Tafuta

Vatican News
2019.10.07Sinodi ya Maaskofu  2019.10.07Sinodi ya Maaskofu   (Vatican Media)

Papa Francisko:Mapya ya Sinodi inaanzia katika makanisa mahalia

Mwezi Oktoba unaanza mchakato wa maandalizi ya Sinodi ya miaka mitatu kwa utashi wa Papa ambapo unajikita katika hatua tatu:kijimbo,kibara na ulimwengu utakaofanyika kuanzia na ushauri na mang’amuzi na utahitimishwa na Sinodi ya Oktoba 2023 Roma.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

 “Mmoja katika kusikiliza wengine; na wote katika kusikiliza Roho Mtakatifu”. Ili kuweza kuona Sinodi ya kweli, ambayo imependekezwa na Papa Francisko, tangu mwanzo wake wa upapa, Sinodi ijayo ya Maaskofu inayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2023, haitafanyika jijini Vatican tu, bali kwa kila Kanisa mahalia katika mabara matano, kwa kufuata hatua ya michakato ya miaka mitatu ambayo ina hatua zke taztu za kijimbo, kibara na ulimwenguni.

Mchakato fungamani wa kisinodi.

Mchakato wa hatua ya kisinodi ulioridhiwa na Papa, umepachapishwa  katika Hati ya Katibu mkuu wa Sinodi ambao unasomeka kwamba: “mchakato wa sinodi fungamani, utatimizwa kwa namna ya dhati katika Maknisa mahali ambazo unaweza kutimizwa ikiwa tu unashirikisha hata mabaraza ya ndani ya kisinodi, yaani Sinodi ya Makanisa ya mashiriki katoliki, Mabaraza na Mikutano ya makanisa  kuhusu sheria na Mabaraza ya maaskofu katika vielelzo  vyao vya kitaifa, kikanda na kibara.

Kwa mara ya kwanza sinodi inakuwa mchanganyiko

Ni mara ya kwanza katika historia ya taasisi hii iliyoanzishwa na Papa Paulo VI kuendeleza na uzoefu wa Ushauri wa Mtaguso wa Pili la Vatican kwamba Sinodi ya ugawanyaji iadhimishwe. Hii hasa inamaanisha   na kukumbusha katika sherehe ya kumbukumbu ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Sinodi, mnamo Oktoba 2015, ambapo Baba Mtakatifu Francisko alikuwa ameelezea shauku yake ya kufanya safari ya pamoja ya watu wa Mungu walei, wachungaji na Askofu wa Roma.

Ufunguzi wa maadhimisho na Papa jijini Vatican

Safari ya kisinodi itafunguliwa jijini Vatican kwa uwepo wa Papa Franciko mnamo tarehe 9 na 10 Oktoba 2021 kwa kuwa na mkutano na tafakari baada kuanza na misa ya takatifu ya ufunguzi.

Hatua za kijimbo:ushauriano na ushiriki wa Watu wa Mungu

Makanisa mahalia yaataanza mchakato wa safari  ya kisinodi mnamo  Dominika tarehe 17 Oktoba 2021 chini ya uongozi wa Askofu wa jimbo. Lengo la hatua hii ni kufanya mashauriano ya Watu wa Mungu na kwa maana hiyo Katibu Mkuu wa Sinodi atatuma Hati ya maandalizi ikifuatana na maswali dodoso pamoja na mapendekezo ili kutimiza mashauriano ya kila Kanisa mahalia. Hati yenyewe itatumwa katika Mabaraza yote, katika Umoja wa wakuu wa mashirika, umoja wa  mashirika ya kitawa makuu, harakati za walei katoliki kimataifa, Vyuo Vikuu  katoliki au vitivo vya kitaalimungu.

Kila Askofu kabla ya mwezi Oktoba 2021 atachagua mhusika kijimbo ambaye atahusika na kuwasiliana na Baraza la maaskofu, na  ambaye kwa mara nyingine atachagua mhusika au kikundi kingine cha kuweza kuwasiliana na Katibu Mkuu wa Sinodi. Mang’amuzi ya kijimbo yatahitimishwa na Mkutano kabla ya Sinodi. Mchango huo utatumwa katika Baraza lenyewe la Maaskofu. Maaskofu watakaounganika katika Mkutano kwa kipindi cha kufanya mang’amuzi, wataandaa ufupisho wa kutuma kwa Katibu Mkuu wa Sinodi. Yote hayo yatafanyika kabla ya mwezi Aprili 2022. Baada ya kupata nyenzo, kwa maana hiyo itakuwa Muhtasari muhimu katika mchakato ambao utakuwa wa kwanza wa Instrumentum Laboris, yaani Hati ya kutendea kazi ambayo mwezi Septemba 2022 itachapishwa na kutumwa katika Makanisa mahalia.

Hatua ya pili ya mabara:mazungumzo na mang’amuzi

Hatua ya pili ni ile ya kibara ambayo inatazamiwa kuanza mwezi Septemba 2022 hadi Machi 2023. Lengo lake ni kuzungumzia juu ya Instrumentum laboris,  yaani Hati ya kutendea kazi. Hatimaye itaaririwa Hati ya mwisho ya kutuma mwezi Machi 2023 kwa Katibu Mkuu wa Sinodi ambaye ataendelea na utayarishaji wa Instrumentum Laboris ya Pili yaani hati ya Pili ya kutendea kazi. Uchapishwaji wake unatarajiwa mwezi Juni 2023.

Hatua ya tatu ni ulimwengu:Maaskofu wa ulimwengu jijini Roma

Safari ya Sinodi, inatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2023 katika maadhimisho ya sinodi ya  Maaskofu jijini Roma, kulingana na taratibu zilizowekwa katika katiba Episcopalis Communio, yaani ya katiba ya mkutano wa maaskofu.

21 May 2021, 14:50