Tafuta

Vatican News
Maandalizi kuelea siku ya Wazee ulimwenguni tarehe 25 Julai 2021:Kauli mbiu ni "na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.(Mt 28,20) Maandalizi kuelea siku ya Wazee ulimwenguni tarehe 25 Julai 2021:Kauli mbiu ni "na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.(Mt 28,20) 

Siku Wazee duniani:Mafundisho ya huruma kwa kizazi kuelekeza watu wadhaifu!

“Ninyi mpo pamoja nami siku zote” ndiyo uchaguzi wa kauli mbiu itakayoongaza siku ya wazee ulimwenguni,katika kilele chake tarehe 25 Julai ijayo.Uchaguzi huu unataka kuonesha nia ya mazungumzo kati ya vijana na wazee, na umuhimu wa kuridhesha imani kwa kizazi. Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha amethibitisha kuwa ni njia ya ufundishaji wa kuwa na huruma ya kuelekeza watu walio wadhaifu zaidi

Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

Mada iliyochaguliwa na Papa Francisko kuongoza Siku ya I ya Wazee ulimwenguni ni “Tazama mimi nipo pamoja nanyi siku zote”(Mt 28,20) itakayoadhimisha tarehe 25 Julai 2021, na ambayo inaweka umakini juu ya ukaribu na mazungumzo kati kizazi na wazee. Ni mada pendwa kwa Papa Francisko hasa kwa kile kinachohusu urithishwaji wa imani. Kauli mbiu hii bado inajionesha wazi na maana yake hasa katika wakati huu mgumu wa janga la covid ambapo, kuwasiliana moja kwa moja na watu, inakuwa vigumu na vizingiti ili kuweza kuwalinda watu wenye kuathiriwa zaidi kama wazee. Hata hivyo  ni hali fulani ambayo imependelea aina ya mafundisho ya kusikiliza kwa aliye mdogo zaidi, na ambaye amejifunza umuhimu wa kufanya uwepo wao uonekane kwa babu na bibi zao na wakati huo huo kwa kutaka kuimarisha mizizi ya historia ya familia yao, kama alivyoeleza Bi Gabriella Gambino, katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la  Walei, Familia na Maisha katika mahojiano na Radio Vatican.

Kwa mujibu wa Bi Gambino amesema mada  iliyochaguliwa ina maana nyingi. Zaidi ilichaguliwa na Baba Mtakatifu kwa sababu ni mada ambayo moja kwa moja inelezea wazo la ukaribu wa Bwana na Kanisa kwa babu na bibi na watu wazee. Kwa dhati  “ tazama mimi nipo pamoja nanyi”, ni kielelezo ambacho wote tunatamani kusikia kutoka kwa Bwana katika mioyo yetu na kwa kila hatua ya ugumu au kila hatua maalum ya maisha yetu, na zaidi kadiri umri unavyozidi kupita. Ujumbe hata hivyo pia una maana sana ya uzuri wa mazungumzo kati ya kizazi , cha  wazee na vijana. Ni ujumbe ambao wazee wanaweza kuwaelekeza vijana, ikiwa tunazingatia utume wa uinjilishaji, wa kutangaza imani ambayo wazee  wanayo na kutaka kuirudisha kwa upya. Vile vile Bi Gambino ameongeza kusema kuwa wazee wanalo jukumu lao. Hiyo ndiyo Mantiki ambayo Papa Francisko anasisitiza sana, lakini pia ni ujumbe ambao vijana wanapaswa kuwapatia bibi na  babu zao  na vile vile  wanaweza kuwapatia wazee wote. Kwa maana hiyo ya kusema  “tazama niko karibu nao, nitakuwa karibu nawe daima”. Na ujumbe huo baadaye ni namna ambayo inaweza kutusaidia hasa sisi kama Kanisa kushinda ile mipasuko kati ya kizazi cha leo hii ambacho kimemegeka mazungumzo na ili kuweza kurudisha mazungumzo hayo, amesisitiza Bi Gambino.

