Tafuta

Vatican News
2021.05.02 Askofu Mkuu.Edgar Pena Parra 2021.05.02 Askofu Mkuu.Edgar Pena Parra 

Peña Parra:Mwenyeheri Hernández,alishuhuhudia Yesu na matendo ya maisha

Askofu Mkuu Edgar Peña Parra,Naibu katibu wa Vatican ameadhimisha Misa Roma kwa ajili ya kushukuru kutangazwa mwenyeheri José Gregorio Hernández Cisneros,aliyekuwa daktari na baadaye kuwa mmisionari.Papa Francisko amemkumbuka mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Naibu katibu wa Vatican wa Mambo ya ndani ya Vatican askofu Mkuu Edgar Peña Parra ameongoza misa ya kutoa shukrani kwa ajili ya kutangazwa mwenye heri Gregorio Hernández Cisneros, Ijumaa tarehe 30 Aprili 2021  aliyekuwa ni daktari na akawa mmisionari huko Caracas, nchini  Venezuela. Katika misa iliyofanyika mchana tarehe 2 Mei 2021, katika Parokia ya Mtakatifu Maria wa Milima jijini Roma, kwa kushiriki jumuiya nzima ya Wavenezuela wanaoishi jijini Roma, Askofu Mkuu amesema  Mwenyeheri alikuwa ni kaka wa maskini na shuhuda wa Yesu kwa sababu hakuwa na maneno bali ni matendo ya maisha.

Akitazama hali halisi ya sasa amesema ni kwa jinsi gani sura ya mwenyeheri mpya ilivyo muhimu katikati ya janga ambalo linawaweka wote katika majaribu na hatari ya kujifikiria binafsi. Lakini pia ni kwa jinsi gani faraja inaletwa na huyo kaka ambaye anaomba akiwa mbinguni, kwa  wakati huu ambapo wengi wako katibu peke yao, wanaogopa na kwa maana hiyo katika yeye upo uwezekano wa kupata rafiki karibu kama alivyoweza kutunza na kusaidia afya ya watu wake, kwa maana alikuwa anapenda watu na aliwapenda kwa sababu alikuwa anampeda Mungu sana.

Askofu Mkuu pia amesisitizia juu ya maneno yaliyosikika kwenye Injili hasa neno la kubaki, ambalo lilionekana mara saba katika Injili ya siku. Kwa mujibu wake amesema ni neno la ushikishano wa maisha kwa maana, ili kuwa mfuasi wa Yesu haitoshi kumjua na kunfuata na kumuiga, lakini ni lazima kudumisha ule uhusiano binafsi na Yeye, kwani Yesu si mtu tu wa kuigwa lakini ni mtu wa kupendwa. Na ni kwa njia hiyo Mwenyeheri Hernández, alionesha hivyo kwa kushiriki misa za kila siku, alikuwa akiweka yote aliyokuwa akifanya, matatizo ambayo yalikuwa moyoni mwake mbele ya altare na kupata faraja na amani ya moyo.

Neno la Mzabibu alilifananisha na muungano hai kati ya Yesu na sisi ambao ni matawi na ambayo daima lazima yapunguzwe. Sisi tuna njaa na kiu ya kuwa na mambo mengi ya kuongeza, lakini Baba wa mbinguni anatamani kwetu tuwe watu rahisi, amesisitiza Askofu Mkuu. Kama mzababu ambavyo hauwezi kutoa matunda yake bila kupunguzwa matawi yake, ndivyo hata maisha bila kutakasika hayawezi kuwa bora. Huwezi kujikamilisha kwa kukusanya na kujirundikia fedha na umaarufu bila kutoa zawadi kwa wahitaji.

Ni lazima kupukutwa ndani mwetu ili Bwana aweze kujaa na na ndiyo maisha ya kiroho, amesisitiza Askofu Mkuu. Kupukutwa hata hivyo hakukukosekana katika maisha ya mwenye heri mpya, lakini alitambua kukabiliana na kukitia , udhaifu na magonjwa. Hakukata tamaa Gregorio Hernández , bali alichagua Injili, alichagua kujikana mwenyewe na kuwasaidia maskini na kujazwa na utajiri mwema. Askofu Mkuu Peña Parra ameshauru kuwa na utambuzi huo wa maisha makamilifu ambayo yanajikita kutoa kwa upendo wa dhati na huo kugeuka kuwa huduma ya kweli kwa wote.

Neno la tatu ambao Askofu Mkuu amesisitiza, ni lile ambalo Yesu anasema 'kweli', akiunganisha na maisha. Katika lugha ya kibiblia, linaelekeza uaminifu, kukubalika bila, kama vile Mungu ambaye anabaki kidete na wala hakatishi tamaa kwa ahadi zake. Kwa sababu kila kitu tunacho mkabidhi kwenye mikono yake, hakipotei. Juhudi zetu hata zile ndogo peke yetu hazitoshi. Zinakuwa hai na thabiti pale tu tunapomkabidhi kwake yote Bwana. Alikuwa anasema Mwenyeheri Hernández kwamba Ikiwa ulimwenguni wapo walio wema na wakatili, lakini walio wema wapo kwa sababu ya Msaada wa Mungu na huo ndiyo ukuu wa neema kwa sababu Mungu ambaye anabaki milele ni upendo, na ka sababu upendo hauna mwisho”. Amehitimisha

Sherehe za kutangazwa mwenyeheri mpya, zimeongozwa na Askofu Mkuu Aldo Giordano, Balozi wa kitume nchini Venezuela na katika fursa hiyo, Papa Francisko ametuma ujumbe kwa njia ya video ambapo anawatakia matashi mema ya nchi kuwa na roho ya mapatano. Vile vile mara baada ya sala ya Malkia wa mbingu, Dominika tarehe 2 Mei Papa amekumbuka mwenye heri mpya alivyotambua uso wa Kristo kupitia wagonjwa.

03 May 2021, 16:56