Tafuta

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limeunda Kikosi Kazi kushughulikia mchakato wa kupambana na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kikundi cha mafia. Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limeunda Kikosi Kazi kushughulikia mchakato wa kupambana na vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na kikundi cha mafia. 

Mwenyeheri Rosario A. Livatino: Kikosi Kazi Dhidi ya Mafia! Hatari!

Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limeunda kikosi kazi kitakachosaidia kunogesha mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi vya Mafia “Scomunica alle mafie”. Lengo ni kuweza kuwa na upeo mpana kuhusu mchakato huu, kwa kuendelea kushirikiana zaidi na Maaskofu kutoka katika sehemu mbalimbali za dunia, wanaotaka kuunga mkono juhudi hizi.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza waamini kuwa Wenyeheri na Watakatifu, Jumapili tarehe 9 Mei 2021 kwa niaba ya Baba Mtakatifu Francisko amemtangaza Mtumishi wa Mungu Rosario Angelo Livatino kuwa ni Mwenyeheri. Huyu ni Hakimu wa kwanza kujipambanua na hivyo kufungua ukurasa mpya katika historia ya Kanisa. Kama mwamini mlei, amekuwa ni mfano bora wa kuigwa katika kutekeleza dhamana na majukumu yake kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi.

Ni katika muktadha huu, Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu limeunda kikosi kazi kitakachosaidia kunogesha mapambano dhidi ya vikundi vya kigaidi vya Mafia “Scomunica alle mafie”. Lengo ni kuweza kuwa na upeo mpana kuhusu mchakato huu, kwa kuendelea kushirikiana zaidi na Maaskofu kutoka katika sehemu mbalimbali za dunia, watakaokuwa tayari kuunga mkono juhudi hizi. Kikosi kazi hiki kinaundwa na wanasiasa wafuatao kutoka nchini Italia: Vittorio V. Alberti, Rosy Bindi, Luigi Ciotti, Marcello Cozzi, Raffaele Grimaldi, Michele Pennisi, Giuseppe Pignatone, Ioan Alexandru Pop.

Kikosi Kazi
10 May 2021, 15:54