Tafuta

Vatican News
2021.03.31 Chanjo dhidi ya Covid kwa maskini, Vatican 2021.03.31 Chanjo dhidi ya Covid kwa maskini, Vatican  (Vatican Media)

Apri 23 ni siku kuu ya Somo wa Papa:maskini wanapata chanjo ya pili

Katika siku kuu ya Mtakatifu George,watarudi mjini Vatican watu 600 wanaotarajia kupata chanjo ya pili dhidi ya Covid.Ni watu 1400 waliokwisha pata dozi za chanjo ambayo ni kama tone la upendo kwa mujibu wa Msimamizi wa Sadaka ya Papa Kardinali Krajewski,akifafanua kuhusu shughuli hiyo ambayo pia inaangukia katika siku kuu ya Papa Fracisko.

Na Sr.Angela Rwezaula -Vatican

Kurudi kwa upya katika moyo wa ukristo, karibu na nyumba ya Papa, katika siku ya somo wake Mtakatifu George ni jambo muhimu. Ni uzoefu ambao unawasubiri kundi la  watu maskini 600 ambao tayari kwa siku ishirini  zilizopita walipewa zawadi ya dozi ya kwanza ya kuzuia covid. Tarehe 23 Aprili wanatarajiwa kupata dozi ya pili ambayo itatolewa katika Ukumbi wa Paulo VI, Vatican mahali ambapo kuliandaliwa kituo cha chanjo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Sadaka ya Kitume inabinisha kwamba zaidi ya wale watakao pokea chanjo vile vile watashiriki siku kuu ya Somo wa Baba Mtakatifu kwa kupokea zawadi.   Hii ni ishara nzuri ambayo inajitokeza kwenye siku  kuu ya mwajina wa Papa yaani ya Mtakatifu George, kama  ilivyo jitokeza hata kwa miaka mingine, kwa mujibu wa Kardinali Konrad Krajewski msimamizi wa Sadaka ya Kitume. Katika fursa hii, Papa Francisko ameamua kutoa zawadi na siyo kupokea lolote kwa mtindo wa kiinjili.

Mnamo mwaka wa 2020, Papa alikuwa ametuma vifaa vya kupumulia nchini Romania, nchi ambayo ina shida hasa kwa sababu ya janga hili kama nchi nyingine zote. Katika miaka ya nyuma hata hivyo alikuwa amewapa  elfu sita za rozari zilizotengenezwa wakati wa Siku ya Vijana Duniani huko Panama kwa vijana wa Jimbo Kuu Katoliki la Milano na yai la chokoleti la kilo 20 kwa maskini katika kantini ya Caritas ya  Kituo cha Reli cha Termini Roma, wakati wa siku kuu kama hii.

Chanjo kwa wanaume na wanawake  wenye umri zaidi  ya 60, na shida kubwa za kiafya na shida katika kupata vituo kwenye vituo vya kitaifa nchini Italia, ilianza mwishoni mwa mwezi Januari. Baadaye  kampeni ilianza tena wakati wa Wiki Takatifu na chanjo ya kwanza ya walio hatarini zaidi walikuwa ni  wageni wa mabweni yanayosimamiwa na Watawa wa Mama Teresa, wengine wakisaidiwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, vilevile chama cha  Mshikamo wa madawa kinachosimamiwa na Kliniki ya Mama wa Huruma kilicohpo Vatican karibu na Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Mpango wa Msaada wa Kitume,na chanjo iliyotolewa kwa watu 1400,  ni tone la upendo kwa mujibu wa  Kardinali Krajewski, na ambao ni wito wa Baba Mtakatifu Francisko kuwa hakuna mtu yeyote atengewe kwa sababu ya wazo hili la chanjo. e Hata hivyo kupitia tovuti ya Sadaka ya kitume inawezekana kutoa zawadi ya chanjo kwa maskini www.elemosineria.va, wale ambao ambao hawaonekani katika mitaa na miji yetu.

Shukrani kwa kampeni hii, euro 100,000 zimetumwa kwa Kardinali Mario Zenari ,Balozi wa Kitume nchini Siria , kwa ajili ya  ununuzi wa chanjo. Kwa mujibu wa Padre  Augusto Zampini, Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya binadamu na mjumbe wa Tume ya Vatican ya Covid-19, ameelezea matumani yake  kuhusu uchangiaji huo ambao utaweza kutuma hata msaada katika maeneo mengine ulimwenguni kwa kuchangia ma kuharakisha kampeni ya chanjo. Hii ni moja ya vipaumbele vitatu vya Tume yao kwa mwaka 2021: afya kwa wote, chakula kwa wote, na kazi kwa wote”.

22 April 2021, 15:08