Tafuta

Vatican News
2021.04.28 Mwenyeheri Charles de Foucauld 2021.04.28 Mwenyeheri Charles de Foucauld 

Kard.Semeraro:Ni michakato mirefu kufikia kutangazwa watakatifu

Kardinali Semeraro akikifafanua kuhusu kuridhia wenyeheri saba ili watangazawe watakatifu amesema kuwa wao hawahitaji sisi bali sisi tunawahitaji wao.Hii inathibitishwa kuona watakatifu wengi wametangazwa wa kupitia mchakato wa safari ndefu ya historia ya Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Si watakatifu ambao wanahitaji sisi bali ni sisi ambao hatuweze kufanya bila kuwa na wao.  Na ndiyo maana ya kutangazwa kwa watakatifu wengi ambao wamekuwapo katika mchakato wa safari ya historia ya Kanisa, kama ilivyo hata wenyeheri wapya waliotangazwa na Papa Francisko katika Mkutano wa kawaida wa makardinali uliofanyika tarehe 3 Mei 2021. Amesema hayo Kardinali Marcello Semeraro, Rais wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza wenyeheri na watakatifu akifafanua hali halisi juu ya kazi ya Baraza lake na juu ya sababu ambazo zinawaongoza kufuika chaguzi na michakato ya kutangazwa watakatifu. Amesema hayo kupitia mahojiano na Gazeti la Osservatore Romano.

Akielezea kama kuna jambo muhimu linalo waunganisha watakaotangazwa kuwa watakatifu Kardinali Semeraro amesema kuwa “Watakatifu ni idadi kuu. Na anaimanisha kwamba kila mmoja, anaelezea upekee wake, hata kama njia zinaweza kuonekana sawa. Kimsingi kwa wote daima kuna uzoefu wa upendo wa Kristo, ambao huwasha moyo wao na huchochea chaguzi jasiri. Katika ya watakao tangazwa watakatifu tunapata historia za uongofu kutoka katika  imani nyingine, kama vile shahidi wa India Lazaro, au kutoka kwa kwa aliyekuwa amebobea ulimwengu, kama vile César de Bus na Charles de Foucauld; lakini pia ishara za kuzaa kiroho, kama vile waanzilishi wa familia za watawa, sura halisi za baba na mama katika roho. Watakatifu ambao wameridhiwa katika mkutano wa makardinali na Papa ni wa nyakati tofauti: kutoka karne ya kumi na sita hadi nusu ya pili ya karne ya ishirini, kama ya de Foucauld na Giustino M. Russolillo: wanasukana katika nyakati za huruma na upendo wa Mungu.

Kardinali aidha akielezea ushuhuda na ujumbe ambao unafikia jamii leo hii kuhusu baadhi yao, kama Charles de Foucauld, walioishi Injili katikati ya mazingira ambayo kwa hakika hayakuwa rahisi, amesema “Wale ambao wanatoa huduma katika Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu mara nyingi hugundua kuwa kutangazwa kuwa mtakatifu inafikia hasa wakati sahihi. Katika Waraka wa hivi katibuni wa papa Francisko wa Wote ni Ndugu Papa Francikos alielekeza kwa Charles de Foucauld kama mfano wa ndugu wa ulimwengu wote kati kati ya watu wa jangwa la Afrika (n. 287).  Wakati huo huo, Mungu alitaka mwenyeheri afikie kwa idhini ya muujiza unaohitajika. Mungu anajua jinsi ya kuwaangazi watu wake njia na taa zipi za kutumia. De Foucauld labda ndiye anayejulikana zaidi kati ya wote ulimwenguni lakini hata hivyo, kwa kushangaza, ndiye yule ambaye alitafuta kujificha katika fumbo la Nazareti. Karibu inaonekana kuwa inalingana na agizo la Yesu: “Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya paa la nyumba” (Mathayo 10:27).

Hakukosa kufafanua juu ya nafasi ya waliowekwa wakfu hasa kati ya hawa kuna waanzilishi wa mashirika ya kike na kiume, ambapo Kardinali Semeraro amesema kwamba hakika wenye heri watano ni waanzilishi wa familia za kitawa.  Na katika Wosia Kitume wa Maisha ya Kiitawa wa (1996), Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika kwamba "jambo ambalo ni la mara kwa mara katika historia ya Kanisa limetolewa hasa na kikundi cha waanzilishi wa kike na kiume ambao walimchagua Kristo na msimamo thabiti  wa Injili na huduma kwa kindugu, hasa kwa maskini na walioachwa peke yao" na aliongeza kuwa "ni huduma hiyo hasa ambayo maisha ya wakfu yanaonesha umoja wa amri ya upendo, katika uhusiano usioweza kutenganishwa kati ya upendo wa Mungu na upendo kwa jirani"  (n.5).

Katika hati hiyo hiyo, maisha ya wakfu yalioneshwa kama picha ya kung’ara, ambayo inawezekana kufuata vipimo vyote vya kutafakari kwa moyo na pia kwa matendo ya maisha ya wakfu. Kwa kumfuata Yesu wakati wa kufunga nadhiri za mashauri ya kiinjili, watu waliowekwa wakfu wanaishi kutoka kwake na wanafurahia uhusiano wa karibu wa mchumba wao ambao kwa njia fulani unatangaza ufufuko (taz. Lumen gentium, n. 44). Katika Mtaguso wa II wa Vatican, kwa  maana hiyo, jukumu kuu la watu waliowekwa wakfu ni kukumbusha ubinadamu ule  uzuri wa Mbingu na hitaji muhimu ambalo sote tunao kwa hilo.

Kardinali Semeraro amefafanua umuhimu wa kutangaza watakatifu kwamba kwa kuwatangaza watakatifu inasaidia dunia, na sio Mbingu. Mtaguso wa Pili ulizungumzia juu ya wito wa ulimwengu katika utakatifu. Katika katiba kuhusu Kanisa pia ni sura kuu na nyenzo, ambayo siri ya Kanisa imefunuliwa (sura ya 1) na ambayo inadhihirishwa kabisa kwa Bikira mwenyeheri (sura ya 7). Kutangaza watakatifu kunasaidia kutuaminisha kuwa wito huu upo kweli,na kwamba Injili "inafanya kazi", kwamba Yesu hakatishi tama  na kwamba tunaweza kuamini Neno lake. Kazi yetu ya utambuzi katika mchakato mzima wa watakatifu haufanyiki hasa kwa kichwa au kwa hisia, bali kwa kupiga magoti, ambayo ni, kwa kuomba na kuomba nuru kutoka kutoka kwa Roho Mtakatifu. Watakatifu hawahitaji kutambuliwa kwetu, zaidi ya Mungu!  lakini tunapowathamini vile, tunatambua uwepo wa Mungu katikati yetu.

 

05 May 2021, 16:34