioni 3 na majimbo 114 katika maeneo ya kimisionari. Milioni 150 za dola ambazo zinahudumia mipango ya kichungaji na kijamii.  Yote hayo kwa lengo la kusaida Papa katika jitihada zake na Makanisa yote mahali iwe kwa sala na ambayo inauisha utume, iwe msaada wa nyenzo kwa ajili ya wakristo ulimwenguni kote. Ikumbukwe mnamo 2020, mwaka ambao unaliibuka janga la virusi vya corona au Covid-19. Papa Fracisko alianzisha ndani ya PMS mfuko wa dharura kwa ajili ya mataisa ya kimisionari ambayo yamekumbwa zaidi na virusi vya corona, na hundi ya kuanzia $ 750,000. Papa mwenyewe, katika ujumbe wake mnamo Mei mwaka jana, alimkumbusha PMS Utume ni zawadi ya bure ya Roho, na sio matokeo ya mikakati, na kwamba kuwa mmisionari ni onesho la shukrani kwa kile kilichopokelewa

05 May 2021, 16:56