Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Armando Matteo kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Armando Matteo kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. 

Padre Armando M. Katibu Mwambata Mafundisho Tanzu ya Kanisa

Padre Armando Matteo alizaliwa tarehe 21 Septemba 1970 huko Cantanzaro, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 20 Desemba 1997 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Cantanzaro-Squillace. Alijiendeleza zaidi katika masomo ya falsafa na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha “Sacro Cuore” Jimbo kuu la Milano.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S.  – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amemteua Mheshimiwa Padre Armando Matteo, kuwa Katibu Mwambata wa Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Padre Armando Matteo, kabla ya kuteuliwa kwake amekuwa ni Jaalimu wa Taalimungu Msingi, Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbaniana na Mkurugenzi wa Jalida la Chuo Kikuu cha Urbaniana: “Urbaniana University Journal”. Itakumbukwa kwamba, Padre Armando Matteo alizaliwa tarehe 21 Septemba 1970 huko Cantanzaro, Italia. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi, tarehe 20 Desemba 1997 akapewa Daraja takatifu ya Upadre kwa ajili ya Jimbo kuu la Cantanzaro-Squillace. Alijiendeleza zaidi katika masomo ya falsafa na hatimaye kujipatia Shahada ya Uzamili, Chuo Kikuu cha “Sacro Cuore” Jimbo kuu la Milano.

Padre Armando Matteo alibadilisha mkondo na kujinga na masomo ya taalimungu, na hatimaye, akajipatia Shahada ya Uzamivu toka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, Roma. Katika maisha na utume wake wa Kipadre, ametekeleza kazi mbalimbali Jimboni mwake. Kati ya Mwaka 2005 hadi mwaka 2011, aliteuliwa kuwa Mratibu wa Kitaifa wa Shirikisho la Vyuo Vikuu vya Kikatoliki nchini Italia, (Ecclesiastico Nazionale della Federazione Universitaria Cattolica Italiana, FUCI). Kunako mwaka 2012 aliteuliwa kuwa Mshauri wa Kitaifa wa Shirikisho la Walimu Wakatoliki Nchini Italia (Nazionale dell’Associazione Italiana Maestri Cattolici, AIMC). Ni Jaalimu wa Taalimungu msingi na mwandishi mbobezi wa vitabu na makala katika masuala ya Kitaalimungu.

Katibu Mwambata
12 April 2021, 15:20