Tafuta

Vatican News
Umuhimu wa wazee katika familia na makuzi ya watoto na vijana Umuhimu wa wazee katika familia na makuzi ya watoto na vijana 

Utume wa wazee kukaribia na kurithisha Imani kwa vijana

Kauli mbiu ya Siku ya Kimataifa ya babu na wazee inatoka katika kifungo cha Injili ya Matayo kisemacho“tazama,mimi nipo pamoja nanyi siku zote” itakayofanyika tarehe 25 Julai 2021 kama ilivyo wakilishwa tarehe 20 Aprili na Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha kwa waandishi wa habari.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Itakuwa ni Dominika tarehe 25 Julai 2021, ambapo itaadhimishwa Siku ya I ya Kimataifa kwa ajili ya babu na bibi na wazee.  Jumanne tarehe 20 Aprili imewakilishwa kwa waandishi wa habari Kauli mbiu iliyochaguliwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya siku hiyo na ambayo inatoka katika kifungu cha Injili ya Matayo kisemacho: “Mimi nipo nawe siku zote” (Mt 28,20). Ni kauli mbiu yenye lengo la kuonesha ukaribu wa Bwana na Kanisa katika maisha ya kila mzee hasa katika kipindi hiki kigumu cha janga.

“Tazama Mimi nipo pamoja nawe siku zote”, pia ni ahadi ya ukaribu na matumaini ambayo vijana na wazeee wanaweza kuoneshana kwa pamoja. Si tu wapwa na vijana, kwa dhati  ni mwaliko kwa wote kuonesha huo ukaribu katika maisha ya wazee, lakini pia hata wazee na bibi na mababu wanao jumumu na utume wa kiinjili, wa kutangaza, wa kusali na kurithisha kizazi cha vijana imani hiyo

Ili kuwezesha ufanisi wa  maadhimisho haya ya Siku ya Kimataifa, Makanisa mahalia katika hali halisi za vyama mbali mbali  kwa mujibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha wanabainisha kuwa katikati ya mwezi Juni, mwaka huu baadhi ya vifaa na ushauri vya kichungaji vitaweza kuwekwa kwenye tovuti yao: www.amorislaetitia.va.

20 April 2021, 15:45