Tafuta

Vatican News
2021.03.31 Chano dhidi ya covid kwa maskini jijini Vatican. 2021.03.31 Chano dhidi ya covid kwa maskini jijini Vatican.  (Vatican Media)

Vatican:Jurkovič,janga limefundisha utegemezi wa familia ya binadamu

Mwakilishi wa Kudumu wa Vatican katika Shirika la Umoja wa Mataifa huko Geneva wakati wa hotuba yake amegusia mada ya ulazima wa usawa wa mgawanyo wa chanjo kati ya Kaskazini na Kusini mwa dunia,akinukuu maneno ya Papayasemayo“kadiri jinsi inavyabaki dharura ya ukosefu wa usawa wa mgawanyiko wa chanjo dhidi ya Covid-19, hatuwezi kuruhusu mitindo ya utaifa uliofungwa unaotuzuia kuishi kama familia ya kibinadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Afya ni faida msingi ya kawaida ya pamoja na hii ni moja wapo ya mafundisho msingi ya Covdi, ambayo kwa hakika ni masomo yake ya kushangaza ambayo yametoa mwanga mpya juu ya kutegemeana kama familia ya wanadamu. Ndivyo amesema Askofu Mkuu Ivan Jurkovič, mwakilishi wa kudumu wa Vatican katika ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Geneva, katika hotuba yake ya Mazungumzo Kimataifa juu ya uhamiaji katika Mashirika ya Kimataifa kwa ajili ya Wahamiaji. Askofu mkuu pia amegusia mada ya ulazima wa kuwa na usawa wa mgawanyo wa chanjo dhidi ya Covid-19 kati ya nchi za Kaskazini na Kusini mwa dunia, akinukuu maneno ya Papa Francisko yasemayo kuwa “kadiri jinsi inavyabaki dharura ya kuongezeka ukosefu wa usawa wa mgawanyiko wa chanjo dhidi ya Covid-19, hatuwezi kuruhusu kuwa mitindo ya utaifa uliofungwa wenyewe  na ambayo inatuzuia kuishi katika familia ya kweli ya kibinadamu" . Kwa sababu hiyo, Mwakilishi wa Vatican amezindua wito ili chanjo iweze kupatikana kwa wote na kurahisha mgawanyo hasa katika nchi zilizo maskini zaidi.

Haki, mshikamano na ujumuishwaji, kiukweli ni mambo matatu msingi wa mantiki ya kufuata ili kukabaliana na changamoto zilizotokana na janga kwa mujibu wa Vatican. Makubaliano ya ulimwengu kwa ajili ya uhamiaji salama, halali na uliopangwa vizuri unahitaji mataifa kuwa makini katika dharura za kiafya za wahamiaji katika sera za kisiasa na mipango ya kitaifa na katika utunzaji wa kiafya. Mkataba wa ulimwengu kwa wahamiaji, Askofu Mkuu Jurkovič anawaalika mataifa husika kuchangia rasiliami na ufundi kwa ajili ya kupanua na kuboresha mifumo ya kiafya kitaifa ili kurahisha upatikanaji wa wake kwa wahamiaji na jumuiya zinazowakaribisha. Askofu Mkuu aidha amebanisha jinsi gani ilivyo kwa bahati mbaya mara nyingi wahamiaji hawatambuliwi kama nao ni wenye haki kama wengine, kushiriki maisha ya jamii na kusahau kwamba nao wana hadhi sawa kama ilivyo za kila mmoja katika dunia hii. Ni jambo la kusikitisha sana, kwamba katikati ya janga, wahamiaji wengi wamekuwa zaidi waathiriwaa zaidi ya jinsi walivyokuwa mwanzo.  Ni wasi wasi mkubwa kwa wale ambao wanajikuta kwenye hali kama hiyo isiyo halali, na hofu ya kufungwa au kuhamasisha na mara nyingi hawana utunzaji wa kimatibabu.

Kwa hivyo, huduma ya afya inapaswa kupatikana na kwa bei rahisi kwa kila mtu, pamoja na wale walio katika mazingira magumu: Inapaswa kudhibitiwa kupitia sheria, sera na vitendo visivyo vya kibaguzi na vya kina, vinavyojikita katika asili ya watu na katika hadhi ya maisha ya mwanadamu katika kila hatua, ambayo ni, tangu kutungwa kwake, kupitia maendeleo yake na hadi mwisho wake wa asili, ameunga mkono sana askofu mkuu. Mwishowe, kutoka kwa mwakilishi wa Vatican uchambuzi juu ya mabadiliko ya tabianchi ukweli ambao unazidi kuchangia maamuzi ya mamilioni ya watu kuondoka majumbani mwao na kukabili hatari za kuhama makazi, basi kuna haja ya kuwa na shaka kidogo juu ya athari za mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira kwa afya. Kama vile Papa Francisko alivyosema, ulimwengu utaibuka kuwa bora au vibaya baada ya janga ikiwa wote tutwajibika. Kilicho na uhakika ni kwamba uhamiaji, kwa vyovyote, itachukua jukumu kubwa katika jamii zetu. Kwa maana hiyo, tukikumbuka mafunzo makubwa kutokana na janga hili, sasa ni wakati wa kutafakari tena vigezo vya kuishi pamoja kama wanadamu kupitia mtazamo wa ushirikiano na mshikamano.

28 May 2021, 14:50