Tafuta

Vatican News
2021.04.24 Margherita wa mji wa Castello, Italia 2021.04.24 Margherita wa mji wa Castello, Italia 

Watakatifu wa Kanisa:Margherita wa Castello kuandikwa katika kitabu cha cha watakatifu

Papa Francisko ameamua kumwema mtawa wa Italia Magerita wa Mji wa Castello katika orodha ya Wakatifu.Kati ya wenyeheri wajao,12 ni wafiadini waliouawa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Uhispania.Watumishi wa Mungu watano miongoni mwao ni daktari Emanuele Stablum na Enrico Ernesto Shaw aliyekuwa mkuu wa viwanda nchini Argentina.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Papa Francisko Jumamosi tarehe 24 Aprili 2021, amekutana na kuzungumza na Kardinali Marcello Semeraro, Raisi wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza Watakatifu, katika mazungumzo hayo, Papa Francisko amethibitisha hitimisho la kawaida la makardinali na Maaskofu kwa wajumbe wa Baraza na kutoa uamuzi wa kuandika  katika Kanisa la ulimwengu ibada ya Mwenye heri Margherita wa mji wa  Castello, Wa Shirika la tatu la Ndugu Wahubiri; alizaliwa kwenye 1287 huko Metola (Italia) kifo chake katika Mji wa Castello (Italia) tarehe 13 Aprili 1320, kuandikwa sawa swa katika kitabu cha watakatifu.  Vile vile katika mkutano huo Baba Mtakatifu ameridhia Baraza la Kipapa la Kuwatangaza watakatifu kwa wafiadini wafuatao Watumishi wa Mungu Vincenzo Nicasio Renuncio Toribio na wenzake 11 wa Shirika la Mkombozi Mtakatifu; waliouawa kwa sababu ya chuki ya imani huko Madrid (Uhispania), kunako 1936;

Fadhila za kishujaa za mtumishi wa Mungu Pietro Marcellino Corradini, Askofu wa Frascati, Kardinali wa Kanisa la Roma , Mwanzilishi wa Shirika la watawa wa Kike Collegine wa Familgia Takatifu; Alizaliwa tarehe 2 Juni 1658 huko Sezze (Italia)  na kifo chake Roma  (Italia)  tarehe 8 Februari 1743; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Emanuele Stablum na alikuwa ni Daktari, Mtawa wa Shirika la Wana wa Mkingiwa dhambi ya Asili: Alizaliwa tarehe 10 Juni 1895 huko Terzolas (Italia)  na kifo chake Roma (Italia) tarehe  16 Machi 1950;

Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Enrico Ernesto Shaw, Mlei mwaminifu na Baba wa familia na alikuwa ni mkuu wa viwanda; Alizaliwa tarehe 26 Februari 1921 huko Paris (Francia) na kifo chake huko Buenos Aires (Argentina)  tarehe 27 Agosti 1962;

Fadhila za kichujaa za Mtumishi wa Mungu María de los Desamparados Portilla Crespo,  Mlei mwaminifu na mama wa familia: Alizaliwa tarehe 26 Mei 1925 huko Valencia (Uhispania) na kifo chake huko Madrid ( Uhispania) tarehe 10 Mei 1996; Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Anfrosina Berardi, Mlei Mwaminifu; alizaliwa  tarehe 6 Desemba 1920 huko Mtakatifu  Marko ya Preturo (Italia) na kifo chake tarehe 13 Machi 1933.

24 April 2021, 18:21