Akijibu swali la mwadishi nini maana ya kukaa karibu na wazee leo hii, amebainisha kwamba ina maana kwa hakika ya kuhamasisha matendo binafsi,  na ya jumla ambayo si tu  ya uchungaji wa ukaribu kwa bibi, babu na wazee katika familia na nje ya familia, lakini pia kwa mfano, katika wakati huu wa janga, “sisi sote  katika familia tumegundua upweke wa babu na babu zetu, wazazi wetu na wazee. Wakati mwingine, ukaribu umekuwa kweli ndani ya familia zetu hasa  ufundishaji wa kusikiliza, na kuwafanya watoto wetu kujua umuhimu huo , kwa mfano,wa kupiga simu kila siku kwa babu na bibi.  Bi Gambino amesema “Ni jinsi gani ni muhimu kujifanya mwingine ahisi uwepo  wa kila siku kwa babu na bibi  ambao wanaishi mbali, wanaoishi peke yao, ambao ni wajane na  juu ya yote hawaishi tena kama wenzi, lakini wako peke yao nyumbani. Kwa watoto wetu hii imeimaanisha sana kwa sababu swali la kila siku lilikuwa ni kwamba Je! Umesikia  babu anaendelea? Je! Ulifanya uwepo wako katika maisha yake? Hii inageuka kuwa tafsiri ya ufundishaji wa huruma, kama Baba Mtakatifu Francisko anavyosema, wa kusikiliza, wa kujifunza kumheshimu mwingine na kujiweka katika viatu vyake, au nafsini  mwake  hasa ikiwa ni mdhaifu zaidi.

Kwa kuzungumza juu ya uhusiano kati ya vizazi sio tu na ukaribu wa wadogo kwa wazee, wa wajukuu kwa babu na nyanya, lakini pia jukumu ambalo babu na nyanya wanaweza kuwa nalo katika ukaribu huu katika kurithisha  imani, Bi Gambino amesema hili ni muhimu sana. Babu na bibi wanaweza kuchukua jukumu kuu katika imani kwa wajukuu zao na watoto wadogo na sio tu katika usambazaji wa imani na uhusiano na Mungu, lakini pia katika uhifadhi wa kumbukumbu, maadili,  mizizi ambayo inaruhusu vijana kuelewa wao ni nani na wanatoka wapi. Swali maarufu la Mtakatifu Agostino linasema: “Ninatoka wapi na ninaenda wapi?”  Hili linahitaji vijana wetu kupata jibu pia katika mtazamo unaoelekeza kwa babu na bibi, na kwa wazee, ambao hutukumbusha sisi ni kina nani na tunatoka wapi. Hii ni muhimu sana na kwa hakika katika  mazungumzo ya imani ni muhimu sana leo hii katika mazungumzo ya vizazi vingi ikizingatiwa kuwa katika jamii isiyo na dini kama yetu, wazazi mara nyingi wanashindwa kuonesha na kurithisha mazungumzo haya ya imani kwa watoto wao.

Siku ya tarehe 25 Julai na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha watapendekeza baadhi ya zana za kichungaji kwa ajili ya kukaribia sana siku hii, na kwa maana hiyo Bi Gambina amethibitisha: “Kwa mfano, kutakuwa na maoni ya majimbo na Parokia ambazo zitatolewa kwa ulimwengu wote, na maoni na maombi ya waamini, familia na mahubiri. Kutakuwa na zana ndogo ndogo, kutakuwa na picha ambayo itapendekezwa kama mfano. Zana ambazo, kwa njia hiyo, zitafanya iwezekane katika ngazi mahalia ya  kusherehekea Siku hii katika jumuiya  zao. Na hii itakuwa muhimu sana, hasa katika wakati huu ambao bado janga linaendelea

21 April 2021, 16:22