Tafuta

Mtakatifu  Faustina Kowalska shuhuda wa Huruma ya Mungu Mtakatifu Faustina Kowalska shuhuda wa Huruma ya Mungu  

Papa Francisko atakuwa na wafungwa,wauguzi na wakimbizi katika sikukuu ya huruma!

Baraza la Kipapa kwa ajili ya Uinjilishaji Mpya imetoa taarifa kuwa Misa itakayoongozwa na Papa Francisko katika Kanisa la Roho Mtakatifu,Sassia katika Dominika ya Huruma ya Mungu tarehe 11 Aprili,watakuwepo wageni kutoka baadhi ya taasisi mbali mbali za huduma ya wafungwa,waguzi,watu wakimbizi kutoka Mashariki ya Kati na Afrika.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Uso wa huruma sio tu unaolezwa katika hati  ya “Misericordiae Vultus”,   ya Jubilei maalum ya  2016,  lakini pia ni kwa mtazamo halisi wa mfungwa ambaye alitolewa kosa lake kwa Mungu, la muuguzi aliyeombwa msaada wa kuokoa maisha, wa mlemavu ambaye anaomba faraja katika shida, wa familia ambayo kwa ajili ya ulinzi wake iliwasili katika nchi mpya kutoka Argentina. Hizi ndizo sura ambazo Papa Francisko atakutana nazo katika Misa ambayo inaadhimishwa Jumapili, tarehe 11 Aprili 2021 saa 10:30 katika Kanisa la Roho Mtakaifu, Sassia, karibu na Vatican kwenye tukio la Siku kuu ya Huruma ya Mungu.

Pia Wamisionari wa Huruma

Miongoni mwao pia ni wakimbizi vijana kutoka Siria, Nigeria na Misri, wakiwemo watu wawili wa Misri wa Kanisa la kikopti  na mtu wa kujitolea wa Siria wa Caritas wa Kanisa Katoliki la Kisiria. Kikundi cha wafungwa kutoka gereza la Regina Coeli, Rebibbia wa kike na Casal ya Marmo, Roma, vile vile watakuwapo baadhi ya watawa Huruma wanaofanya kazi katika Hospitali, uwakilishi wa wauguzi kutoka Hospitali ya Roho Mtakatifu, Sassia karibu na madhabahu hiyo. Pamoja na Papa kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka kwa Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya, Wamisionari mbali mbali wa Huruma wataungana, wakiwakilisha makuhani zaidi ya elfu moja, wa taasisi zilizoanzishwa wakati wa Jubilei ya Maalum, ambayo Papa aliwakabidhi utume unao unganishwa na maadhimisho ya sakramenti ya Upatanisho na mahubiri ya fumvo la huruma ya kimungu.

Misa itatangazwa moja kwa moja kupitia majukwaa ya Vatican News

Usomaji wa masomo watakuwa ni waseminari, wakati huduma ya liturujia itafanywa na vijana kutoka parokia nje kidogo ya Roma. Kwa kufuata sheria za kuzuia maambukizi ya Covid, mahudhurio ni madogo kwa watu 80. Misa Takatifu itatangazwa kwenye majukwaa yote ya Habari ya Vatican (www.vaticannews.va), na mtiririko mzima kwenye tovuti (www.divinamisericordia.it ) na kutakuwapo na huduma  kwa viziwi na watu wasiosikia kwa njia ya kutafsiri (LIS) lugha ya ishara.

10 April 2021, 18:14