Tafuta

Vatican News
WOSIA WA KITUME WA AMORIS LAETITIA,UMEFIKISHA MIAKA 5 TANGU KUCHAPISHWA KWAKE 8 APRILI 2016 WOSIA WA KITUME WA AMORIS LAETITIA,UMEFIKISHA MIAKA 5 TANGU KUCHAPISHWA KWAKE 8 APRILI 2016 

Padre Mello,Amoris Laetitia ni barua ya Papa ya upendo kwa familia

Mipango mbali mbali inaendelea kwa ajili ya kukumbuka miaka 5 tangu kwa Wosia wa Kitume wa Papa Francisko huchapishwe mnamno 8 Aprili 2016.Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei,Familia na Maisha akizungumza katika Kipindi cha Radio Vatican na Ninyi”,amesema kuwa ni hati ambayo inastahili kuwa kiini cha familia katika jamii na katika Kanisa.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Wosia wa Amoris Laetitia wa Papa Francisko uliotiwa saini mnamo tarehe 19 Machi 2016 na kuchapishwa mnamo tarehe 8 Aprili mwaka huko, ambao unahusu upendo katika familia ni tunu la tafakari ya Papa Francisko na maaskofu wa Kanisa kwa njia ya Sinodi mbili ya kwanza mnamo 2014 ambayo ilikuwa maalum kuhusu “Changamoto za uchungaji wa familia” katika muktadha wa uinjilishaji na Sinodi ya 2015 iliyokuwa inahusu “Wito na Utume wa familia katika Kanisa na ulimwengu mamboleo”.  Katika fursa ya kukumbuka miaka mitano ya kuchapishwa kwake kwa maana hiyo ni fursa ya kuchukua na kutazama wigo wa waraka huo muhimu wa kipapa na mipango iliyopangwa kwa mwaka huu, kwa mujibu wa Padre Alexandre Awi Mello, Katibu wa Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha akizungumza kwenye Kipindi cha “Radio Vatican na Ninyi”.

Padre Alexandre Awi Mello amesema kuwa “Baada ya Wosia wa Evangelii gaudium, yaani Furaha ya Injili, na  ambayo ni mpango mzima wa upapa wa Papa Francisko, mada kuu ya kwanza ambayo Papa alitaka kuizungumzia ilikuwa hasa familia. Aliitisha Sinodi mbili ili kuweza kutafakari kwa kina mada hii na kupendekeza njia thabiti za kichungaji. Tangu mwanzo Papa alikuwa anajua sana umuhimu wa familia katika jamii na kwa Kanisa. Familia inayokaribisha maisha, inayofundisha vizazi, inayopitisha na kurithisha imani, na maadili kwetu, ambayo hujenga jamii kutoka ndani. Kwa maana hiyo ilikuwa muhimu sana tangu mwanzo kutafakari na maaskofu wa ulimwengu wote juu ya mada hii ambayo imekuwa na nafasi kuu katika upapa wake. Sasa maadhimisho ya mwaka wa tano ni fursa ya kurudisha familia katikati ya umakini wa kichungaji wa Kanisa” amesisitiza Padre Awi Mello.

Akielezea juu ya mapokezi ya wosia huu katika nchi mbali mbali hasa katika familia za kikatoliki ulimwenguni na hasa katika kujikita kwenye matendo  ya dhati kufuatia na uzoefu wake, Padre Awi amesema: “Mapokezi ya Amoris Laetitia yamekuwa tofauti sana ulimwenguni kote. Majimbo mengi na mikutano ya maaskofu mara moja waliipokea vizuri sana. Walibadilisha mipango yao ya kichungaji, na kuacha waongozwe na maoni na mapendekezo yake. Na wengine kiukweli kidogo na katika maeneo mengi lengo hasa lilikuwa kwenye sura ya VIII inayohusu udhaifu wa familia. Kwa hali yoyote, ni kweli kwamba familia nyingi zinajua, lakini hakika haijulikani kwa familia nyingine nyingi pia. Na ni dhambi kwa sababu hii ni hazina kwa familia”.

Maneno ya Papa yanakusanya kila dhihirisho la zaidi ya miaka miwili ambayo Kanisa na maaskofu wote, kuanzia na baraza ya maaskofu. Hatimaye Papa aliandika barua ya upendo kwa familia, kwa maana hiyo maadhimisho ya mwaka wa tano tangu kuchapishwa ni fursa nzuri ya kuvuta  kutoka kwenye droo barua hii ya upendo, na kuisoma tena, kuendelea na ushauri wake kwa vitendo, kwa sababu Papa anafanya vitendo kama ilivyo tabia yake. Wosia unakwenda katika maelezo ya maisha ya familia: jinsi ya kukuza upendo na katika kuondokana na na shida za kweli, na mateso ya familia. Kutumia tafakari ya kichungaji ya ushauri  wa  kitume pia ni fursa nzuri.

Hata hivyo Amoris laetitia, na familia ni fursa ya kutembea pamoja kiukweli bila kusahau, kuzinduliwa kwa  waraka huu, katika mwaka wa familia Amoris Laetitia  ulioanzishwa wakati wa sherehe ya Mtakatifu Yosefu na  katika mpango ambao unaendelezwa mbele wa Baraza hili kwa ushirikiano na Vatican News na Baraza la Kipapa la Mawasiliano., Ambayo kila mwezi kwa vipindi 10 kutakuwa na video na tafakari za Papa na ushuhuda wa familia kutoka ulimwenguni kote. Katibu wa Baraza amefafanua kuwa “Ni mpango mkubwa sana na sisi kama Baraza la Walei tutakuwa na mipango mingine kama hii, nzuri sana, ya safu ya video kwenye familia. Pamoja na video ambazo zitachapishwa kila mwezi kutakuwa pia na mafundisho  ya kazi ya kichungaji katika familia na kwa hiyo itawezekana kufanya kazi pamoja kama wenzi, kama familia hata katika parokia, kwa vikundi na wanandoa wengine”. Vile vile amesema

Kwa maana hiyo ni msaada mzuri sana kutumia na kujifunza zaidi juu ya wosia ,kuanzia na maneno ya Papa pia kutoka kwa ushuhuda wa familia, lakini pia kutakuwa na mipango mingine ya kuanzishwa kwa mfano kuna Siku ya Wazee, bibi na babu ambayo itafanyika katika Dominika ya nne ya Mwezi Julai na Siku Kuu ya Watakatifu Johakimu na Anna Bibi na babu yake Yesu. Na mipango mingine   kwa mfano, jukwaa ambalo tutakuwa na mwaka huu na wale wanaohusika na huduma ya familia kutoka ulimwenguni kote na pia njia kumi na mbili ambazo tunataka kupendekeza familia kutekeleza Amoris Laetitia. Programu hii yote inaweza kupatikana kwenye tovuti yetu ya www.amorislaetitia.va. Kwa maana hii, mabaraza ya maaskofu, parokia, majimbo  pia wamealikwa kuchukua mipango, kama hiyo sio kwamba tutafanya kila kitu. Hapa kuna rasilimali ambazo tunataka kutoa ili kukuza wosia wa Kitume. Hakika jambo muhimu zaidi litatokea katika kila jimbo na katika kila parokia. Wito ni kwa familia na pia kuhamasisha makuhani wa parokia na maaskofu wao kuchukua fursa hizi ambazo Papa anatupatia kusoma tena na kugundua uzuri wa himizo hili la kitume.”

10 April 2021, 10:50