Tafuta

Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Gabriel Randrianantenaina kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tsiroanomandidy, lililoko nchini Madagascar. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Gabriel Randrianantenaina kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tsiroanomandidy, lililoko nchini Madagascar.   (Vatican Media)

Askofu Gabriel Randrianantenaina Jimbo Tsiroanomandidy, Madagascar

Papa Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Gabriel Randrianantenaina kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tsiroanomandidy, lililoko nchini Madagascar. Askofu mteule Gabriel Randrianantenaina anatoka Jimbo Katoliki la Moramanga. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la Maaskofu Katoliki Madagascar. Alizaliwa 26 Februari 1969.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Gabriel Randrianantenaina kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki la Tsiroanomandidy, lililoko nchini Madagascar. Askofu mteule Gabriel Randrianantenaina anatoka Jimbo Katoliki la Moramanga. Hadi kuteuliwa kwake alikuwa ni Katibu mkuu mtendaji wa Baraza la Maaskofu Katoliki Madagascar. Askofu mteule Gabriel Randrianantenaina alizaliwa tarehe 26 Februari 1969 huko Tanambe. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 31 Mei 1997 akapewa Daraja Takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo Katoliki la Ambatondrazaka.

Kunako Mwaka 2006 Jimbo liligawanywa katika majimbo mawili naye akachagua kwenda kujiunga na Jimbo jipya la Moramanga. Tangu wakati huo, amejiendeleza zaidi katika masomo ya taalimungu na falsafa na kati ya mwaka 2003 hadi mwaka 2010 alikuwa Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana ambako alijipatia Shahada ya Uzamili, amewahi pia kuwa Mratibu wa Shughuli za Kimisionari Wilayani Anosibe An’Ala kati ya mwaka 2015 hadi mwaka 2016. Mratibu wa Miito kati ya mwaka 2003 – 2010 na Gambera kati ya mwaka 2010 hadi mwaka 2015. Kati ya Mwaka 2016 hadi kuteuliwa kwake kuwa Askofu alikuwa Jimbo, alikuwa ni Karibu mkuu mtendaji wa Baraza la Maaskofu Katoliki Madagascar.

Askofu mteule
01 May 2021, 15:52